Israel yaishutumu Iran kuvuka mstari mwekundu

Israel yaishutumu Iran kuvuka mstari mwekundu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,974
Reaction score
871,042
Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema Iran usiku wa kuamkia leo imevuka mstari mwekundu kutokana na mashambulizi yake ya makombora kulenga maeneo ya kiraia hivyo ijiandae kwa majibu makali

Katz amesema mashambulizi ya Iran yatajibiwa kwa viwango vya juu kuharibu uwezo wa Iran kushambulia tena raia wa Israel.

Shirika la habari la Iran International limeonya kwamba taarifa kutoka maafisa wa Israel mpango uliopo mezani kama moja ya majibu hayo ni kushambulia miundombinu ya mafuta na gesi

Iran imesema mashambulizi dhidi ya Israel yataendelea na yatafanyika hadi kwenye kambi za mshirika mkuu wa Israel Marekani zilizopo ukanda huo wa mashariki ya kati

Wakati huo huo asubuhi hii kumeripotiwa mlipuko mkubwa katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mehrabad nchini Iran katika shambulio kubwa la Israel la kimkakati ambalo bado haijafahamika lilikuwa limemlenga nani, Shirika la habari la AP limeripoti taarifa hiyo nmekuekea hapo chini kwenye comments

Pichani ni picha za matokeo ya mashambulizi ya Iran usiku wa kuamkia leo nchini Israel
1749894058482.jpg
 
Pichani juu ni mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel ikizuia makumi ya makombora ya masafa marefu kutoka Iran na chini ni matokeo ya madhara ya makombora machache yaliyofanikiwa kupenya na kutua

Iran inafanyaje kuupenya mfumo wa Iron Dome? Mfumo huo una kiwango maalumu cha idadi ya makombora unaoweza kuyazuia kwa wakati mmoja hivyo Iran inachofanya ni kurusha idadi kubwa zaidi ya makombora hayo ili yanayozidi yapenye hata hivyo Iron Dome inatajwa kwamba imeendelea kufanyiwa maboresho kuongeza idadi ya udhibiti wa pamoja

Kiufupi Israel isingekuwa na mfumo huu thabiti wa ulinzi wa anga majengo yote yanayoonekana pichani yangekuwa majivu kutokana na wingi wa makombora yanayorushwa na Iran kwa wakati mmoja

Israel kwa sasa inalenga kukomesha uwezo wa Iran kuzalisha makombora hayo ya masafa marefu ambapo tayari usiku wa kuamkia jana katika mashambulizi yake ililenga pia kituo kikuu cha Iran cha programu ya uzalishaji wa makombora hayo ya kimkakati

Usikae mbali...
1749895152820.jpg
 
Back
Top Bottom