matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,596
- 15,393
Baada ya Marekani kupeleka meli zake za kivita zenye thamani ya matrillioni. China na yeye anapeleka karibu na Gaza meli zake za kisasa z kivita nne.
Baada ya israel kuharibu uwanja wa ndege wa Damascus na Allepo. Leo dege kubwa la Iran limetua Syria likiwa na shehena za silaha kutumia uwanja wa kambi ya jeshi la urusi. Ikitokea Israel ikashambulia huo uwanja vita haitakuwa ndogo.
Shehena za silaha zinazoshushwa israel, makumi ya madege ya kivita ya US hayakauki Tel aviv airport ni ushahidi kuwa mlengwa sio Hamas. Ni kitu kikubwa zaidi ya hicho.
Kuzidiwa mapema kwa Jeshi la israel siku ya kushambuliwa na Hamas maana baadhi ya vyanzo vinasema sio kweli jeshi lilichelewa lakini lilifika kwa wakati ila hamas waliwazidi nguvu hadi ilipofika mchana. Ukizingatia kauli ya Rais wa Israel leo kuwa Hamas wamejipanga kutumia silaha za kemikali, Ukilinganisha na biti alilotoa Netanyahu ikiwa Hesbullah wataingilia kati, kunauwezekano ili kufupisha vita israel kutumia silaha kubwa kubwa za hatari ikiwemo Nuclear kwa mahasimu wake Iran.
Mvuto mkubwa unaoongezeka kuihusisha Russia, China na US katika vita hivi kama busara isipotumika dunia iko kwenye hatari ya WW3.
Ni hayo tu.