Siku Zote Mahusiano Hukupa Upofu na Kukuaminisha kuwa Sehemu ulipo ni Sahihi bila kutambua kuwa Moyo Wa Mtu ni Msitu.
Unaweza ukaamini unapendwa kwa Asilimia zote lakini kumbe katika Moyo Wa mwenzako hakuna Kitu kama Hicho.. Anakuchukulia wewe kama Chombo Cha kumstarehesha na Siku Ambayo Utakuja Kugundua ukweli na hapo ndip utakapoamini kuwa Haya tunayosema ni Sahihi.
Kwenda kujiaminisha kwa Mwanamke/mwanaume na kuonyesha mapenzi yako yote basi jiandae Ama kwa kudharauliwa na Hata kulizwa.
Mbinu hii nimeipokea na nitajitahidi kuitumia tatizo penzi la kweli halifanyiwi na wala halina Majaribio
Mkuu ulimwoa au ulimchumbia? Hebu funguka bana nimejifunza mengi hapashem ungeingia ndani ya moyo wangu nakujua nilichokibeba nadhani ungenishangaa kwanini naandika haya. Nimepanda Upendo wangu kwenye Mwamba ambao kamwe hakuna mmea ulio na uwezo wa kumelea..
Nikajitia upofu wakutokuona kila nilichotendewa. Niliziba masikio kwa ndugu na marafiki nikiamini kuwa nalinda penzi la mke wangu mtarajiwa lakini sikujua kuwa nilikuwa nikiuingiza Moyo Wangu kwenye moto.. Moto Ambao Umeniunguza na Kuufanya Moyo Wangu upoteze ule Ujasiri Wake..
Nililia sana, nilisimangwa sana, nilitukanawa na kuitwa majina ya kila aina lakini Yote hiyo kwa sababu nilimpenda, nilimjali na Kumthamini.. Sikutaka kumuoma Akilia lakini mimi alinifanya nilie. Sikutaka kumuona akiteseka, lakini akaniacha mimi katika mateso Makali... Hakika kuna mengi ambayo niliwaza mengi lakini sikuwa na thamani tena shem ila Mungu ni Mwema Kwangu..
Bado naishi lakini maisha yenye kumbukumbu mbaya sababu ya Mapenzi....
SIHITAJI KUPENDA TENA WALA KUPENDWA.. HIKI NINACHOPITIA SITAKI NISABABISHE MWINGINE AKIPITIE.. MOYO WANGU
Mkuu ulimwoa au ulimchumbia? Hebu funguka bana nimejifunza mengi hapa
alikuwa ni mchumba na alikuwa akitambulika kwetu nami nilikuwa nikitambulika kwao.. Sikuwahi kuhisi kama Angeondoka katika maisha Yangu na Kuniacha katika Maumivu makali Sana... Niliwahi kupenda lakini nadhani kwake Upendo ulipitiliza... Naishi kwenye furaha na nafurahia maisha nikiwa Ibrah mpya na mwenye mipango mikubwa
Ni mengi yaliosababisha lakini kubwa kabisa ni kudanganywa na familia yake na kuamua kuvunja ahadi na uchumba bila kunitaarifu mimi kisha kumuondoa hapa nchini
Pole sana mkuu. Nimeifuatilia story yako na imenigusa sana tena sana.
Nimeshapoa mkuu ingawa nimeingiwa na hali ambayo bado sijajua itaniisha lini.. Nachukia mapenzi, nachukia kupendwa na nachukia mahusiano... Mpira ndio mpenzi wangu na Jf ndio mchepuko wangu
Yeah! Alikuwa ikidate na mwanaume mwingine wakati nipo chuo na huyo mwanaume ndio anayeishi nae mpaka leo Huko Canada
Mkuu hamna kitu inauma kama kuwa betrayed like that. Labda nikuulize ulikuja kujua vipi?
Pole sana
Yeah! Alikuwa ikidate na mwanaume mwingine wakati nipo chuo na huyo mwanaume ndio anayeishi nae mpaka leo Huko Canada
Duh pole aiseee, watu huwa hawaelewi kwa nini watu wapo single ili hali hawana kipingamizi chochote. Wasichokijua ni maumivu yaliyojificha ndani ya mioyo yao kwani huwa wanatabasamu kwa nje lakini mioyo yao inalia.
Kuumizwa na uliyempa uhai wako ni janga kwa kweli. Kuna kale kamsemo kanasema some people are alive because its illegal to shoot them.......
Mkuu hayo ni mazito! Ina maana baada Ya kujua hauko mwenyewe bado ukaendelea kuwa nae hoping atabadilika?
nimekuja kugundua nikiwa nimeshachelewa na Ulikuwa mpango Mahsusi Uliyopangwa ili nifanye maamuzi. Na nilipomwambia tu ilikuwa ni kama Kumpa nafasi... Nilitukanwa na kudharauliwa sana mwisho nikaambiwa huna hadhi ya kuishi na binti yetu.. Maumivu niliyoyapata Siku Hiyo Mungu alikuwa Shahidi... Nililia karibia miezi miwili.. Nilifanya mitihani Yangu huku nikilia.. Sikushangaa nilipodisco kwa kweli sipendi kulikumbuka hili
Moja kati ya njia salama za kumuacha mpenzi wako ni kumuacha huku ukiwa na sababu iliyo wazi au watu waliosababisha.
Yaan kama stori ipo kama ilivyo, silioni kosa la mpenzi wako bali ni mazingira yanayomzunguka(ndugu)(wazazi).huyu alikupenda ila msimamo au maamuzi yake yalitegemea wengine wanatakaje.
Nina imani hata wewe una maumivu ya kawaida tu, sababu unajua mpenzi wako aliondoshwa akaolewe kwingine kwa shinikizo.ila unachukia mapenzi sababu hukuwahi kujiandaa au kufikiria hii.
Mapenzi yanauma zaidi uachwe bila sababu bana, afu unaachwa anayeoa/olewa mko sawa au umezidi muonekano hata status ya maisha.huu ndio wakati ambao mtu huwa anaua au kujiua mwenyewe.cha msingi hapo mkuu kwanza shukuru yaan kwa yaliyonikuta naona kama unajifunza hivi.
Afu usichukie mapenzi wala wanawake utaumiza malaika wa watu bure waliofundwa wakaelewa.cha msingi chukua muda kuusoma huu mchezo unaoitwa mapenzi.utaelewa kitu.
Ukiwa na tabia ya kutibuka nyongo utajikuta nje ya geti kila siku wakati watu wanasherehekea ndani.maana hata wakati wa kutafuta mpenzi wa kweli kuna mitihani yote hii unayolalamikia hapa, ni safari.......safari ndefu.