Naona unarudia kosa lile lile. Nasubiri majibu ya maswali yangu. Hakuna aya iliyo onyesha ya kuwa Uyahudi si ukafiri katika ulizo weka wewe.Eti unauliza kama nimeshasoma tafsiri yoyote ya Qur'an tukufu!!!?--- kwani hizo tafsiri zimetoka kwa mtume (saw) ??!!.
Qur'an inajitafsiri yenyewe, hebu angalia hizi aya:-
1----- Kila ummati tumewajalia kawaida ya ibada wanayoishikilia basi wasikugombeze katika jambo hili na uite kwa mola wako bila shaka wewe upo juu ya muongozo. (22:67) Qur'an .
2----Hakika walioamini na mayahudi na masabii na wakristo waliomuamini Allah na siku ya mwisho na WAKATENDA MEMA basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
(5:69) Qur'an
3"------ basi hapana shaka zingalivyunjwa nyumba za watawa na MAKANISA na MASINAGOGI na MISIKITI ambamo ndani yake jina la ALLAH linatajwa kwa WINGI.
(22:69) Qur'an .
Hizo aya tatu zinaonyesha kuwa UYAHUDI SIO UKAFIRI lakini hazijasema kwamba Mayahudi hawawezi kuwa makafiri, tofautisha kati ya UYAHUDI na MAYAHUDI.
Sasa wewe onyesha aya inayosema UYAHUDI NI UKAFIRI.
Aya inayokuchanganya ni hii:-
ان الدين عند الله الاسلام Hakika dini mbele ya Allah ni Uisilamu (3:19).
Kwa uwezo wako mdogo wa ufahamu wewe unaona kwamba hiyo aya anapinga ukweli wa dini zingine, Hiyo inashadidia UKWELI NA UZURI WA UISILAMU DHIDI YA DINI ZINGINE ZILIZOLETWA NA MANABII WALIOPITA, YAANI UISILAMU NI DINI ILIYOKAMILIKA KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA YA BINADAMU, Dini zingine hazijakamilika na vitabu vyao vimeishaingizwa mikono na kama atapatika mtu mwema katika dini hizo ALIYEMUAMINI ALLAH na SIKU YA MWISHO na KUTENDA MEMA (5:69) basi hatakuwa na khofu na hatahuzunika, na hii ni pamoja na Waumini (Waisilamu)----- kumbuka yule anayemuamini Allah ni lazima pia atamuamini mtukufu mtume (saw).
Usipokubali jambo hili basi basi utasababisha ikhitilafu katika aya za Qur'an, (aya 5:69 na aya 3:19).
----Unataka kujua maana ya ukafiri na ushirikina----.
Je Kwanza umeelewa tofauti kati ya UYAHUDI na MAYAHUDI ? ??, mbona warukia mada mpya??
Naona unarudia kosa lile lile. Nasubiri majibu ya maswali yangu. Hakuna aya iliyo onyesha ya kuwa Uyahudi si ukafiri katika ulizo weka wewe.
Pili,hujajibu maswali yangu na sijatoka nje ya mada.
Tafsiri zinatoka kwa mtume na aya hujifasiri kwa zenyewe ila si kwa namna unayofanya wewe.
Nasubiri majibu ya maswali niliyo kuuliza.
Weka ushahidi unao onyesha ya kuwa nabii Musa amekuja na dini inayoitwa UYAHUDI. Ukiweka hiyo na mimi nakuwa Qadiani kama wewe.Hapo nilivyofafanua kwa mujibu wa aya za Quran huwezi kuwa na swali bali kujibaraguza tu.
Uyahudi ni dini aliyokujanayo nabii Musa as, Taurati ndicho kitabu cha sheria alichokuja nacho na nyumba zao za ibada zinaitwa Sinagogi na wafuasi wa hiyo dini wanaitwa Mayahudi, wanaweza kupatikana wayahudi wema au wabaya na Uyahudi usilaumiwe kwa mabaya ya Wayahudi jinsi ambavyo wanaweza kupatikana waisilamu wema au wabaya na Uisilamu usilaumiwe kwa mabaya ya Waisilamu.
Hapo utakuwa umepata somo, waila wapi imesemwa UYAHUDI NI UKAFIRI???.
Weka ushahidi unao onyesha ya kuwa nabii Musa amekuja na dini inayoitwa UYAHUDI. Ukiweka hiyo na mimi nakuwa Qadiani kama wewe.
Kadhalika nilikuomba uthibitishe ya kuwa kipindi cha nabii Musa Uyahudi ulikuwepo. Hili najua mpaka unakufa huwezi.
Nimeshakuwekea aya huko nyuma zinazo onyesha ya kuwa Uyahudi na Ukristo ni ukafiri.
Kadjalika nilikuuliza Ukafiri ni nini na Ushirikina ni nini ? Hili huwezi jihu sababu ukijibu utakuwa unadhihirisha ujinga wako.
Nasubiri ushahidi na majibu ya maswali yangu,uwe unaweka hoja.Allah anasema katika Makanisa, MASINAGOGI na misikiti humo jina lake linatajwa sana, sasa tuambie humo kwenye MASINAGOGI ni watu wepi hufanya ibada???
Mishipa ya shingo, macho na povu zinakutoka kuwakufurisha Watu ambao Allah anawatambua kwamba miongoni mwao watu wema wanaweza kupatikana!!!--- unajipa hati miliki ya kukufurisha watu kana kwamba wewe ndiye MTU SAFI SANA na wengineo unaweza kuwaita MAKAFIRI kwa utashi wa nafsi yako utadhani dini ni urithi binafsi uliopata kutoka kwa Babu yako!!!.
UYAHUDI SIO UKAFIRI JINSI UISILAMU AU UKRISTO SIO UKAFIRI lakini waumini wa dini hizo wanaweza kuwa makafiri.
Hadi somo likuingie akilini.
Nasubiri ushahidi na majibu ya maswali yangu,uwe unaweka hoja.
Nabii Issa aliacha Ukristo ? Maana yake wanao zungumziwa hapo ni wale walio amini ndiyo maana katika aya Allah amewatoa na akatumia majina ya Uyahudi na Ukristo kuweka bayana,ila Uyahudi na Ukristo ni Ukafiri na Ushirikina kama nilivyo weka aya huko nyuma.
Maswali yangu najua huwezi kujibu ndiyo maana unayakimbia,lakini hapa mpaka ujibu maswali niliyo kuuliza.
Shusha vifungu vya biblia vilivoandikwa kuwa tuibariki Israel au tukiilani tutalaaniwa.
Kabla ya Misri hawa watu hawajawahi kuwa na kwao mweee. Waliwakuta waamori wakawapiga mishale na upinde.
Mungu alimwambia ondoka Ibrahimu needs nchi ya mbali.....huko ndiko kumeleta balaa. Sijui kwanini Mungu alimtaka Ibrahimu aondoke.
Nasubiri majibu ya maswali yangu,unachofanya hapa unarudia kile ulicho kidai huko pasi na ushahidi.Hapo katika hii aya (2:62) Allah ameanza na maneno "Hakika waaminio" halafu baadaye akaendelea kutaja "Mayahudi na Wakristo na Wasabii---"
Kama hao Mayahudi na Wakristo na Wasabii wangalikuwa ni waumini (Waisilamu) iweje sasa ataje majina ya imani zao???, mfano leo mkristo akiwa Muisilamu itafaa aendelee kuitwa Mkristo wakati kisha kuwa muumini wa kiisilamu???!!--- hiyo ni hoja mfu bali muflisi. Waaminio waliotajwa katika aya hiyo na zingine nyingi ndani ya Qur'an zinawakilisha Waisilamu walioamini.
Angalia hizi aya zinayowaweka Mayahudi na Wakristo na Masabii katika kundi moja la Watu wa kitabu.
"Wao wote si sawa. Katika watu wa kitabu wamo watu wanaosimama wakasoma aya za Allah nyakati za usiku na pia wakasujudu.
Wanamuamini Allah na siku ya mwisho na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanaharakia mambo mema; na hao ndio miongoni mwa watendao mema.
Na heri yoyote watakayoifanya hawataikataliwa; na Allah anawajua wamchao".
(3:113-115) Qur'an
Hapo utaona Allah kawa categorise Mayahudi na Wakristo na Wasabii (watu wa kitabu) na kawaacha Waumini katika hiyo aya, sasa huwezi sema Waumini, Wayahudi Wakristo na Wasabii ni watu wa dini moja au imani moja nk, wakati katika aya ya (22:67) inasema kila umma Allah umeupangia njia yake ya ibada.
UYAHUDI SIO UKAFIRI, lakini wayahudi wapo wengi makafiri.
Na ukome kuwakufurisha watu ambao yawezekana imani yao ni kubwa kuliko imani yako.
Nasubiri majibu ya maswali yangu,unachofanya hapa unarudia kile ulicho kidai huko pasi na ushahidi.
Unarudia swali ambalo nimeshalijibu.Hebu na mimi jibu maswali yangu basi:--
Msikitini wanaswali Waisilamu, je katika Sinagogi na kanisani wanaswali watu gani??? (Kumbuka katika nyumba hizo jina la Allah linatajwa kwa wingi kwa mujibu wa Qur'an).
Wapi Quran inasema UYAHUDI NI UKAFIRI?? (Kumbuka ni UYAHUDI na sio Mayahudi).
Unarudia swali ambalo nimeshalijibu.
Mpaja najiuliza kwanini hujibu maswali yangu...?
Nasubiri ushahidi. Na unatakiwa utubu kwa kumzulia nabii Musa UONGO kwamba amakuja na dini ya Uyahudi.Mimi narudia kwa namna tofauti ili akili yako huenda ikakaa sawa ili uache tabia ya kukufurisha watu kama kwamba wewe umepewa dhamana na Allah kukufurisha watu, unapokufurisha watu yapasa na wewe ujichunguze imani yako kwani yawezekana wewe ni muovu sana kuliko huyo unayemkufurisha.
Jambo la pili wewe huwa husomi Qur'an kwa tafakur ndiyo maana nimekuwa nakupa aya ili ukae kitako uzisome.
Maswali yako yameshajibiwa na aya nilizokwisha toa.
Wewe tu ndiye unayeshindwa kujibu swali la msingi wa majadiliano yetu; Ni wapi Qur'an inasema UYAHUDI ni UKAFIRI??? (Kumbuka kuna tofauti kati ya Uyahudi na Mayahudi).
Swali jingine ni hili; Je ni watu gani huwa wakiswali ndani ya Sinagogi (ambamo humo hutajwa jina la Allah kwa wingi)???
Angalia kamusi huenda itakusaidia kidogo kujua Sinagogi (Synagogue) ni nini.
Kwani kuna; Msikiti / Mosque, Kanisa/Church, na Sinagogi/Synagogue ambamo kwa mujibu wa Qur'an jina la Allah hutajwa kwa WINGI ndani ya nyumba hizo.
Uyahudi sio Ukafiri, ni dhambi kubwa kukufurisha kitu ambacho Allah hajakikufurisha: احفاذ لسنك chunga ulimi wako Mtume saw alisema kwani ulimi ni kiungo komojawapo kinachoweza kumchumia mtu madhambi.
Ulitaka biblia iletwe na nani,kama si Mungu kuwatumia watu au kisa ni wazungu na waarabu vipi leo waafrika tunavyokwenda kuhubiri nje.Bible ililetwa wakati wa ukoloni, wazungu walichukuwa Mali zetu wakaacha mashimo na Bible sisi tukashikilia Bible. Uislamu uliletwa wakati wa utumwa ukaanzia pwani na njia za watumwa walikopitia.
Nasubiri ushahidi. Na unatakiwa utubu kwa kumzulia nabii Musa UONGO kwamba amakuja na dini ya Uyahudi.
Kisha uniambie hizo aya Mtume alizifasiri vipi na maswahaba zake walizielewa vipi na kuzifanyia kazi vipi.
Hujaweka ushahidi unao onyesha ya kuwa Uyahudi si ukafiri,yaani najiuliza mpaka nashangaa yaani aya iko wazi inasema kabisa wale walio amini katika Mayahudi mbona aya haukusema wale walio amini katika Waislamu ?
Hujajibu maswali yangu.
Uyahudi ni UKAFIRI na ni USHIRIKINA.
Mimi siamini kama kuna Mungu na wala siamini katika dini yoyote hii ikijumlisha hata dini za asili za mababu zetu lakini kwa reference ya Bible kama unaiamini basi usiiamini vipande upendavyo na kuacha usivyovipenda kwa sababu zako binafsi, Bible inatanabaisha ya kuwa Israel ni taifa teule la Mungu.
Acha kudanganya watu kwa kujifanya unajua mambo kumbe ni pumba tupu. Ur ya kaldayo ipo Iraq ya kusini. Iraq na uturuki wapi na wapiSio kweli kwani makabila mengine ya Waarabu yalikuwepo kabla ya Ibrahimu hajahamia maeneo hayo kutoka Ur ya Kardayo (Uturuki) na moja ya makabila hayo ni Wafikisti (Philistines ,Wapelestina).
Waarabu waliokuwa uzao wa Ibrahimu ni Waismael wana wa khedari na wengi wao walitokea Saudia mahali ambapo Ismail aliishi yeye na mama yake baada ya kuachwa na Ibrahimu eneo hilo na baada ya miaka kadhaa Ibrahimu aliporudi eneo hilo kipindi Ismail kisha kuwa mkubwa na eneo hilo limeshakuwa na majazi ya watu kwasababu Maji ya zamzam yalikuwepo hapo, ndipo Wakainua kuta za nyumba tukufu ya makka, hao watu waliojumuika hapo kwenye hiyo chemchem na kufanya makazi hapo Walikuwa ni Waarabu ambao sio Wazao wa Ibrahim (as) ni kutokana na hao Waarabu ndimo Ismail alipata mke.
Unapozungumzia Waisraeli lazima Uanze hivi:- Ibrahimu----Isihaka--- Yakubu (Israeli)---Makabila/koo 12 za waisraeli.
Na unapozungumzia Waarabu WALIITOKANA NA Ibrahimu unatakiwa uanze hivi: Ibrahimu---Ismail----- khedari-----Waarabu wa Ismail. Hivyo utaona sio waarabu Wote wametokana na uzao wa Ismaili au uzao wa Ibrahimu.