Italy nchi nzuri pengine kupita zote duniani

Kaka ukiitaja Italy nachanganyikiwa. Mimi naipenda sana timu yao ya Taifa the Azzuri. Siku Ile Baggio anakosa penati na Brazil niliumwa. Mbaya zaidi unapoutaja mji wa Torino au Turin kule Fiat zinapotengenezwa! yule bibi kizee wa Torino anakotokea. Juventus klabu yangu pendwa the Bianconeri Forza Juve! Kwa nini nisipate mvinyo niongeze maisha?
Mmh mbona mnasifia nchi za watu namna hii kweli!!?
 
Ni kweli, Italia ikiwa moja ya nchi za mediterranean ina ardhi yenye mimea ya kijani inayovutia kwa macho. Miundombinu ya barabara zake zilizojengwa kiustadi kupita kwenye milima na mabonde ni kitu ambacho mtalii yeyote hawezi kukosa kukiona na kukitaja katika simulizi yake.

Jiji la Roma ndio mji wangu la kwanza kukanyaga kwa mara ya kwanza ndani ya bara la ulaya. Kabla ya kuruhusiwa kutua, tulilizunguka jiji kwa dakika 20 na kupata fursa ya kuona madhari ya jiji hilo na pemezoni kutokea angani. Masaa 16 niliyosubiri kuunganisha safari, yalitosha kabisa kujifunza kwa haraka kuwa watariano hawana kabisa ile kitu tunaita ubinadamu hasa kwa mwafrika.
 
Sheria zao kwasasa ni Kali kwasababu ya wimbi la wakimbizi kutoka nchi za afrika kaskazini ila fursa kubwa huku kwa cheap labor ya waafrika ni viwandani ngoja nikipata muda nitafafanua hasa italia ya kaskazini ndio kwa matajiri na ndio kwenye fursa
Usiache kutupa Fursa za huko ukipata wasahaa.
 
Ni wabaguzi sana hao wataliano hadi wanaweza wakakutemea mate ngozi nyeusi japo sio wote wana tabia hiyo ila wengi wao. Madem zao watamu kinoma noma na ukimkuna vilivyo lazima akahadithie wenzie
 
Nimekaa miaka sita kwenye Hii nchi hakika ni nchi nzuri mnoo geographical location yake ni katikati ya ulaya watu wake ni wachapa kazi ila pia wapenda starehe mnoo dini kuu ni Roman Catholic

nchi Hii ina hazina ya historia ya kale iliyohifadhiwa vyema pengine kuliko nchi yoyote duniani pia miji yake ina ustaarabu wa kale kuliko nchi yoyote ya ulaya

Jaribu kutembelea miji Hii utaamini nisemayo

Turin
Milan
Genoa
Rome
Cicily

Kisiwa cha Cicily ndipo kundi la mafia lilizaliwa
Miaka sita niliyokaa italia nimejifunza mambo mengi umaskini upo hasa kusini ila kwa ujumla ni nchi tajiri yenye viwanda vingi vikubwa

Waitalia wanapenda Sana ngono hata viongozi wa serikali wanakumbwa Sana na haya makashfa ya ngono rejea kashfa ya dungadunga ya waziri mkuu tajiri Silvio berluscon angalau Romano prodi alikuwa ametulia ukifika Roma usisahau kufikia piaza navona

Karibuni italia
Nilitegemea mswahili kama wewe mwisho wa siku utasema karibu zanzibar au kilimanjaro kwa hao waitaliano lakin nothings at all?? unatupa habari za watu wanapenda starehe sijui madudu gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afrika Kusini (kwa Madiba) nako ni maskini?
Kusini sijui kuna nini? Kila kusini ya nchi yoyote ndio wananchi wake huwa masikini.
Tanzania.
Sudani
Uganda
Kenya
Malawi
N.k
Mikoa yake ya kusini ni masikini

oooooops!
 
Back
Top Bottom