It is hard to be a man/ Sio jambo rahisi kuwa mwanaume kamili

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,972
3,511
Maisha yanabadilika kwa kasi ya ajabu sana, vijana wa kiume wa miaka ya sasa hawako tayari kufa kwa kipigania kutimiza ndoto zao, mwanaume yuko tayari kulelewa na Jimama au ajuza kusudi tu apate urahisi wa maisha na kutelekeza mke wake pamoja na watoto hii ni aibu sana hasa kwa vijana waliozaliwa miaka ya 1986 kuendelea mpaka 2000s.

Mwanaume kuchelewa kuoa kisa unaogopa maisha tayari unakosa sifa ya kua mwanaume, haiwezekani mwanaume unashindwa kuvumilia njaa kwa usiku mmoja huo ni utoto.

Mwanaume unatakiwa kupambana usiku na mchana kufikia ndoto zako ata kama itatokea ukatengwa na Ndugu, marafiki, wazazi au hata kupoteza uhai huo ndio uanaume.

Nawasikitikia wanawake sana kwani wengi wao wanaolewa na mwanaume wenye sifa na tabia zisizo za kiume, mwanaume yuko tayari kutelekeza familia bila taarifa yeyote na kutokomea kusikojulikana.

Kuwa mwanaume sio kua na uume tu pia maamuzi ya kiume ya kuweza kukomboa familia, jamiii na taifa lako huo ndio uanaume.

Mwanaume wa kileo kazi kujichubua, kuchonga nyusi na kupaka rangi kucha aseee aibu kweli, mwanaume anajipodoa kuliko mwanamkee Hatari tupu.......wakina Dada please jitahidini kuchagua mwanaume sio kukubali mtu tu kwa muonekano sijui urefu wake ama rangi utakuja kujutia pindi mambo yanakuwa magumu na unahitaji faraja na msaada wa mwanaume kumbe ulienae ana uume tu sio mwanaume.......

Nawaza kama wakoloni wangelikuako bado mpaka Leo hii watanzania waleo walivyowaoga tusingelipata Uhuru kamwe.

Leo hii unakuta mwanaume anaogopa kwenda JKT huu si upumbavu kabisa na wazazi wake wanamuunga mkono......

Wimbo wa Diamond platnumz wa Nitarejea una maneno yenye kuhamasisha uanaume kuna haja ya serikali kubadili mitaala ya elimu kusudi tupate wakina Patrice Lumumba, Thomas Sankara, Paul kagame, Museven, Vladimir putin na wakina Che uvara wengine wengi katika jamii yetu ya Leo.

Mwanaume wa Leo anakwama kodi anaandika Uzi jf, anakwama msosi kwa siku anakimbilia kuanzisha Uzi, mtu unakwama kumlipia mtoto ada ya 2m wa darasa la pili unalia kwanini usimpeleke shule za serikali?? Itafika kipindi mwanaume wataanza kuomba michango kusudi wakalipe mahari ukweni ..........huuu ni upuuzi sana........

Mwanaume hataki kazi za suluba kuamka SA 11 asubuhi anaona kero kwa halii hii kweli tutafika tunakotaka, madhara yake ndio mwanaume kutaka kuwa wanwake hatari tupu.......

Yajayo yanasikitisha sana. ITS HARD TO BE A MAN.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni ukweli mchungu
Ila hapa nahisi unatuzungumzia zaidi wanaume wa dar.
Barikiwa sana kiongozi.

Maendeleo hayana chama
 
Sasa hizi formula unazoleta zilipitishwa bunge lipi? Kwangu mimi mwanaume ni uweze kutunza tu familia yako kwa kadri ya uwezavyo, kama anatoga masikio na kutinda nyusi kisha anaenda kukata mauno stejini kama huyo Diamond utasema sio mwanaume ilihali anapigania ugali wa wanawe?
 
...

Mwanaume hataki kazi za suluba kuamka SA 11 asubuhi anaona kero kwa halii hii kweli tutafika tunakotaka, madhara yake ndio mwanaume kutaka kuwa wanwake hatari tupu.......
Uwa najiuliza hivi na wenzetu uwa wanawaza kama sisi kuwa ili uwe mwanaume lazima utumie nguvu kuliko akili? Ila itakuwa hapana kama wangekuwa wanawaza hivi wasingeendelea kwa kuinvent vitu vya kurahisisha kazi.
Yani mambo yanabadirika hatuwezi kuendelea kuishi kama zama za mawe siku hizi hata chakula una order kwenye simu as long as unajua jinsi ya kutengeneza pesa.
Tumia akili kuliko nguvu tengeneza pesa hata ukiamka saa 5 hakuna tatizo.
yaliyobaki naunga mkono hoja
 
Wanaume wa sikuhizi tunaogopa kuowa mke asie na kazi (golikipa)
............Unasema hivi kesho unakuja hapa kuomba ushauri wa app ya kusoma msg kwenye simu ya mtu kumbe umemkusudia mkeo nyumbani umemuhisi ana uhusiano na staff mwenzake!

Hata hamjui mnachokitaka,Mungu alikupa wewe uwezo na maarifa ya kutafuta chakula cha familia hayo mawazo ya kwamba uowe halafu mkeo aje akusaidie maisha na kukulisha unayatoa wapi?Yaani wewe ndo umedhihirisha content ya huu uzi,mwanamke kazi yake ni kuzaa watoto na kuwalea akiwasimamia kwa karibu wawe na maadili mema hujaambiwa ukaowe mwanamke akulishe.

Usiseme tena hivi mbele ya watu utachekwa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKWELI NI KWEMA HAYO YALIYOSEMWA NI UKWELI..WANAUME WA SIKUHIZI NI SOFT SANA...NGUVU HAMNA HATA MTU AKIKWAMA NA MKOKOTENI/GARI BARABARNI HASASUKUMI,KAZI KUCHATI, KAZI NI KUBET TUU, WAKIKUTA MTU ANAONEWA HAWEZ KUONGEA YAANI SHIDA TUPU,MIM NIMESHUHUDIA MTU ANAIBIWA NA TAPELI KWENYE GARI NA KUNA WANAUME WALIKUWA WANAANGALIA TU,IKABIDI NIANZE KUTEMBEZA KIBAO KWA TAPELI NAYEJIFANYA KILEMA .....SOFT ANS STUPID GENERATION.
 
Uwa najiuliza hivi na wenzetu uwa wanawaza kama sisi kuwa ili uwe mwanaume lazima utumie nguvu kuliko akili? Ila itakuwa hapana kama wangekuwa wanawaza hivi wasingeendelea kwa kuinvent vitu vya kurahisisha kazi.
Yani mambo yanabadirika hatuwezi kuendelea kuishi kama zama za mawe siku hizi hata chakula una order kwenye simu as long as unajua jinsi ya kutengeneza pesa.
Tumia akili kuliko nguvu tengeneza pesa hata ukiamka saa 5 hakuna tatizo.
yaliyobaki naunga mkono hoja
Mtoa maada hajasema ni lazima ufanye kazi za suluba halafu utagunduaje teknolojia ya kurahisisha kazi bila kuifanya kwanza kwanza kazi husika? Hata uspoifanya wewe nazan lazma uone watu wakiifanya hyo kaz ndpo upatiepo wazo la kutengeneza mashine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo mengine bwana ... kwahiyo kina nicola tesla and Co. Ambao hawakuwahi kuwa na familiar walikuwa ni wanawake ....

Tatizo letu wabongo Tunawaza sana Ngono na kuipa kipaumbele sometimes kuliko hata kula

Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu za tesla kutokuoa huwez kuzilinganisha na alizotoa mleta maada. Jamaa kasema baadh ya wanaume wanaogopa kuoa kisa maisha magumu. Sasa tesla alikua na ugumu wa maisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UKWELI NI KWEMA HAYO YALIYOSEMWA NI UKWELI..WANAUME WA SIKUHIZI NI SOFT SANA...NGUVU HAMNA HATA MTU AKIKWAMA NA MKOKOTENI/GARI BARABARNI HASASUKUMI,KAZI KUCHATI, KAZI NI KUBET TUU, WAKIKUTA MTU ANAONEWA HAWEZ KUONGEA YAANI SHIDA TUPU,MIM NIMESHUHUDIA MTU ANAIBIWA NA TAPELI KWENYE GARI NA KUNA WANAUME WALIKUWA WANAANGALIA TU,IKABIDI NIANZE KUTEMBEZA KIBAO KWA TAPELI NAYEJIFANYA KILEMA .....SOFT ANS STUPID GENERATION.
Hahahahahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom