IST inakula sana mafuta, sijui tatizo

IST inakula sana mafuta, sijui tatizo

Mkuu Ushirombo, kashughulikie yafuatayo:-

1. Angalia tenki la mafuta kama lina unyevunyevu. Kama linao basi linavujisha mafuta.

2. Angalia mfuniko wa tenki? Unafunga vizuri? Ni vizuri ubadilishe au badilisha seal zake

3. Kagulia pipes za mafuta kutoka kwenye tenki na kurudi kwenye tenki pamoja na fuel rail. Hakikisha hazina unyevunyevu wa kuvujisha mafuta

4. Angalia 'Charcoal Canister' kama inafanya vizuri

5. Cheki pipe ya kutoka kwenye 'Charcoal Canister' to intake manifold kama imechomekwa vizuri

6. Nozzles kama zina muda mrefu zibadilishe. Kusafisha haisaidii na zenyewe huwa zinachoka

7. Hakikisha spark plugs zako zote zinachoma

8. Badilisha Oxygen sensors

9. Safisha throttle body yote kwa sababu carbon deposits huwa inajaa ndani yake hivyo kuziba hewa kuingia kwenye combustion chambers

10. Hakikisha Overdrive button ipo 'ON'

11. Hakikisha Crankase ventilation System inafanya kazi vizuri (PCV pipes na PCV valve hazijaziba)

Ukishayafanya hayo rudi utupe maendeleo Mkuu.

haswaa umempa jibu muafaka! akicheki hivi Lazma atagundua tatizo lilipo! tatizo ni fundi gan muelewa atakayempata? maana mafundi wengi huwa wanafanya trial and error tu!
 
Last edited by a moderator:
haswaa umempa jibu muafaka! akicheki hivi Lazma atagundua tatizo lilipo! tatizo ni fundi gan muelewa atakayempata? maana mafundi wengi huwa wanafanya trial and error tu!

Ni kweli mkuu. Labda tungepata mwelekezo wa Fundi mkali
 
Mkuu unge edit bs yani umegoogle ukayamwaga jinsi yalvyo

haina shida mkuu edit wewe au ulitaka ionekane kama nimetowa kichwani mwangu??

haina shida hapa tunatafuta dawa so hata kama utaitoa kijijini au kwa google ilimladi tu mgonjwa apone
 
Mkuu Ushirombo, kashughulikie yafuatayo:-

1. Angalia tenki la mafuta kama lina unyevunyevu. Kama linao basi linavujisha mafuta.

2. Angalia mfuniko wa tenki? Unafunga vizuri? Ni vizuri ubadilishe au badilisha seal zake

3. Kagulia pipes za mafuta kutoka kwenye tenki na kurudi kwenye tenki pamoja na fuel rail. Hakikisha hazina unyevunyevu wa kuvujisha mafuta

4. Angalia 'Charcoal Canister' kama inafanya vizuri

5. Cheki pipe ya kutoka kwenye 'Charcoal Canister' to intake manifold kama imechomekwa vizuri

6. Nozzles kama zina muda mrefu zibadilishe. Kusafisha haisaidii na zenyewe huwa zinachoka

7. Hakikisha spark plugs zako zote zinachoma

8. Badilisha Oxygen sensors

9. Safisha throttle body yote kwa sababu carbon deposits huwa inajaa ndani yake hivyo kuziba hewa kuingia kwenye combustion chambers

10. Hakikisha Overdrive button ipo 'ON'

11. Hakikisha Crankase ventilation System inafanya kazi vizuri (PCV pipes na PCV valve hazijaziba)

Ukishayafanya hayo rudi utupe maendeleo Mkuu.

Wewe ni fundi aisee!!! elekeza please tulete magari yetu
 
Last edited by a moderator:
Nimeelimika sana kuhusu mfumo na matumizi ya gears za gari kupitia hii thread. Mana kuna vitu nilikuwa cjui vizuri hasa matumizi ya OD ingawa ni mtumiaji mkuu wa gari.
Much respect kwa muanzisha mada,Ushirombo na wachangaji walio-comment +ve things. Kidole 007,chacha kisri,eliza wa tegeta,lege na pdidy.
Mungu awabaliki sana jamani..
 
Kwa kifupi gia za magari zimegawanyika mara tatu. Kuna Underdrive Gears, Direct Drive Gears na Overdrive Gear(s). Underdrive Gears ni gia ambazo zinafanya input shaft ya kwenda kwenye Gearbox (ambayo ni Output shaft ya Engine) inapozunguka mzunguko mmoja inapelekea output shaft (Propeller shaft / Drive shaft) izunguke for less than one turn. Mara nyingi kwa Gari ambazo zina Gear nne, Gia namba moja, mbili na Gia ya Reverse ni Underdrive Gears.

Direct Drive Gears ni gia ambazo zinafanya Input shaft ya kwenda kwenye Gearbox inapozunguka mzunguko mmoja inapelekea output shaft na yenyewe kuzunguka mara moja. Kwa gari zenye Gia nne, Gia namba tatu ni Direct Drive Gear.

Sasa, Overdrive Gears ni gia ambazo zinafanya Input shaft ya kwenda kwenye Gearbox inapozunguka mzunguko mmoja inapelekea output shaft (Propeller / Drive Shaft) izunguke zaidi ya mzunguko mmoja. Kwa gari zenye Gia nne, Gia namba nne ni Overdrive Gear.

Relationship ya mizunguko kati ya Input shaft na Output shaft ndiyo kwa kitaalamu inaitwa 'Gear ratio'. So, Underdrive Gear ratio inakuwa higher than 1 (Mfano 1:0.5), Direct Drive Gear ratio always inakuwa ni 1 (i.e. 1:1) na Overdrive Gear ratio inakuwa less than 1 (Mfano 1:1.6).

Aidha, Kwa gari zenye Gia tano, sita, nane na kuendelea inategemea na jinsi manufacturer ame-design gear ipi iwe Underdrive, Direct Drive na Overdrive Gear. So unaweza kukuta gia zaidi ya moja mfano gia namba tano na sita ndiyo Overdrive Gears kwenye Gearbox yenye gia sita, nk. It depends on the design.

Sifa ya Underdrive Gears ni gia zenye nguvu lakini hazina speed. Sifa za Overdrive Gears ni gia ambazo hazina nguvu lakini zinazalisha speed kubwa. Sifa ya Direct Drive Gear ina sifa ambazo zina range between the two above. Yaani zina nguvu ingawa si kama Underdrive Gears lakini ni zaidi ya Overdrive Gear na zina Speed ingawa si kama Overdrive Gears lakini ni zaidi ya Underdrive Gear

Matumizi ya Overdrive Button
Unapowasha Overdrive button "ON" maana yake umeiruhusu gearbox ku-engage hadi kwenye Overdrive Gear gari iki-meet certain conditions (Mfano spidi ikifikia level flani). Uzuri wa Overdrive Gear ni kwamba ina-save mafuta kwa sababu input shaft (Output shaft ya Engine) itakapozunguka mzunguko mmoja itapelekea matairi ya gari(through Propeller / Drive shaft) kuzunguka zaidi ya mzunguko mmoja (Assuming Axle Ratio ni 1:1) na hivyo kukufikisha unapokwenda kwa kutumia mafuta machache yatakayotumika kuzungusha engine mara mmoja tu tofauti na Underdrive Gears ambazo ili matairi yazunguke mzunguko mmoja ni lazima engine izunguke zaidi ya mzunguko mmoja (na hivyo mafuta kuchomwa mengi).

So Overdrive inapoiweka 'OFF' maana yake unaizuia gearbox ku-engage into higher gears ambazo kimsingi zina-save mafuta. Aidha, inapoiweka 'OFF' huku gari unaikimbiza kwa kunyaga sana accelerator pedal unachosha Engine.

Unaruhusiwa kuweka 'OVERDRIVE OFF' katika mazingira ambayo unapanda mlima wenye kilomita nyingi. Mfano unapopanda Mlima Kitonga ni muhimu kuweka 'OVERDRIVE OFF' lakini usikanyage accelerator pedal saana hadi mwisho (doing so unaweza pasua head gasket). Kwa kufanya hivyo utakuwa imeiambia Gearbox kwa mazingira uliyomo Overdrive Gears are irrelevant so just engage on Underdrive Gears only. Ushuhuda wa hili upo hata kwenye Gari za Manual. Hata ukianzia na gia yako namba nne kutoka chini ya Kitongo ukapanda nayo kwa speed mwisho wa siku ukifika katikati itakubidi tu urudi kwenye gear namba mbili au moja ambazo ndizo gia nzuri za kupandia Milima. Kwa sababu underdrive gears zina nguvu ya kupandisha gari Mlima kuliko na Overdrive Gears.

CC: CYBERTEQ, Ushirombo, charger TCleverly, mandingo6262, etc

Jamani katika watu wa kupongezwa ni pamoja na huyu mheshimiwa, napendekeza apewe forum yake ya utaalamu wa magari, ukweli siku hizi magari yamekuwa kama simu ukishajua kuandika sms twende kazi kumbe kuna mambo mengi unapaswa kuyajua ili umaximize matumizi ya gari lako.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ushirombo, kashughulikie yafuatayo:-

1. Angalia tenki la mafuta kama lina unyevunyevu. Kama linao basi linavujisha mafuta.

2. Angalia mfuniko wa tenki? Unafunga vizuri? Ni vizuri ubadilishe au badilisha seal zake

3. Kagulia pipes za mafuta kutoka kwenye tenki na kurudi kwenye tenki pamoja na fuel rail. Hakikisha hazina unyevunyevu wa kuvujisha mafuta

4. Angalia 'Charcoal Canister' kama inafanya vizuri

5. Cheki pipe ya kutoka kwenye 'Charcoal Canister' to intake manifold kama imechomekwa vizuri

6. Nozzles kama zina muda mrefu zibadilishe. Kusafisha haisaidii na zenyewe huwa zinachoka

7. Hakikisha spark plugs zako zote zinachoma

8. Badilisha Oxygen sensors

9. Safisha throttle body yote kwa sababu carbon deposits huwa inajaa ndani yake hivyo kuziba hewa kuingia kwenye combustion chambers

10. Hakikisha Overdrive button ipo 'ON'

11. Hakikisha Crankase ventilation System inafanya kazi vizuri (PCV pipes na PCV valve hazijaziba)

Ukishayafanya hayo rudi utupe maendeleo Mkuu.

Mkuu tupatie private contact zako tuweze kupata ushauri zaidi, manake gari za siku hizi unampelekea fundi anakuuliza mbona haoni kaburata.
 
Last edited by a moderator:
Mi nimetoa ushauri kwa Ushirombo naambiwa namlisha tango, so its better ndugu yetu charger aliyesema namlisha tango basi yeye akatoa elemu maana yeye ndiyo anafahamu vizuri. Mtu hana imani na Mimi kwa nini niendelee kuwalisha matango??

Mkuu tupatie contact tukualike Mwanza utoe semina ya utunzaji na uendeshaji wa hivi vi baby walker, manake vingine tunavinunua vilishachoka tayari nakuta passo ina km 167,000. lazima magonjwa kama hayo unayoyaeleza hayakosi.
 
Last edited by a moderator:
eddy nakupongeza sana,watu wengi wanashindwa kuelimisha watu kupitia jf,lkn ww umeilindendea haki jukwaa hili.
 
Pole sana Mkuu. Hiyo gari nina wasiwasi MKubwa ulinunua ikiwa tayari mbovu na ilipigwa service tu. Wabongo wengi wanaangalia klm ilizotembea badala la engine. Ni ngumu saana kuwa na gari uliyotembea klm hizo na kuwa na matumizi ya mafuta kiasi hcho. Mi nilinunua IST cc 1500, ikiwa na klm 174,000 from japan, nimesafiri nayo Dar_Mbeya, Dar-Arusha, Dar-.kahama. Achana na route za kawaida na fuel consuption ni 16.4km/ltr. Hiyo tafuta mteja uza ishakuwa kimeo.

Sasa nani ataenunua kimeo:what:
 
Wana JF, Nina IST CC 1490, Mileage 89000km, Nilisafiri toka Mwanza to Dar ikaanza tatizo la kutumia mafuta zaidi ya kawaida yake, ilikua inatumia 16km/litre lakini sasa hivi inaenda hadi 8km/litre. Nimefanya yafuatayo lakini bado tatizo; nimebadili engine oil na gearbox oil, nimetoa plugs nikaweka mpya, nimesafisha nozels, air filter na oil filter.

Nisaidieni jamani nifanye nini zaidi ili irudi kama zamani? Nafilisika mie.

Kuna mdau kachangia very deep, mtu wa wakawaida akijarib vyote hivyo ni kumwongezea frastrutions tu incase kila akimaliza kimoja tatizo bado lipo, mleta mada gari yako ina engine ya 1NZ(one of the best engine, na kwenye hybrid ipo pia), gari lako ni 4WD,so my suspicions lies on 4WD botton, ama kwenye diff(rear), angalia hivi kwanza, then benda ukafanye diagnosis(ni kama 50, 000 hivi), utapata kujua nini hasa kina tatizo
 
Chacha tusaidie IST inaweza kuwa na 4WD?
 
Mkuuu mwambie aje kwangu nitamfanyia.diagnosis bure kabisa bila kumtoza hata sh.
Nitamfanyia ki jf zaidi.
My contact 0717228064.
mm nipo mwenge dar ila.kazi popote pale inafuatwa
 
Mkuu Ushirombo, kashughulikie yafuatayo:-

1. Angalia tenki la mafuta kama lina unyevunyevu. Kama linao basi linavujisha mafuta.

2. Angalia mfuniko wa tenki? Unafunga vizuri? Ni vizuri ubadilishe au badilisha seal zake

3. Kagulia pipes za mafuta kutoka kwenye tenki na kurudi kwenye tenki pamoja na fuel rail. Hakikisha hazina unyevunyevu wa kuvujisha mafuta

4. Angalia 'Charcoal Canister' kama inafanya vizuri

5. Cheki pipe ya kutoka kwenye 'Charcoal Canister' to intake manifold kama imechomekwa vizuri

6. Nozzles kama zina muda mrefu zibadilishe. Kusafisha haisaidii na zenyewe huwa zinachoka

7. Hakikisha spark plugs zako zote zinachoma

8. Badilisha Oxygen sensors

9. Safisha throttle body yote kwa sababu carbon deposits huwa inajaa ndani yake hivyo kuziba hewa kuingia kwenye combustion chambers

10. Hakikisha Overdrive button ipo 'ON'

11. Hakikisha Crankase ventilation System inafanya kazi vizuri (PCV pipes na PCV valve hazijaziba)

Ukishayafanya hayo rudi utupe maendeleo Mkuu.

Ushauri mzuri sana ila uko too technical, kwa mtumiaji wa kawaida hizo terminology ulizotumia ni ngumu kuelewa ,ni bora ungemshauri aje kwako kama wewe ni fundi, au apeleke gari kwenye diag computer
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom