Kwa kifupi gia za gari zimegawanyika mara tatu. Kuna Underdrive Gears, Direct Drive Gears na Overdrive Gear(s). Underdrive Gears ni gia ambazo zinafanya input shaft ya kwenda kwenye Gearbox (ambayo ni Output shaft ya Engine) inapozunguka mzunguko mmoja inapelekea output shaft (Propeller shaft / Drive shaft) izunguke for less than one turn. Mara nyingi kwa Gari ambazo zina Gear nne, Gia namba moja, mbili na Gia ya Reverse ni Underdrive Gears.
Direct Drive Gears ni gia ambazo zinafanya Input shaft ya kwenda kwenye Gearbox inapozunguka mzunguko mmoja inapelekea output shaft na yenyewe kuzunguka mara moja. Kwa gari zenye Gia nne, Gia namba tatu ni Direct Drive Gear.
Sasa, Overdrive Gear ni gia ambazo zinafanya Input shaft ya kwenda kwenye Gearbox inapozunguka mzunguko mmoja inapelekea output shaft (Propeller / Drive Shaft) izunguke zaidi ya mzunguko mmoja. Kwa gazi zenye Gia nne, Gia namba nne ni Overdrive Gear.
Relationship ya mizunguko kati ya Input shaft na Output shaft ndiyo kwa kitaalamu inaitwa 'Gear ratio'. So, Underdrive Gear ratio inakuwa higher than 1 (Mfano 1:0.5), Direct Drive Gear ratio always inakuwa ni 1 (i.e. 1:1) na Overdrive Gear ratio inakuwa less than 1 (Mfano 1:1.06).
Aidha, Kwa gari zenye Gia tano, sita, nane na kuendelea inategemea na jinsi manufacturer ame-design gear ipi iwe Underdrive, Direct Drive na Overdrive Gear. So unaweza kukuta gia zaidi ya moja mfano gia namba tano na sita ndiyo Overdrive Gears kwenye Gearbox yenye gia sita, nk. It depends on the design.
Sifa ya Underdrive Gears ni gia zenye nguvu lakini hazina speed. Sifa za Overdrive Gears ni gia ambazo hazina nguvu lakini zinazalisha speed kubwa. Sifa ya Direct Drive Gear ina sifa ambazo zina range between the two above. Yaani zina nguvu ingawa si kama Underdrive Gears lakini ni zaidi ya Overdrive Gear na zina Speed ingawa si kama Overdrive Gears lakini ni zaidi ya Underdrive Gear
Matumizi ya Overdrive Button
Unapowasha Overdrive button "ON" maana yake umeiruhusu gearbox ku-engage hadi kwenye Overdrive Gear gari iki-meet certain conditions (Mfano spidi ikifikia level flani). Uzuri wa Overdrive Gear ni kwamba ina-save mafuta kwa sababu input shaft (Output shaft ya Engine) itakapozunguka mzunguko mmoja itapelekea matairi ya gari(through Propeller / Drive shaft) kuzunguka zaidi ya mzunguko mmoja (Assuming Axle Ratio ni 1:1) na hivyo kukufikisha unapokwenda kwa kutumia mafuta machache yatakayotumika kuzungusha engine mara mmoja tu tofauti na Underdrive Gears ambazo ili matairi yazunguke mzunguko mmoja ni lazima engine izunguke zaidi ya mzunguko mmoja (na hivyo mafuta kuchomwa mengi).
So Overdrive inapoiweka 'OFF' maana yake unaizuia gearbox ku-engage into higher gears ambazo kimsingi zina-save mafuta. Aidha, inapoiweka 'OFF' huku gari unaikimbiza kwa kunyaga sana accelerator pedal unachosha Engine.
Unaruhusiwa kuweka 'OVERDRIVE OFF' katika mazingira ambayo unapanda mlima wenye kilomita nyingi. Mfano unapopanda Mlima Kitonga ni muhimu kuweka 'OVERDRIVE OFF' lakini usikanyage accelerator pedal saana hadi mwisho (doing so unaweza pasua head gasket). Kwa kufanya hivyo utakuwa imeiambia Gearbox kwa mazingira uliyomo Overdrive Gears are irrelevant so just engage on Underdrive Gears only. Ushuhuda wa hili upo hata kwenye Gari za Manual. Hata ukianzia na gia yako namba nne kutoka chini ya Kitingo ukapanda nayo kwa speed mwisho wa siku ukifika katikati itakubidi tu urudi kwenye gear namba mbili au mmoja ambazo ndizo gia nzuri za kupandia Milima. Kwa sababu underdrive gears na zina nguvu tofauti ya kupandisha gari Mlima kuliko na Overdrive Gears.
CC:
CYBERTEQ,
Ushirombo,
charger TCleverly,
mandingo6262, etc