Itanigharimu kiasi gani kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti?

Dec 8, 2021
25
55
ITANIGHARIMU KIASI GANI KUTALII KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI?
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa ufafanuzi kwa wale wanaotamani kwenda kutalii lakini hawajui itawagharimu shilingi ngapi.

Gharama ya kutalii mara nyingi inabadirika kutegemeana na sababu mbalimbali kama vile...

Kampuni utakayotaka kutumia, upatikanaji wa gari(kama ni gari binafsi au ya kukodi), chakula, na malazi endapo utapenda kulala hifadhini.

Kwa ufupi tu makadirio ya upesi kwa kundi la watu 2 hadi 5 itagharimu kuanzia laki 5 kuendelea kwa safari ya siku moja (Day Trip). Na kwa kundi la watu 6 hadi 12 itagharimu kuanzia laki 6 na kuendelea. Kama safari itahusisha kulala hifadhini gharama zinaweza ongezeka kutegemea na endapo utachagua kulala lodge, campsite au hostel.

Endapo pia utatumia gari binafsi gharama zinaweza kupungua Hadi kufikia shilingi laki 2-3 kwa kundi la watu 2 hadi 5.
Kumbuka: Gharama zinahusisha kiingilio Cha HIFADHI, chakula, muongoza watalii na tozo ya gari.

KAMA UNA SWALI LOLOTE TAFADHARI ULIZA NA NITAKUJIBU HAPAHAPA!
Kwa wakazi wa mikoa ya kaskazini, pwani na kati kama vile Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Tanga, Pwani n.k wanaweza kwenda Hadi Arusha au Moshi na kuzungumza na kampuni za watalii zinazopatikana maeneo hayo.

Kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa inapendeza zaidi kuanzia safari yao katika mji wa Mugumu kupitia geti la Tabora-B au Ikoma na kumalizia katika geti la Ndabaka.
Binafsi napatikana katika mji wa Mugumu, Wilayani Serengeti.
Asante!


FB_IMG_16389600333263825.jpg
 
Me nataka nije na my wife wangu. Je muda gani mzuri nita enjoy sitaki kuwe na wazungu wengi.

Kila kitu juu yenu kuanzia gari. Safari ya kulala usiku mmoja. Sasa sijui tofauti ya camps

Hizo gharama ni kuanzia getini au hata nikiwa Njombe gharama ni hizo hizo?
Gharama hizo ni za kuanzia mji uliopo jirani na HIFADHI. Hivyo basi kwa Serengeti jirani zaidi ni mji wa Mugumu. Kwa wewe uliepo Njombe itapendeza zaidi ukisafiri kwa basi Hadi Arusha Kisha Karatu ndipo uanzie safari ambapo utapita Kwanza Ngorongoro ndipo ufike Serengeti. Au unaweza pia kusafiri hadi Mwanza Kisha upande basi Hadi Mugumu ndipo uingie Serengeti.
 
Me nataka nije na my wife wangu. Je muda gani mzuri nita enjoy sitaki kuwe na wazungu wengi.

Kila kitu juu yenu kuanzia gari. Safari ya kulala usiku mmoja. Sasa sijui tofauti ya campsite hostel na lodge.
Muda wote utaenjoy. Kuanzia mwezi wa sita Hadi wa kumi na Moja ndipo Kun wazungu wengi. Lakini siyo maeneo yote ya HIFADHI kwani Serengeti ni kubwa sana ni vigumu kuitembelea yote Kwa siku moja. Mara nyingi wazungu wqnapenda kufuatilia uhamiaji wa nyumbu, kwahiyo inawezekana kuitembelea maeneo mengine ambapo kunakuwa hakuna nyumbu kwani watu wanakuepo wachache.
Gharama ya kulala hostel ni 5600 Kwa usiku ila inakua kama bweni mnalala watu wengi, lodge gharama zinaanzia 20,000 Hadi 1,000,000 na campsite gharama hazitofautiani sana na za lodge.
Kwa safari ya siku moja Kwa budget ya kawaida andaa angalau kuanzia 800,000.
Karibu sana, unaweza nicheki Kwa namba hii nikupe muongozo zaidi....0625818341.
 
Ahsante Sana mkuu,nataka bike kutarii na familia yangu ya watu watatu,baba na mama pamoja na watoto wawili wa chini ya miaka mitano, nitala siku moja

Gharama yake ni shilingi gapi ?
Umemaanisha jumla ni watu saba?
Kwa watoto chini ya miaka mitano hawalipii kiingilio hivyo basi gharama zao zitakua chakula na usafiri.
Kama mtapendelea kulala ndani ya HIFADHI gharama zitaanzia shilingi laki nane (800,000).
KAma mtalala nje ya HIFADHI gharama zitakua kati ya laki sita Hadi saba (600,000-700,000).
Kumbuka nje ya HIFADHI gharama za lodge nzuri tu za kawaida ni kuanzia elfu kumi na Tano.
KAribu sana mkuu Serengeti.
 
Toa mchanganuo, gharama za kuingia hifadhi kiasi gani, usafiri ukikodi kwa siku kiasi gani
NItafafanua gharama za kuingia hifadhini kuanzia saa 12 asubuhi Hadi saa 12 Jioni (yaaani day trip) pamoja na Aina za usafiri na gharama zake kama ifuatavyo.

1. Kwa kutumia gari Aina ya LAND CRUISER inayofunguka juu (OPEN ROOF) na inayobeba Hadi WATU WANNE(four passenger seats) gharama ni shilingi 560,000/=. Gharama hizi zinahusisha kukodi gari, mafuta, Kodi ya gari inapoingia hifadhini, chakula Cha asubuhi na mchana, kiingilio Cha watu 4.
Mkiwa kikundi Cha watu 4 hapa Kila mmoja atalipia angalau 140,000/=.

2. Kwa kutumia gari Aina ya LAND CRUISER inayofunguka juu (OPEN ROOF) na inayobeba Hadi WATU SITA (six passenger seats) gharama ni shilingi 700,000/=. Jumla ya watu hapa mtakua 6, endapo mtakua pungufu gharama zitapungua kidogo kwenye chakula na kiingilio hifadhini. Kwa kawaida kiingilio ni shilingi elfu kumi na mbili (12,000/=) Kwa mtu mzima kuanzia miaka 16. Watoto chini ya miaka 5 ni bure. Wastani gharama ya chakula Kwa mtu mmoja ni shilingi elfu kumi (10,000/=) Kwa breakfast na lunch.
Mkiwa kikundi Cha watu 6 hapa Kila mmoja atalipia angalau 120,000/=.

3. Kwa kutumia gari Aina ya HIACE inayobeba Hadi WATU 7 HADI 12 gharama ni shilingi 750,000/=. Hapa mnaweza kuwa kikundi Cha Hadi watu 12, endapo mkiwa pungufu gharama zinaweza kupungua kidogo kama nilivyoelezea hapo juu.
Mkiwa kikundi Cha watu 12, hapa Kila mmoja atalipia angalau 65,000/=.

4. Kwa kutumia gari Aina ya COASTER AU TATA inayobeba wastani wa WATU 13 HADI 30 gharama itakuwa ni shilingi 1,500,000/= (milioni Moja na nusu). Mkiwa pungufu ya idadi hiyo gharama itapunguza kidogo pia.
Mkiwa kikundi cha watu 30 hapa Kila mmoja atalipia angalau 50,000/=.

5. Kwa kutumia gari Aina ya NOAH inayoweza kubeba WATU 2 HADI 6 gharama itakuwa shilingi 450,000/= (laki nne na nusu).
Mkiwa kikundi Cha watu 6 hapa Kila mmoja atalipia angalau 75,000/=.


Kumbuka Gharama hizo ni Kwa jumla na zinabadirikabadirika kutokana na Aina ya gari utakayopenda kutumia. Land Cruisers zinazofunguka juu zinafaa zaidi kwani zinanafasi ya kutosha ndani, madirisha makubwa na zinafika popote ndiyo maana zinagharama kubwa kukodi.

Endapo una gari binafsi utagharamika kununua mafuta ambayo yatatosha kuzungumza angalau 300km. Pia utalipia tozo ya gari kutokana na uzito wake. Gharama nyingine utakazolipa ni za kiingilio kutokana na idadi ya watu utakaokuwa nao na pia utamlipa muongoza watalii (tour guide) Ili akupeleke maeneo wanapopatikana wanyama Kwa urahisi. Gharama za tour guide Kwa siku inategemea a ila Kwa wastani ni shilingi elfu hamsini (50,000/=).
Chakula unaweza andaa chako au ukanunua nje ya HIFADHI kupunguza gharama.

Karibu sana mkuu, unaweza nicheki nikakupeleka wakati wote.
Mnaweza ungana mkawa wengi Ili kupunguza gharama ya mmojammoja.
 
Me nataka nije na my wife wangu. Je muda gani mzuri nita enjoy sitaki kuwe na wazungu wengi.

Kila kitu juu yenu kuanzia gari. Safari ya kulala usiku mmoja. Sasa sijui tofauti ya campsite hostel na lodge.
Naunga mkono swali hilii
 
Back
Top Bottom