Mkuu kumbuka Michuzi analipiwa hizi safari na pesa za walipa kodi, unaposema kila mtu na nafasi yake unamaanisha kila mtu ale nafasi yake, ufisadi utaisha kweli nchi hii?
Truck drivers, hawa wanakuwa wanafanya service, wameajiriwa kwa ajili hiyo, kama hao truck drivers? Je Michuzi analipwa mshahara kwa ajili ya kupiga picha rais anaposafiri? Kama anaposafiri analipwa offpocket allowance, analipwa allowance hiyo mara ngapi kwa mwaka?
Jamani Watanzania, hebu tufunguke macho. Hakuna anayeona kwamba hapa kuna misuse of resources.
naamini kila safari official ina wahusika na sitetei matumizi yasiyo ya lazima, ila najaribu kutetea tusimhukumu michuzi kwa kufanya kazi aliyoagizwa na bosi wake
Kwani hapa nimetoa tuhuma kwa Michuzi? Rudia tena mabandiko yangu.
Ufisadi sio lazima EPA, ufisadi kama huu ndio unaimaliza serikali kwa sasa. Baada ya watu kuona kwamba wizi professional umeshtukiwa, wamehamishia makazi katika safari.
Kama ilivyowekwa hapo juu kwamba kila mtu ale kwa nafasi yake, watu wanakula kweli.
Hakuna anayetaka kuhoji hili kwa sababu ataambiwa na 'wivu'. Ni mamilioni mangapi ya walipa kodi yanalipia watu kwenda vekesheni?
Asante sana Blueray maelezo yako, nimeipata hiyo freudian slip kama ulivyoitumia.
and lets move on
Tu-move forward katika kudiscuss hili au tu-move forward na kudiscuss mambo mengine kwa sababu hili halina mshiko na tuache kumwonea Michuzi 'wivu'?
Yote mawili
... au tu-move forward na kudiscuss mambo mengine kwa sababu hili halina mshiko na tuache kumwonea Michuzi 'wivu'?
Wanapokuwa wanakata ticket huwa waajia ratiba inaisha lini, kwa nini wasirdi nyumbani soonest possible kuokoa pesa za walipa kodi?
What so special with a photo by Michuzi? cant a photo be taken by anybody from the Tanzanian Embassy in the United states? Kwa mfano, kwa nini isiwe lazima kwa secretary wa Ubalozi kujua kupiga picha ndipo aaajiriwe ili aweze kufanya kazi kama hizo inapobidi? Huu ni ufujaji wa pesa za walipa kodi usio wa lazima.
Yupo kikazi ktk msafara wa JK, kwa wabongo kwenda nje kikazi wanaichukulia ni vekesheni, hata mabalozi wetu wako vekesheni.
Inaniuma sana mimi na ma phds yangu sipati safari kama michuzi ndio maana naiunga mkono hii thread
kwani ''Misupu'' kwenda US ni tatizo mpaka tumlaumu JK?Wa kulaumiwa ni JK kwani bila JK huyo Misupu hasingefika huko US
...
Concept za "appearance of impropriety," au "appearance of corruption" bado kweli kweli kwa nchi yetu.
Michuzi ilibidi awe ameshakuwa fired. Kuna siku alihojiwa na Radio Butiama kuhusu tovuti yake, akatamka haya: "...hii blogu ni kama mdudu, akishakuingia hakutoki, na kweli, mimi sasa nimeprove kwamba ni kweli, kwa kweli, yani najikuta kwamba sasa hivi nakuwa dedicated zaidi huko kuliko hata huko Daily News. Saa zote naangalia vitu vya kuwapa wasomaji wangu..." (Full interview hapa)
Kwa maneno hayo tu, ilibidi Michuzi awe fired tayari. Anatumia muda, camera, picha na video toka archive za DAILY NEWS. Mfano, hivi karibuni kuna ka video kaliwekwa DAILY NEWS kanasema "Dewji Speaks on Tanzanian Football...." Kale ka link kakawa hakafunguki. Siku ya pili kakapachikwa MICHUZI blog kakawa kanacheza. Yani bila noma kabisa anachanganya video anazitoa DAILY NEWS anazihamishia MICHUZI, shaghala baghala.
Sasa anachanganya kazi ya ziara ya rais na kuwahoji ma DJ wa Voice of America na "wadau" wengine kuhusu kukutana na Chris Tucker kwenye hoteli DC. Hawezi kuwa vacation maana ana file reports DAILY NEWS toka ziara ianze, na sidhani kama alijilipia tiketi yule. Ana dharau maadili ya kazi blatantly. Ni nidhamu ya kifisadi.
wewe nae.......unajua maudhui ya blog ya michuzi? ile ni blogu yake ana mamlaka ya kuinndesha anavyotaka....mra ngapi kila anaposafiri anasema yuko vekesheni sio lazima aandike wewe unavyotaka aandike.... jamani hii ni very low kwa JFinian.....