Issue ya IPTL mchezo unachezwa hapa kuwakanganya watu:

Binafsi nimekuwa nikifuatilia issue ya IPTL ambapo nimekuwa nikijiuliza sana wanaosema PESA si za UMMA wanatumia kigezo gani na hivyo hivyo wanaosema pesa ni za UMMA wanatumia kigezo gani? Nimepitia vizuri baadhi ya documents na barua zinazotembea hapa jamvini yangu sakata hili lianze na kujiridhisha kuwa mchezo unachezwa au umeanzia kuchezwa hapa.

Wapigaji wa fedha hizi kwanza kabisa waliamua kubadilisha tafsiri ya malengo ya kufungua Escrow account: Tafsiri sahihi kwa uelewa wangu ni kwamba, Escrow account ilifunguliwa baada ya kutokea mgogoro kati ya Tanesco na IPTL. Hapa ieleweke vizuri ni kati ya Tanesco na IPTL na si kati ya wamiliki yaani shareholders wa IPTL.

Mgogoro ulikuwa ni kwamba, Tanesco waligundua ongezeko kwenye ukokotoaji wa capacity charge tofauti na gharama halisi kwenye mkataba hivyo kuamua kufungua Escrow account kwa madhumuni ya kuhifadhi hilo ongezeko TU wakati mgogoro dhidi ya ongeko hilo unashughulikiwa. Hapa pia ieleweke kwamba escrow account ilifunguliwa na Tanesco kwa kuweka fedha za ongezeko la capacity charge tu na si malipo halisi ya matumizi ya umeme wa IPTL

Kinachoonekana, baadaye wabia wa IPTL yaani Melchimal na VIP Engineering nao walikuja kutofautiana hasa kwenye kugawana Mapato (shares) kutokana na mauzo ya umeme Tanesco, hivyo basi kuamua fedha za mauzo ziende Escrow account mpaka watakaporidhiana. Hapa maana yake nini: Maana yake ikawa kwamba account hii ikawa na pesa za aina mbili Yaani ile pesa ya ongezeko inayolalamikiwa na Tanesco na pesa halisi ya mauzo ya umeme ambayo iliwekwa baada ya wabia kutofautiana.

Baada ya PAP kudai kununua hisa za wabia wote waliokuwa wanagombana yaani VIP Engineering (30%) and Melchimal (70%) na kupeleka shauri la kufuta kesi mahakamani hivyo kuwa na mamlaka ya kumiliki mali na madeni ya IPTL. Hapa ndipo wajanja hawa wakabadili tafsiri nzima ya kufungua account ya escrow kwa kutaka kuuonesha UMMA kuwa account hii ilifunguliwa kwa sababu ya ugomvi wa wabia wa IPTL yaani VIP na Melchimal hizo kwa kuwa hisa zote kwa sasa zipo chini ya PAP basi automatically fedha zote za Escrow pia ni za PAP

Kumbe uhalisia ni kwamba ndani ya fedha hizo kulikuwa na fedha nyingi sana za Tanesco ambayo ilikuwa inalalamika kuibiwa na IPTL baada ya kuona kuna ongezeko la kniyemela katika kukokotoa capacity charge. Uhalisia ni kwamba ilitakiwa fedha hizi zisitolewe ili kusubili uamuzi wa mahakama dhidi ya malalamiko ya Tanesco kuhusu ongezeko hilo ili kama Tanesco ikionekana ndio ilikuwa inapunjwa basi ichukue pesa zake. Hapa ieleweke kwamba uamuzi wa mahakama haimaanishi uamuzi wa mahakama kati ya wabia wa IPTL (Melchimal na VIP) bali ni uamuzi wa mahakama kati ya Tanesco na IPTL dhidi ya ongezeko linalolalamikiwa na Tanesco

Inasemekana uamuzi wa mahakama kati ya Tanesco na IPTL umekuja kutoka katika kipindi ambacho wajanja wameshavuta hela tayari na zaidi taarifa za mitandao zinasema madai ya Tanesco yalikuwa ni genuine hivyo ilitakiwa calculation ya capacity charge ifanyike upya na kulikuwa na uwezekano fedha karibu zote za kwenye account hiyo kama zingekuwa hazijachotwa zingetakiwa kukabidhiwa Tanesco achana na fedha zingine za kodi kutokana na mauzo ya HISA na uamisho wa mkataba kwenda kwa mbia mpya.

Kwa hiyo hata zile fedha za uzalishaji nazo zirudi Tanesco ? Ulisema VIP na Melchaar waligombana na fedha za malipo ya uzalishsji zikawekwa Escrow.
Sasa unasema fedha zote za Tanesco .hesabu zako haziko sawa umeme haukutolewa bure
 
Ndo maana katika ripoti ya CAG imeoneshwa overpayment to IPTL,mkuu umeweka vizuri sana
 
Kwa hiyo hata zile fedha za uzalishaji nazo zirudi Tanesco ? Ulisema VIP na Melchaar waligombana na fedha za malipo ya uzalishsji zikawekwa Escrow.
Sasa unasema fedha zote za Tanesco .hesabu zako haziko sawa umeme haukutolewa bure

Mkuu katika watu wote walio changia Mpaka sasa ni wewe tu ambaye unaona hesabu zake hazipo sawa! Nitakuwa sahihi nikisema kuwa wewe ndio haupo sawa na Si hesabu zake

Ishu ipo hivi VIP na huyo mshenzi mwenzie ambao ni wamiliki wa IPTL walikuwa na ugomvi kuhusu pato wanalopata kutoka TANESCO(hii Haina uhusiano na mgorogoro kati ya IPTL na TANESCO). Hivyo wabia Hawa wakaamua hela zao ziwekwe BOT mpaka mgorogoro wao uishe. Tatizo ni kwamba hela zilizo tokana na ugomvi wa wabia/wamiliki wa IPTL zilichanganywa na hela zilizotokana na mgogoro kati ya IPTL na TANESCO,na baadae ikaamuliwa hela zote wachukue IPTL wakati kulikuwemo na hela za TANESCO pia sababu zilichanganywa zote.

Umeelewa sasa?
 
Soma vizuri hiyo post yangu ielewe then ujitahidi angalau kidogo kuinua akili yako ndio utaipata picha bila hivyo huwezi kuelewa na utaendelea kuja na majibu au maswali kama haya
 
Swali:
Kama TANESCO inaidai au imedhulumiwa na IPTL ni kitu gani kinazuia kupata haki yake? Ikiwa

1. bado wanafanya biashara na IPTL
2. Mitambo iko tegega na unaweza kutaifishwa... Na kwa kuwa hilo liko why would ESCROW account be the only solution? As if the IPTL ni kampuni ya mfukoni?
 
Siamini kama wasomi wa Bot wanaweza kuchanganya hera toka sources mbili tajwa.....bas kutakuwa na tatizo kubwa sana huko.....
 
Asante kamanda...umetoa mwanga ila bado fedha ni za umma, TANESCO ambaye ndiye aliekuwa na kiasi kikubwa cha fedha ni shirika la Umma...hivyo kama maamuzi ya mahakama yameamua kua ukokotoaji wa capacity charge urudiwe na kuna dalili kua fedha zile zingelipwa kwa TANESCO basi Umma umeibiwa
 
Mchecheto wa nini? Report iko tayari na baadhi ya evidence ziko humu. It's just a matter of time 28.11.2014
 
Kuna msemo wa hekima unasema hivi 'KILA LILILO NA MWANZO HALIKOSI KUWA NA MWISHO'
 
Inasemekana uamuzi wa mahakama kati ya Tanesco na IPTL umekuja kutoka katika kipindi ambacho wajanja wameshavuta hela tayari na zaidi taarifa za mitandao zinasema madai ya Tanesco yalikuwa ni genuine hivyo ilitakiwa calculation ya capacity charge ifanyike upya na kulikuwa na uwezekano fedha karibu zote za kwenye account hiyo kama zingekuwa hazijachotwa zingetakiwa kukabidhiwa Tanesco achana na fedha zingine za kodi kutokana na mauzo ya HISA na uamisho wa mkataba kwenda kwa mbia mpya.[/QUOTE]

Mkuu sikuelewi unaposema INASEMEKANA.Labda tupe mwanga zaidi kuhusu hukumu ya mahakama.
 
Mkuu katika watu wote walio changia Mpaka sasa ni wewe tu ambaye unaona hesabu zake hazipo sawa! Nitakuwa sahihi nikisema kuwa wewe ndio haupo sawa na Si hesabu zake

Ishu ipo hivi VIP na huyo mshenzi mwenzie ambao ni wamiliki wa IPTL walikuwa na ugomvi kuhusu pato wanalopata kutoka TANESCO(hii Haina uhusiano na mgorogoro kati ya IPTL na TANESCO). Hivyo wabia Hawa wakaamua hela zao ziwekwe BOT mpaka mgorogoro wao uishe. Tatizo ni kwamba hela zilizo tokana na ugomvi wa wabia/wamiliki wa IPTL zilichanganywa na hela zilizotokana na mgogoro kati ya IPTL na TANESCO,na baadae ikaamuliwa hela zote wachukue IPTL wakati kulikuwemo na hela za TANESCO pia sababu zilichanganywa zote.

Umeelewa sasa?

Kuna wengine humu wanadai fedha yote ilikuwa ni 300b
Na hawo PAP/IPTL walichota 200b huoni kuwa wamechukua chao tu?
 
wachangiaji wenzangu, tunaposoma habari tusisahau kuunganishwa na kichwa chake. Mtoa uzi ameeleza mchezo ulivyochezwa ili kuwachanganya watu na wajanja kuiba kirahisi. Hili lilifanyika kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wakiwemo maboss wa BOT na wa sekta zingine nyeti za serikali.
 
Hata mimi nimeelewa Hivyo ila Ishu ni kwamba kwanini hela za mgogoro wa ndani ya Kampuni binafsi(IPTL) iwekwe BOT? Na kwanini hiyo hela ichanganywe na ile ya mgogoro wao na TANESCO?

Mgogoro wa IPTL na TANESCO ni tofauti na mgogoro wa ndani baina ya wabia hivyo Hizo hela hazi kupaswa kuwekwa kwenye account moja.

Hii Ishu ilipikwa kiufundi sana,hata Huo mgogoro wa wabia wa IPTL ni wa kutengeneza ili wazichanganye hela pamoja huko BOT baadae wazichote.

Kwa hela ambayo IPTL ilikuwa inaingiza isingewezekana iweze kufilisika na hiyo sababu iliyotolewa juu ya mgogoro baina ya shareholders haina mashiko. Iweje wabia mgombane kuhusu mgao wa fedha wakati documents za umiliki wa kampuni zinaonyesha wazi asilimia ya hisa zinazo milikiwa na kila mmoja(30% VIP na 70% Hao wapuuzi wengine). Mnaanzaje kugombana kuhusu mgao ilihali kila kitu kipo stated?

Huu ni mchongo ulipangwa ili watu wapige hela za uchaguzi 2015
mkuu BOT inatunza pesa za makampuni binafsi?, ninaloona hapa ni mpango wa wizi ulio sukwa, aliye uza hisa na aliye nunua ni mmoja! isipo kuwa anabadili majina kuonesha kuwa kuna mmiliki mpya. Pia kuna uwezekano mkubwa kuwa pesa yote kwny akaunti ilikuwa ya tanesco hao wengine ni geresha tu.
 
Kuna wengine humu wanadai fedha yote ilikuwa ni 300b
Na hawo PAP/IPTL walichota 200b huoni kuwa wamechukua chao tu?

Akili iliyotumika kupiga mshiko huo lengo lake ni kukufanya uwe na akili na fikra hizo. Inahitajika akili zaidi ili kuufahamu mchezo vizuri. Kuna documents nyingi sana hapa jamvini jitahidi kuzipitia uzisome utaelewa na hata hukumu ya jaji Utamwa ilikuwa ni kukamilisha mpango mzima. Pitia vizuri hukumu hiyo then soma vizuri documents na barua alizopost Manyerere then uzifanyie analysis kwa kutumia akili ya juu utapata picha, nasisitiza soma na analyse kwa akili ya juu.
 
mkuu BOT inatunza pesa za makampuni binafsi?, ninaloona hapa ni mpango wa wizi ulio sukwa, aliye uza hisa na aliye nunua ni mmoja! isipo kuwa anabadili majina kuonesha kuwa kuna mmiliki mpya. Pia kuna uwezekano mkubwa kuwa pesa yote kwny akaunti ilikuwa ya tanesco hao wengine ni geresha tu.

That's why pia kuna utata mkubwa wa jinsi shares za wabia zilivyouzwa na na values ya share hizo
 
Inasemekana uamuzi wa mahakama kati ya Tanesco na IPTL umekuja kutoka katika kipindi ambacho wajanja wameshavuta hela tayari na zaidi taarifa za mitandao zinasema madai ya Tanesco yalikuwa ni genuine hivyo ilitakiwa calculation ya capacity charge ifanyike upya na kulikuwa na uwezekano fedha karibu zote za kwenye account hiyo kama zingekuwa hazijachotwa zingetakiwa kukabidhiwa Tanesco achana na fedha zingine za kodi kutokana na mauzo ya HISA na uamisho wa mkataba kwenda kwa mbia mpya.

Mkuu sikuelewi unaposema INASEMEKANA.Labda tupe mwanga zaidi kuhusu hukumu ya mahakama.[/QUOTE]

Mkuu ndio hapo inabidi kama great thinker nawe uishughulishe akili yako kufikiri zaidi ili upate picha zaidi na kuwasaidia wengine kuelewa, huwezi kufafanuliwa kila kitu fanya analysis
 
Binafsi nimekuwa nikifuatilia issue ya IPTL ambapo nimekuwa nikijiuliza sana wanaosema PESA si za UMMA wanatumia kigezo gani na hivyo hivyo wanaosema pesa ni za UMMA wanatumia kigezo gani? Nimepitia vizuri baadhi ya documents na barua zinazotembea hapa jamvini yangu sakata hili lianze na kujiridhisha kuwa mchezo unachezwa au umeanzia kuchezwa hapa.

Wapigaji wa fedha hizi kwanza kabisa waliamua kubadilisha tafsiri ya malengo ya kufungua Escrow account: Tafsiri sahihi kwa uelewa wangu ni kwamba, Escrow account ilifunguliwa baada ya kutokea mgogoro kati ya Tanesco na IPTL. Hapa ieleweke vizuri ni kati ya Tanesco na IPTL na si kati ya wamiliki yaani shareholders wa IPTL.

Mgogoro ulikuwa ni kwamba, Tanesco waligundua ongezeko kwenye ukokotoaji wa capacity charge tofauti na gharama halisi kwenye mkataba hivyo kuamua kufungua Escrow account kwa madhumuni ya kuhifadhi hilo ongezeko TU wakati mgogoro dhidi ya ongeko hilo unashughulikiwa. Hapa pia ieleweke kwamba escrow account ilifunguliwa na Tanesco kwa kuweka fedha za ongezeko la capacity charge tu na si malipo halisi ya matumizi ya umeme wa IPTL

Kinachoonekana, baadaye wabia wa IPTL yaani Melchimal na VIP Engineering nao walikuja kutofautiana hasa kwenye kugawana Mapato (shares) kutokana na mauzo ya umeme Tanesco, hivyo basi kuamua fedha za mauzo ziende Escrow account mpaka watakaporidhiana. Hapa maana yake nini: Maana yake ikawa kwamba account hii ikawa na pesa za aina mbili Yaani ile pesa ya ongezeko inayolalamikiwa na Tanesco na pesa halisi ya mauzo ya umeme ambayo iliwekwa baada ya wabia kutofautiana.

Baada ya PAP kudai kununua hisa za wabia wote waliokuwa wanagombana yaani VIP Engineering (30%) and Melchimal (70%) na kupeleka shauri la kufuta kesi mahakamani hivyo kuwa na mamlaka ya kumiliki mali na madeni ya IPTL. Hapa ndipo wajanja hawa wakabadili tafsiri nzima ya kufungua account ya escrow kwa kutaka kuuonesha UMMA kuwa account hii ilifunguliwa kwa sababu ya ugomvi wa wabia wa IPTL yaani VIP na Melchimal hizo kwa kuwa hisa zote kwa sasa zipo chini ya PAP basi automatically fedha zote za Escrow pia ni za PAP

Kumbe uhalisia ni kwamba ndani ya fedha hizo kulikuwa na fedha nyingi sana za Tanesco ambayo ilikuwa inalalamika kuibiwa na IPTL baada ya kuona kuna ongezeko la kniyemela katika kukokotoa capacity charge. Uhalisia ni kwamba ilitakiwa fedha hizi zisitolewe ili kusubili uamuzi wa mahakama dhidi ya malalamiko ya Tanesco kuhusu ongezeko hilo ili kama Tanesco ikionekana ndio ilikuwa inapunjwa basi ichukue pesa zake. Hapa ieleweke kwamba uamuzi wa mahakama haimaanishi uamuzi wa mahakama kati ya wabia wa IPTL (Melchimal na VIP) bali ni uamuzi wa mahakama kati ya Tanesco na IPTL dhidi ya ongezeko linalolalamikiwa na Tanesco

Inasemekana uamuzi wa mahakama kati ya Tanesco na IPTL umekuja kutoka katika kipindi ambacho wajanja wameshavuta hela tayari na zaidi taarifa za mitandao zinasema madai ya Tanesco yalikuwa ni genuine hivyo ilitakiwa calculation ya capacity charge ifanyike upya na kulikuwa na uwezekano fedha karibu zote za kwenye account hiyo kama zingekuwa hazijachotwa zingetakiwa kukabidhiwa Tanesco achana na fedha zingine za kodi kutokana na mauzo ya HISA na uamisho wa mkataba kwenda kwa mbia mpya.

maana yake kuna case mbili
Tanesco vs IPTL
Machmar vs vip
Sasa naona jamaa wamejificha huko kwenye MACHMAR vs VIP wakasahau ya TANESCO vs IPTL
We just wait and see
Time will display everything in light
 
Back
Top Bottom