Israel siyo taifa teule

Nasubiri majibu ya maswali yangu.

Unarudia kile kila pasi na ushahidi.

Umemzulia nabii Musa kwamba ameleta Uyahudi,hujanipa ushahidi.
 
Nasubiri majibu ya maswali yangu.

Unarudia kile kila pasi na ushahidi.

Umemzulia nabii Musa kwamba ameleta Uyahudi,hujanipa ushahidi.


Angalia hoja hii:-

TUNAWAJUA WANAOMTAJA ALLAH KWA WINGI HUMO MISITINI NA MAKANISANI, JE WANAOMTAJA ALLAH KWA WINGI NDANI YA MASINAGOGI NI WATU GANI ???!! ( the case is dismissed walonga bazungu 🤣).

Katika kujibu swali hilo ndipo utakuwa umeishajijibu mwenyewe maswali yako.

Na kamwe hutotaka kujibu hilo swali kwasababu ujinga wako wa kung'ang'ania kwamba UYAHUDI NI UKAFIRI utabainika.
 
Nasubiri majibu ya maswali yangu.
 
Nasubiri majibu ya maswali yangu.


Majibu ya maswali yako yapo kwenye swali hili :--

Wanaotaja kwa wingi jina la Allah ndani ya MASINAGOGI wanaitwaje???

Ukishajibu swali hili wala hutohitaji mimi nijibu chochote.

Kwani utakapojua hao ni akina nani basi utajua hao ni Wafuasi wa nani, wanafuata kitabu gani, je wanachofuata ni ukafiri ??? nk,--- so simple indeed.

Na hapo hapo utajiuliza je hao watu wanawezaje kuwa wanafuata UKAFIRI wakati Allah anawatambua kwamba wao humo Sinagogini huwa wanalitaja kwa wingi Jina lake!!

Qur'an ni kitabu cha watu wanaotumia akili sana. A falaa taakiluun??🤣

Na ukome kukufurisha watu hovyo.
 
Mkuu mbona unajichanganya.
Unaongelea israel. Mara unamuweka sabaya. .
Mara unaamini biblia na yesu kristu, na unaamini waisrael. Mara tena ghafla huamini kauli za waisrael tukueleweje mkuu
 
Mkuu mbona unajichanganya.
Unaongelea israel. Mara unamuweka sabaya. .
Mara unaamini biblia na yesu kristu, na unaamini waisrael. Mara tena ghafla huamini kauli za waisrael tukueleweje mkuu
Hata darasani kuna wale slow learner. Nakushauri kama mpe mtu wa karibu yako simu asome halafu akueleweshe.
 
Hao wamebarikiwa full stop. Wako kwenye mikono ya Mungu. Leo unaweza kuona wanateseka lakini ni Mungu anataka wainue macho juu wamwangalie kwa ajili ya ukombozi wao.
 
watu wengi hawasomi biblia a kuielewa dio maana ukisema taifa la israeli ya leo sio teule kama iliokua mwanzo wanruka maili mia tatu ila ukweli ni kwamba waisraeli hata yesu mwenyewe alisha sema katika biblia kwamba wao wameshamkaidi mungu kwa hiyo dunia nzima leo i teule sio wao peke yao..lakini watu wanaenda kanisani kusikiliza maudhui ya mapastor bila hata kufikiria
 
Nasubiri majibu ya maswali yangu. Hapa mpaka ukiri.
 
Nasubiri majibu ya maswali yangu. Hapa mpaka ukiri.



Katika hizi aya kuna majibu ya maswali yako na hapa HUCHOMOKI:-

1-----Hakika WAAMINIO na MAYAHUDI na WAKRISTO na WASABII, YEYOTE miongoni MWAO atakayemuamini Allah na SIKU YA MWISHO na KUFANYA VITENDO VIZURI basi WATAPATA UJIRA WAO KWA MOLA WAO wala haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. ( 2:62) Qur'an .

2 " -----Na lau kama Allah hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka ZINGALIVUNJWA NYUMBA ZA WATAWA NA MAKANISA na MASINAGOGI na MISIKITI ambamo ndani yake JINA LA ALLAH linatajwa KWA WINGI" (22:40) Qur'an .


Je humo kwenye Masinagogi ni watu gani hutaja KWA WINGI jina la ALLAH????---- tunajua Watu wanaotaja jina la Allah kwa wingi ndani ya MAKANISA na MISIKITINI,

Lengo langu utanabahi na uache kuropoka TAKFIR zako za hovyo pale unapojisikia. Unajifanya wewe ndiye Mtume wa TAKFIR uliyetumwa na Allah kufanya kazi hiyo!!! 🤣

Tena wewe nimeishakujua kwa aina ya ubishi wako kwani unazo ID zaidi ya moja humu ndani.
 
Kwahiyo wew unaakili sana kuliko wao kijana , quran imekuja miaka800 baada ya ukiristo je hao Wayahudi walioyajwa walikuwa wanakaa wapi kabda ya quran kukuingiza cha kike
 
Kwahiyo wew unaakili sana kuliko wao kijana , quran imekuja miaka800 baada ya ukiristo je hao Wayahudi walioyajwa walikuwa wanakaa wapi kabda ya quran kukuingiza cha kike
mi habari za quran nazijuaje na huku mi mkristo nilichosema nimesoma kwenye bible kitu amabacho inabidi usome pia
 
Unajua bado najiuliza kwanini hujibu maswali yangu ? Kwanini huonyeshi ya kuwa Mayahudi ni dini gani yaani huonyeshi kwanini mayahudi si makafiri.

Aya ya juu inaonyesha ya wazi ya kuwa Uyahudi na Ukristo ni Ukafiri ndiyo maana Allah akasema sharti la wao kupata ujira ni lazima waamini na watende wema,sasa kama Uyahudi si ukafiri kwanini Allah awape sharti la kuamini na kutenda wema ? Mwanzoni mwa aya Allah ameanza na Waumini ambao ni Waislamu yaani Waislamu tayari wameamini ndiyo maana hakuna sharti hilo.

Lakini kadhalika aya ya pili inatilia mkazo sababu majumba hayo yalikuwa yanatumika kwa ajili ya ibada kwa wale walio amini katika Mayahudi na Wakristo.

Kwahiyo aya hizo bado ziko dhidi yako sababu zimejikita katika kuamini,na simefafanua ya kuwa dini hizo mbili ni Ukafiri na ni Ushirikina,ndiyo maana kuna sharti la kuamini na kutenda mema.

Sasa nakuuliza swali tena hao wamepewa sharti la kuamini nini ? Je kuamini ya kuwa Uzair ni mtoto wa Allah au Issa ni mwana wa Mungu au Utatu mtakatifu ?

Sasa nasema hivi mpaka unakufa hata Gulamu mwenyewe Allah amlaani hakuweza kuthibitisha ya Uyahudi si Ukafiri.

Nakuongezea tena Swali,Ukristo ni dini aliyo ileta nani ?

Sasa sitakujibu tena mpaka utakapo fanya haya yafuatayo :

1. Nataka uthibitisho wa kuonyesha ya kuwa Uyahudi si Ukafiri.

2. Uyahudi ni dini,lakini je ni ile ambayo Allah ameiridhia ? Kama Uyahudi si ukafiri uniambie ni nini ? Sababu katika sura ya 5 aya ya 3. Allah amesema wazi kabisa ya kuwa Dini ya kweli mbele yake ni Uislamu.

3. Maana yake kama Uyahudi si Ukafiri naana yake ni Uislamu. Je wapi ushahidi juu ya hili ?

4. Ulidai ya kuwa nabii Musa alileta Uyahudi. Weka ushahidi huo.

5. Thibitisha ya kuwa kipindi cha nabii Musa uyahudi ulikiwepo.

6. Nini maana ya Uyahudi ?

7.Ukafiri ni nini ?

Nimemaliza,silei ujinga.
 



Maswali yako yote yamejengeka katika msingi kwamba Uyahudi na Ukristo na Usabii sio dini, mimi ninakuambia hizo ni dini tena dini hizo zimekuwepo hata kabla ya Uisilamu huu uliojengwa katika nguzo tano, na ndio maana Allah akatenganisha; Waumini, Wayahudi, Wakristo, Wasabii. Kama makundi yote hayo wangalikuwa ni Waisilamu wa nguzo tano basi lingetumika neno moja tu la WAUMINI, kama jinsi leo mtu akisilimu huwa haitwi kwa dini au kabila lake alikotokea bali ataitwa Muumini au Muisilamu tu.

Wayahudi na Wakristo ndio Wanaitwa kwa ujumla wao "Watu wa kitabu" na wamekuwa wakiabudu ndani ya Makanisa na masinagogi hata kabla Uisilamu huu wa nguzo tano haujafika.


Angalia hii aya:-

Wao wote si sawa . Katika watu wa kitabu wamo watu wanaosimama wakasoma aya za Allah nyakati za usiku na pia wakasujudu.

Wanaamini Allah na siku ya mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanaharakia mambo mema; na hao ndio miongoni mwa watendao mema.

(3:113-114) Qur'an .

Hao watu wa kitabu ndio hao wanaomtaja Allah kwa wingi katika majumba yao ya ibada Masinagogi na makanisa, (ingawa leo hii kuwapata ni shida sana kwani wameishaingia kwenye imani za kishirikina na maandiko yao yameshatiwa mikono), lakini Misingi ya dini zao iliyokuwepo hapo kabla ilikuwa ni misingi ya haki na ndio hiyo misingi Allah anaizungumzia kuhusu hizo dini.

Isitoshe Allah katika (22:67) anasema:-

Kila ummati TUMEWAJALIA kawaida ya ibada wanayoishikilia----.


Sasa inatakiwa usome hizo aya zote kwa pamoja na utafakari sio KUKURUPUKA tu na Kukufurisha dini au watu hovyo!!!---- unakuwa kama "Nabii mkufurishaji"??!.
 
Jibu maswali niliyo kuuliza. Hakuna sehemu niliyo sema UYAHUDI si dini na Ukristo kwamba si dini. Hizi zote ni Dini,ila unaposema kwamba si Ukafiri ndiyo unatakiwa ulete ushahidi.

JIBU MASWALI NILIYO KUULIZA.
 
Jibu maswali niliyo kuuliza. Hakuna sehemu niliyo sema UYAHUDI si dini na Ukristo kwamba si dini. Hizi zote ni Dini,ila unaposema kwamba si Ukafiri ndiyo unatakiwa ulete ushahidi.

JIBU MASWALI NILIYO KUULIZA.


Haya na wewe jibu: Wanaolitaja kwa wingi jina la Allah ndani ya Sinagogi ni watu gani??

jibu swali langu.
 
Hili liko wazi na hao si Wayahudi kidini wala si Wakristo kidini bali wanafata mafundisho sahihi ya mitume,na hawa kiistilahi huitwa "Hawariyuuni", yaani wale watu wote ambao waliwatii mitume wao na kuwafata hawa watalipwa pepo yaani kwa ujumla nao ni Waislamu. Hakuna mtume ambaye hakuwa Muislamu. Na kila mtume alikuwa na "Hawariyuun" wake kama alivyosema Shaykh Swaleh al Fawzaaniy (Allah amuhifadhi).

Ndiyo maana nataka ujibu maswali yangu.

Aya hiyo ni sawa na aya hii katika Qur'aan. Anasema Allah aliye juu :

78. Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka. (al-Maaidah : 78).

Hapa utaniambia hao walio kufuru ni kina nani katika Wana wa Israeli ?

Ama kuhusu aya ya 67 katika sura ya 22.

67. Kila umma tumewajaalia na ibada zao wanazo zishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwendea kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye Uwongofu Ulio Nyooka. (al Hajj : 67)

Hili liko wazi kila nabii alipewa namna yake ya kuabudu na sheria zake ila wote walikuwa na imani moja yaani Waislamu. Watu wa nabii Musa walikuwa wanasali kwa siku mara mbili na sala zao ilikuwa ni rakaa mbili mbili,kadhalika ilikuwa nguo ikapata najisi basi ili kuitoa najisi lazima ukate kile kipande kilicho patwa na najisi hiyo,lakini sheria ya Mtume wetu ni tofauti na hiyo. Kwahiyo hili ni jambo maarufu.

36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha. (an Nahl : 36).

Aya hii inathibitisha ya kuwa mitume wote itikadi yao ni moja.

Kwahiyo bado hujajibu swali hata moja.
 
Haya na wewe jibu: Wanaolitaja kwa wingi jina la Allah ndani ya Sinagogi ni watu gani??

jibu swali langu.
Hili nilishalijbu tangu zamani,laiti kama ungekuwa mtu wa kuelewa na kufata haki hii kadhia ingekuwa imeshapita. Ni wale ambao wameamini katika Mayahudi.
 
Hao wamebarikiwa full stop. Wako kwenye mikono ya Mungu. Leo unaweza kuona wanateseka lakini ni Mungu anataka wainue macho juu wamwangalie kwa ajili ya ukombozi wao.
Kwahiyo wewe umeumbwa ukiwa na laana? Msimsingizie Mungu ushuzi mnaoambiwa na wachungaji. Israel ni taifa kama taifa lingine. Hakuna cha uteule wala shangazi yake uteule. Biblia imeandika kwamba Mungu hawezi kuacha mwenye haki ateseke. Soma Zaburi 23. Wateule wanaoteseka sio wateule wa Mungu bali wa shetani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…