Itakuwa tarehe 15/10/2013 niombeeni Waungwana.

Itakuwa tarehe 15/10/2013 niombeeni Waungwana.

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,773
Habari zenu wakuu,
Kama hakutakuwa na mabadiliko hiyo ndiyo tarehe ninayotarajia kufunga ndoa
kila kitu kinaenda vema, najua ni vigumu kuchangia fedha n.k lakini ni rahisi
kushiriki kwa hisia. Naomba muelekeze maombi yenu kwangu niweze kufanikiwa
katika jambo langu hilo kwani ingawa hatuonani wengi wenu humu nimekuwa
nikiwahi kama ndugu au jamaa, ndio maana hata ninapotoa taarifa hii najisikia
faraja kubwa sana.

Ahsanteni.
 
Mkuu hongera sana!
Mungu akujaalie ndoa bora!
...
Kwa msaada tu Zama ktk thread alizoanzisha Himidini, takriban zote lakini hasa hasa ktk thread yake 1 (jina nimeisahau) ameelezea vizuri sana kuhusu siku za mwanzo ambazo wanandoa hufurahia penzi zito ambalo haliwezi kuendelea kutokana na mfumo wa maisha.
Akaendelea kuelezea ni vipi munatakiwa kukabiliana na hiko kipindi cha pili kinachotazama maisha zaidi kuliko mapenzi!!!
...
Nakutakia ndoa njema!
 
Mkuu GAZETI hongera sana kwa uamuzi huo na Mungu akutangulie jatika safari yako hii
Muombe Mungu aanze na wewe katika maisha haya ya unyumba na akuongoze katika safari hii unayoenda kuianza
Umeamua na umechagua fungu jema nakutakia kila la kheri mkuu
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana kwa hatua uliyofikia na karibu sana kwenye Club ya watu wazima....

Umejiandaaje lakini??

Usijekuwa kama jamaa aliyeulizwa kama yuko tayari kuoa kimaandalizi, naye akajibu,..."niko tayari kabisa kwani nimeshanunua socks za kuvaa siku ya harusi yangu"....lol!!


Babu DC!!
 
Hongera mkuu,Wengine ngoja tuzeeke zeeke kwanza !!Pia tunakukaribisha siku yakikushinda usikose kuja kuyamwaga humu MMU

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama ulifuata maandiko matakatifu ya kutofanya zinaa kabla ya ndoa hongera sana.Jiandae kumpa mwenzi wako orgasm ya uhakika.Cha kufanya tafuta vitabu vya ndoa ili ujifunze zaidi aina zote za orgasm, pia unaweza ukapata uzoefu zaidi kwa ku google kwenye internet.Pamoja na mambo mengine lakini tendo la ndoa ndio chanzo cha watu kuoana.Mungu alisema zaeni mkaongezeke pia ni jambo la kuzingatia.Nawatakia mafanikio mema ila hakikisheni Mungu anakuwa pamoja nanyi hata kabla ya kufanya tendo la ndoa tafadhali Muombe Mungu kwanza.
 
MUYOOL...:nod::nod::nod: Tuombe, "Baba katika....... tunakushuru kwa muda na wakti kama huu uliotukutanisha tena hapa ku-do ze nidful. Tusaidie tuweze kufika kunako mlima sayuni pamoja. Baba ututangulie. Tunakualika uwe pamoja nasi...:disapointed::disapointed::disapointed:"

Na kwa sisi single BUT not lonely: Tunakutakia kila la heri na KWAHERI. On behalf of: Rural Swagga, mwekundu, mzabzab et al..
 
Last edited by a moderator:
Hongera mkuu,Wengine ngoja tuzeeke zeeke kwanza !!Pia tunakukaribisha siku yakikushinda usikose kuja kuyamwaga humu MMU

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums


Kwani nini unamwangia mtoto watu?

Kwa nini unategemea kuwa yatamshinda??

Mbona wengine tumezeeka hadi kustaafu na hatujashindwa?

Babu DC!!
 
Hongera sana GAZETI na kila la heri katika maisha mapya.
 
Last edited by a moderator:
MUYOOL...:nod::nod::nod: Tuombe, "Baba katika....... tunakushuru kwa muda na wakti kama huu uliotukutanisha tena hapa ku-do ze nidful. Tusaidie tuweze kufika kunako mlima sayuni pamoja. Baba ututangulie. Tunakualika uwe pamoja nasi...:disapointed::disapointed::disapointed:"

Na kwa sisi single BUT not lonely: Tunakutakia kila la heri na KWAHERI. On behalf of: Rural Swagga, mwekundu, mzabzab et al..
Singles wasio wabishi wanazidi kujitoa, sisi bado tupo tu.
 
Last edited by a moderator:
Mungu awabariki na kuwalinda
Mungu awainulie uso wake na kuwafadhili
na Mungu awabariki kila muingiapo na mtokapo.
 
Kila la kheri ktk ndoa yako hiyo siku ya jumanne trh 15 oct. ukumbuke kupost japo picha moja ya ndoa.
Ahsante mkuu nimechelewa kukujibu kutokana na uslow wa mtandao.
 
Mkuu hongera sana!
Mungu akujaalie ndoa bora!
...
Kwa msaada tu Zama ktk thread alizoanzisha Himidini, takriban zote lakini hasa hasa ktk thread yake 1 (jina nimeisahau) ameelezea vizuri sana kuhusu siku za mwanzo ambazo wanandoa hufurahia penzi zito ambalo haliwezi kuendelea kutokana na mfumo wa maisha.
Akaendelea kuelezea ni vipi munatakiwa kukabiliana na hiko kipindi cha pili kinachotazama maisha zaidi kuliko mapenzi!!!
...
Nakutakia ndoa njema!

Karibu mkuu na Mungu akutangulie
Ahsante sana
 
Back
Top Bottom