IST inakula sana mafuta, sijui tatizo

IST inakula sana mafuta, sijui tatizo

uza ununue ingine
Wana JF, Nina IST CC 1490, Mileage 89000km, Nilisafiri toka Mwanza to Dar ikaanza tatizo la kutumia mafuta zaidi ya kawaida yake, ilikua inatumia 16km/litre lakini sasa hivi inaenda hadi 8km/litre. Nimefanya yafuatayo lakini bado tatizo; nimebadili engine oil na gearbox oil, nimetoa plugs nikaweka mpya, nimesafisha nozels, air filter na oil filter.

Nisaidieni jamani nifanye nini zaidi ili irudi kama zamani? Nafilisika mie.
 
Chacha tusaidie IST inaweza kuwa na 4WD?

Ndio, hata corolla pia,
NCP60,ni 2NZ engine, 1290CC(2WD),
NCP61, NCP65 ni 1NZ engine, 1490Cc(4WD)


http://www.beforward.jp/toyota/ist/bf133660/id/128265/


Mleta mada kuna fundi kajitolea kukufanyia hiyo kitu bure, chukua contact zake ufaidike na offer ya JF
 
Mkuu Ushirombo, kashughulikie yafuatayo:-

1. Angalia tenki la mafuta kama lina unyevunyevu. Kama linao basi linavujisha mafuta.

2. Angalia mfuniko wa tenki? Unafunga vizuri? Ni vizuri ubadilishe au badilisha seal zake

3. Kagulia pipes za mafuta kutoka kwenye tenki na kurudi kwenye tenki pamoja na fuel rail. Hakikisha hazina unyevunyevu wa kuvujisha mafuta

4. Angalia 'Charcoal Canister' kama inafanya vizuri

5. Cheki pipe ya kutoka kwenye 'Charcoal Canister' to intake manifold kama imechomekwa vizuri

6. Nozzles kama zina muda mrefu zibadilishe. Kusafisha haisaidii na zenyewe huwa zinachoka

7. Hakikisha spark plugs zako zote zinachoma

8. Badilisha Oxygen sensors

9. Safisha throttle body yote kwa sababu carbon deposits huwa inajaa ndani yake hivyo kuziba hewa kuingia kwenye combustion chambers

10. Hakikisha Overdrive button ipo 'ON'

11. Hakikisha Crankase ventilation System inafanya kazi vizuri (PCV pipes na PCV valve hazijaziba)

Ukishayafanya hayo rudi utupe maendeleo Mkuu.

Mkuuu hapo kwenye namba 10 paliwahi nisumbua miaka 10 iliyopita, nilipopata ushauri mpaka sasa gari zangu zinanusa fuel tu.
Vile vile kwa kuwa alikuwa highway bila shaka alizidi mwendo kasi zaidi ya 100km/h na inafahamika ulaji wa mafuta unakuaje chini na juu ya 100km/hr
 
Last edited by a moderator:
aji

Kadanga-13:23 Today-

Ninauza mashine yenye uwezo wakusaga tani mbili za chupa na tani tano za plastic ngumu mfano ndoo, madumu nk . bei sh.6,000,000 si hitaji dalali. Contact:0715185333

Reply
 
aji

Kadanga-13:23 Today-

Ninauza mashine yenye uwezo wakusaga tani mbili za chupa na tani tano za plastic ngumu mfano ndoo, madumu nk . bei sh.6,000,000 si hitaji dalali. Contact:0715185333

Reply

Umepotea njia.
 
Umewahi kuendesha gari?!

hilo siyo jibu. matumizi ya mafuta katika gari yanategemea mambo mengi

1. tairi
2. upepo
3. mwendo
4. mzigo
5. barabara
6. service
7. ukubwa wa ingine
8. upangiliaji wa gia


watanzania wengi hawajui matumizi,faida na hasara ya nilivyovitaja hapo juu.
 
Mkuu si umjibu tuu kama unajua? Kumbuka utawasaidia na wengine wasiojua na hawajapata nafasi ya kuuliza



achana naye huyo hajui sasa hapo anajaribu kuondoa ujinga wake kwa njia ya kuhoji.
 
Mkuuu hapo kwenye namba 10 paliwahi nisumbua miaka 10 iliyopita, nilipopata ushauri mpaka sasa gari zangu zinanusa fuel tu.
Vile vile kwa kuwa alikuwa highway bila shaka alizidi mwendo kasi zaidi ya 100km/h na inafahamika ulaji wa mafuta unakuaje chini na juu ya 100km/hr



kuhusu kuzidi au kupungua kwa ulaji wa mafuta unaotokana na mwendo hiyo hutegemeana na muundo wa engine. mfano land cruiser mkonge wa 2010 kadri unavyoongeza mwendo ndivyo inavyokunywa lakini Subaru kadri unavyoongeza mwendo ndivyo ulaji wa mafuta unavyopungua
 
Sie wengine tumeshazoea 6km/litre so kwa mwezi full tank mara tatu. Aisee kumbe ist 16km/litre hapo mkuu lazima ulalamike
 
kibongo bongo ! ukiagiza ni shi ngapi na huchukua mda gani. kuchukulia bongo au kuagiza kipi bora

Mpya = 0Km kwa sisi wengine,
Kibongo bongo = kuagiza iliyotumika Japan ama kwingineko
Kuu kuu = iliyotumika tayari hapa bongo

So nlijibu kwa maana ya ukiagiza mpya(kwako),

Ukiagiza huchukua maximun 2month,ukinunulia hapa pia ni sawa, u see the unit, u test n so so(ila mara nyingi wana temper nazo, ie KM)
 
Back
Top Bottom