Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema leo kuwa wamemuondoa” Waziri wa Ujasusi wa Iran, Esmail Khatib, katika shambulio la usiku kucha. Hata hivyo, Iran bado haijathibitisha kifo cha Khatib.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Katz alisema kuwa “mshangao mkubwa unatarajiwa katika siku hii kwenye maeneo yote ya mapambano,” bila kutoa maelezo zaidi.
“Tutaendelea kuwazuia na kuwawinda wote,” alisema.
Aidha, Katz alisema kuwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameipa jeshi mamlaka kamili ya kuwaua maafisa wengine waandamizi wa Iran wanaolengwa bila kuhitaji idhini nyingine ya ziada.
===========
Israel's Defence Minister Israel Katz said on Wednesday that they "eliminated" Iran's Intelligence Minister Esmail Khatib in a strike overnight. However, Iran has not confirmed Khatib's death.
While announcing Khatib's death, Katz said that "significant surprises are expected throughout this day on all the fronts," without elaborating.
"We will continue to thwart and hunt them all down," he said.
Katz said that Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu has given the military a free hand to kill any other senior Iranian official being targeted without taking additional approvals.
Source: Al Jazeera, Reuters