Israel kumsaidia Trump dhidi ya Kim

Israel kumsaidia Trump dhidi ya Kim

hujui hata historia. nenda kasome ujerumani ilipigana vita na mataifa mangapi ulaya na kuyatawala.
ok.inawezekana ni hivyo sijui,ninachojaribu kuandika ndio ukweli.hapo hoja ni kukuzwa mno kiuwezo kivita kwa israel dhidi ya maadui zake.nimetumia historia ili kuweka sawa kumbukumbu kuwa ni kwa nini inakuzwa?kipi kimeikuza.Isreal still ipo ivo huwezi kuifananisha dola la Rumi ya kale ya akina Constantine II au Nero N.K.wala akina Hitler,Israel bado ipo na ipo kileleni mwa mafanikio kiteknoloji hasa madawa,kilimo,silaha n.k. mfano timu mbili za mpira zinapotaka kupambana wachambuzi watachambua uwezo wa kila timu kwa kuangalia na kuichambua kila timu kwa haki historia yake mafanikio yake katika mashindano mbalimbali,mwishowe uwezo wa sasa kwa kuangalia vikosi vyao.hapo unaweza pata picha timu gani ipo kwenye nafasi ya kushinda dhid ya mwenzake japo kuna matokeo ya kushangaza pia.mathalani real madrid ikicheza yanga dar es salaam ni waz madrid kupewa nafas ya kushinda.
 
Swali

Je israel ina fight yenyew kama yenyew au inakuwa na msaada toka sehemu flani

Je israel inaweza kujiendesha yenyewe kama yenyew bila msaada kutoka chanzo chochote
Majibu ni Laa! Bali dola kubwa kubwa tu zinailinda lasivyo ingebaki stori tu
 
Mkuu kitu kimoja nilichojifunza kwa waisrael huwa hawapendi kuonekana ni wababe na wananguvu wakihojiwa mfano kuna Mossad wastaafu wanaongea wazi kabisa kuwa Israel haina nguvu ya kumpiga Iran, Hezbollah, haman nk....wewe ingia YouTube utaona......alafu ishu nyingine Israel huwa aanzishi ugomvi Ila kombora lolote likigusa ardhi ya Israel tena mbaya Zaidi ikaua raia wake, malipo yake utayaona
Israel mwaka huu huu kashambulia kiwanda cha silaha huko somalia, mbona hajaenda kuishambulia Iran sponsor wa Hezbollah?
Kama kawaida yake anaonea mapanya tu mapaka analalamika.
Juzi juzi tu kaishambulia syria, bado anaikwepa Iran.
Nashangaa sana watu mnao under estimate uwezo wa hao waajemi Israel na Marekani wao hata hawamchukulii poa huyo Muajemi, ila tu Mtanzania ndiye anamchukulia poa.
Sasa hivi nchi nyingi zimejiweka vizuri hata kama wakipigana vita wakashindwa ila hiyo vita haitowaacha salama, haitokuwa vita kama ya gang la USA na Iraq, wala vita ya siku 6.
Kama unadai ex mossad agents wanasema kuwa Israel haina uwezo wa kumpiga Iran, we ni nani mpaka uwaze wanadanganya hawajikwezi? Kwanini usikubariane nao kuwa wanasema ukweli maana wao ni former Mossad agents kama ulivyosema mwenyewe.
 
Kiziwi amuombe msaada kipofu wa kusomewa barua.
Israel inakuzwa tu kisa inaonea vipanya ikikutana na wababe utasikia wamekimbilia UN wanapiga kelele.
Inaonea vipanya. Hao wababe ni kina nani? Isreal interest yake kubwa ni kuhakikisha taifa lao liko salama na ukitaka kujua wao ni panya wa aina gani hebu tishia taifa lao.
 
Iran kamtishia mara ngapi mbona hamshambulii analilia lia UN,
Kama kaweza vuka bahari kaifuata Somalia kushambulia kiwanda cha silaha anashubdwaje kuishambulia Iran sponsor mkubwa wa Hezbollah ambaye ni mshambuliaji mkubwa wa Israel?
 
Mkuu siku zote Israel huwa anatoa warning kwa raia wa kawaida kuwa wanakuja kushambulia, hii inafanyika ukanda wa Gaza na Huko Kwa Hezbollah, shida huwa inakuja kwa hao wanamgambo kuwakataza na kuwatishia raia wa kawaida kuwa wasiondoke maeneo yao na kinachotokea ni kuuwawa kwa hao wanamgambo na raia.....waarabu hawathamini saana miili yao wao wanaona kufa ni kitu cha kawaida tu.....alafu ugomvi wa Israel na Wanaojiita wapalestina hautaisha leo wala kesho, chamsingi tuwaache tu kama walivyo maana ndo maisha walioamua kuishi,utafanya nini sasa
Tufanye yetu tu
 
Israel mwaka huu huu kashambulia kiwanda cha silaha huko somalia, mbona hajaenda kuishambulia Iran sponsor wa Hezbollah?
Kama kawaida yake anaonea mapanya tu mapaka analalamika.
Juzi juzi tu kaishambulia syria, bado anaikwepa Iran.
Nashangaa sana watu mnao under estimate uwezo wa hao waajemi Israel na Marekani wao hata hawamchukulii poa huyo Muajemi, ila tu Mtanzania ndiye anamchukulia poa.
Sasa hivi nchi nyingi zimejiweka vizuri hata kama wakipigana vita wakashindwa ila hiyo vita haitowaacha salama, haitokuwa vita kama ya gang la USA na Iraq, wala vita ya siku 6.
Kama unadai ex mossad agents wanasema kuwa Israel haina uwezo wa kumpiga Iran, we ni nani mpaka uwaze wanadanganya hawajikwezi? Kwanini usikubariane nao kuwa wanasema ukweli maana wao ni former Mossad agents kama ulivyosema mwenyewe.
vita wakati mwingine hutawaliwa na propaganda jiongeze.akina masawi bwire na Thobias Kifaru ni wengi nako huko.yuko wapi sahaf/sjui shahaf wa irak?
 
Hizo propaganda mbona hazifanyi syria ambako kila mara anapeleka midege yake tu?
Kwanini anazifanya kwa Iran tu?
Jibu ni moja tu na liko wazi kuwa Iran siyo ya mchezo mchezo ndiyo maana analialia isipate kutengeneza nukes ambazo napo last week wao israel wamesema taarifa walizonazo nikuwa tayari waajemi wana nuclear war heads.
 
lakini kwa nini unapenda kuona iran inashambuliwa na israel?kwa nn usitaman aman?
 
Hakuwezi kuwa na amani wakati kuna wanaokandamizwa.
Kuna wanaojiona bora kuliko wengine na kuna wanaotaka fanya watakavyo lakini wengine wasifanye.
Now mwendo wa jino kwa jino
 
sasa nani anakandamizwa na nani,pia anajiona bora?ivi wewe ni raia wa nchi gani?unafikiri vita ndio suluhisho la kuleta usawa duniani?athari za vita hazitaiacha dunia salama.naomba wapigane miaka mia ijayo pengine ntakuwa sipo
 
Kati yao wawili nani anaongoza kushambulia wenzake? Si Israel na bwanake USA.
Nchi nyingine zimeona mfano, kilichotokea Afghanistan, Iraq, Libya n.k kimefanya nchi nyingine ziwekeze zaidi kwenye silaha za kivita maana wanasema mwenzako akinyolewa zako tia maji.
Israel imeshambulia nchi nyingi kwa kigezo eti wadhamini wa ugaidi.
Hivi unajua ni mara ngapi Mossad ilijaribu kumuua sadam bila mafanikio?
 
tunakoenda sio salama,joto la vita kuu ya tatu ya dunia limepanda sana.hali shwari.
 
Kwani Trump ni mwanachama wa Jamiiforum? au huwa anaingia kama guest hum?
 
Back
Top Bottom