Ismail Jussa na siasa katika ELIMU


Mkandara,

..Prof.Malima alidai kuna hujuma ktk mfumo mzima wa usahihishaji mitihani.

..akaenda mbali na kudai kwamba wanafunzi hawatumii namba za mitihani wakati anajua fika kwamba namba za mitihani zilikuwepo tangu hajateuliwa kuongoza wizara hiyo.

..mimi nadhani tatizo letu ni kwamba linapokuja suala la elimu tunajali zaidi QUANTITY kuliko QUALITY. hata Prof.Malima alikuwa anajadili "idadi" na siyo "viwango."

..wakati wa zoezi la UPE serikali iliweka umuhimu mkubwa ktk kuandikisha watoto wengi shule ya msingi bila kuhakikisha kwamba watoto hao wanapatiwa elimu inayokidhi viwango.

..shule za sekondari za kata nazo zimeanzishwa kwa mtindo uleule, na mentality ya enzi za zoezi la upe. tumejikita ktk idadi na siyo viwango.

..kwanini wananchi wajenge shule 10 zisizo na waalimu wa kutosha, maabara, na maktaba? kwanini wasianze na shule 3 zilizojitosheleza?
 
Angewashauri wazanzibari wenzake wavunje muungano angekewa amefanya jambo la maana na ndio njia pekee ya kukwepa vitu kama NECTA
 
Mkuu Mkandara, nakubaliana na wewe ila hoja yangu goes a bit beyond kwamba we need delibarate affimative actions kwa muslims na wazanzibari ili kubalance the equilibium ya usawa katika elimu ya juu!.

Muundo wa BOT gavana lazima atoke bara, na naibu gavana lazima atoke Zanzibar, tangu tumeiunda miaka mingi ilipita bila kuwa na naibu gavana kutoka Zanzibar eti kwa sababu hakuna Wanzanzibar wenye sifa!, aliyepo sasa inadaiwa hana sifa ila kapewa tuu ili mradi!. naamini kuna Wanzanzibar wanauwezo only if kama wakiwezeshwa kujaza nafasi hiyo kihalali na sio kwa kupewa tuu!.

Nimepita pale UDSM lazima tukubali tukatae mfumo wetu wa elimu uliwapendelea watu wa dini fulani, baada ya kulitambua hilo, ilibidi affimative action ifanyike kwa walionyuma kupaishwa huku waliombele waki mark time ili tulingane tusonge mbele pamoja!.

Huu ni ukweli mchungu kuubali ila watu wote amba wako just genuinely hili wanalijua, unless nao walifumbia macho tuu kwa kuendekeza udini wa preference za dini zao!,

We need affimative action!.
 

Ndinani,

..siyo kwamba watu ni wazembe, lakini there is no incentive ya kumpeleka mtoto shule.

..kwanini mzazi masikini alazimishwe kumpeleka mwanae kwenye shule yenye wanafunzi sitini na waalimu wawili?

..halafu mtoto anapoteza miaka minne baadaye mnamwambia mzazi kwamba mwanawe amefeli.

..unajua hata kule kwenye maeneo yenye mwamko wa kielimu waliona the difference btn mtoto aliyeenda shule na aliyebaki kijijni kuchunga ngombe na kulima mashamba. tofauti hiyo ndiyo iliyopelekea wengi wakapeleka watoto shule.
 
hebu tazama hii picha, kisha huitaji kuelezwa kama huyu ni timamu ama laaah....unajua Kisaikolojia unaweza kumtafsiri mtu hata kwa picha



Ukiangalia vizur hii picha utaona vizuri madhara ya UBWABWA.
Ukiangalia sura ya huyu kiumbe hai(ingawa sina uhakika) utagundua ni sura iliyojaa majonzi na majuto tele.
Tuwe tunawasamehe watu wa aina hii
 

Jusa amechanganyikia,huwezi kuwa mwanasheria ukawa unaongea utumbo kiasi,mfano akitoa taa
https://www.jamiiforums.com/newreply.php?do=newreply&p=3302203
 

Pasco,

..I disagree with the form of affirmative action ur proposing.

..mimi napinga quota system, badala yake napendekeza tujielekeze kuhakikisha kwamba elimu yenye viwango ni haki ya kila Mtanzania bila kujali kabila, dini, au jinsia.

..hii elimu tunayoizungumzia hapa imeletwa na dini nchini kwetu. it is understandable kwamba kutakuwa na disparities ktk suala zima la elimu baina ya dini mbalimbali.

..matatizo ya elimu yanahitaji our collective efforts as a nation kuyatatua. badala ya kutumia udini kushughulikia matatizo hayo, labda tutumie kanda, mikoa, etc ili tuweze kuwa kitu kimoja.

..my point ni kwamba Muislamu wa Kagera ana nafasi nzuri kielimu, kuliko Mkristo wa Sumbawanga. Kwa hoja hiyo tunaweza kuweka udini pembeni tukashughulikia matatizo haya kama Watanzania.
 

kama anataka kuvunja muungano labda,akaanze na ule wa east timor kisha atue mumbai ale pilipili
 

Duu! sijawahi kuona mtu anayejiita msomi halafu anakuja na stori za kijiweni na kuzigeuza utafiti!
Mkuu barubaru naskia wewe ni mahiri sana wa mashairi na ngonjera na nadhani ndo kipaji chako!
Tafadhal usifananishe masuala yanayohitaji utafiti kuwa kama tenzi za ngonjera na mashairi yako! poor you!
 
Mkuu Joka Kuu, kutoa mtihani mmoja kwa mwanafunzi aliyeanzia madrasa vs aliyeanzia nursery matokeo ndio hayo!? Sijui Zanzibar wana Div 1 ngapi!. Performance ya shule Kiislamu ndio indicator, we have a serious problem that needs serious addressing it!. Last year nilikuwa SA na kuna idadi kubwa ya Watanzania stranded and living in destitute ukiasikia majina yao, they leave something to be desired!.

Japo hakuna proper research kuhusu ni kina nani waliojaza jela zetu you'll be surprised!. Tuna tatizo ambalo tunalifungia macho!, wakija hapa Al Qaeda, Al shabab na Boko haram, you will be surprised who would be the recruit!.

Lets face the issue sio denial!.
 
Mkuu wangu ni lazima tuwe tunajiuliza maswali magumu, na kutafuta njia bora kwa rtaabu na kujitoa mhanga kuliko kutafuita mchawi...
Haya pengine twende tararibu..
1. Ikiwa namba za watoto ndizo zinatumika ktk kusahihisha mitihani kwa nini matokeo yanaandikwa majina ya watihaniwa.. hayo majina wameyapata wapi badala ya namba zao..hakuna wakati wowote namba zimetumika kutoa majibu ya watihaniwa iweje tuseme zinazotumika ni namba kusahihisha? hali ukitazama vyuo vinavyotumia namba hutoa hata majibu kwa kunukuu namba hizi na sio majina. Ni wkaati gani namba zinabadilika kuwa majina na kwa nini walitumia namba ikiwa orodha ya matokeo zinatolewa kwa majina?.

2. Na kama Kigoma Malima ambaye alikuwa waziri wa ELIMU alisema namba zitumike kusahihisha mitihani badala ya majina wakati (kwa madai yako) namba ndio zinatumika... huoni kama unajikanyaga hapo! Sasa kwa nini ilikuwa issue kubwa sana kukubali kutumia namba badala ya majina na nakumbuka vizuri sana mgogoro wa matumizi ya namba dhidi ya majina.

Huwezi kunionyesha mahala hata sehemu moja ambayo Malima alikuwa akijali QUANTITY na sii QUALITY wakati hatukuwa na shule za kutosha kabisa na ndipo alipogundua kwamba sii kwamba watu walikuwa wakishindwa mitihani bali nafasi za kwenda Sekondary, High school na University. Na kikubwa zaidi hadi anaondoka Chuo kikuu cha Dar na Mziumbe vilikuwa katika vyuo bora duniani na sio Tanzania tu..Shule za msingi waliandikisha watoto wachache kuliko wakati wote na record zipo..hii quantity gani unayozungumzia.

3. Mkuu wangu swala la quantity hili amekuja nalo Lowasssa na JK lakini ndani ya mfumo ule ule ulojengwa wa kujuana. Nakubaliana kabisa na ndugu yetu alohoji hapo nyuma kama ni haki tunatakiwa kuwasaidia waloshindwa tukaacha watu waliofanya vizuri. tatizo siii kuwasaidia wala sikubaliani na Pasco ktk kuwapa tafu Wazanzibar kwa sababu wanalalamika isipokuwa kinachotakiwa ni kurekebisha mfumo mzima wa ELIMU. Na sipendi kurudia rudia hoja yangu maana watu watanielewa vibaya na tutatoka ktk mjadala huu lakini mfumo wa ELIMU nchini ni mbovu toka waandalizi, Wadau na washirika wa Idara zinazohusika hadi Shule zenyewe.

UTU wa binadamu yeyote huanzia ktk ELIMU, kumnyima mtu elimu ni sawa na kuwacha Mnyama pori maana hata hao huwa tamed..Inashangaza sana kuona watu tunashindana kwa asilimia 9 ya washindi, huoni kama ELIMU imekuwa sawa na sinia la Biriani lilowekwa ktk kundi wa watu 10. hata yawepo masufuria mangapi mpango wa shule unatakiwa uboreshwe. hadi leo hii tunavyozungumza kuna shule zina watoto zaidi ya 100 darasa moja na walimu wawili tu. Kinachofanyika ni sawa na mgao wa Umeme unakatika sana sehemu za Uzalishaji na biashara lakini sii Mikocheni na Msasani kwa viongozi. Hii sii akili hata kidogo mkuu wangu.
 


Aaaaagh....Jussa tena...
This guy is a virus....Always talking ****...

Hivi Jussa ni lazima uwe unaongea kila kitu jamani...? remember "A silent fool is considered wise" , at least try this...
 

Ukistaajabu ya musa utaona ya bokoharam. Elimu iliyopo imeletwa na wazungu hasa wamissionary. Sababu hii ni tosha kukuta wakristo wengi wamesoma. Lakini jambo la kushangaza huko wanakosahihisha na kupanga matokeo hakuna waisilamu kwenye team? Kama wamo wajitokeze waeleze ukweli. Kama napo huwa hawapangwi kwenye team hizo basi ielezwe. Maana hapa kuna watu wana incite u-boko haram kwa mambo ya kizushi tu.
 

Mkandara,

..hivi wewe kwenye mitihani ya taifa uliandika namba, au jina?

..ninavyoelewa mimi kinachosahihishwa ni paper yenye namba ya mtahiniwa.

..unadai vyuoni hawatumii majina: je, umeshawahi kuona shahada ya chuo kikuu imeandikwa namba ya mtihani[usajili] ya mhusika na siyo jina lake?

..mfano mmoja wa Malima kujali quantity na siyo quality ni kuanzisha mtindo wa double session ambapo aliongeza idadi ya wanafunzi wanaochaguliwa kwenda sekondari pale dsm bila kuhakikisha kwamba ubora wao kitaaluma unawaruhusu.

..zaidi, kipindi cha Malima mtihani wa form 2 ulioanzishwa na waziri Jackson Makweta mtangulizi wake ulisitishwa.
 
Mkuu wangu nimesoma zamani enzi ya Nyerere lakinia najua fika kwamba unatakiwa kuandika Jina na namba na unaweza kwenda site ya NETCO to verify isipokuwa sina uhakika mtihani wa darasa la saba ndio wanatumia namba. Mkuu mimi mzazi kwa nini nilalamikie kitu kisichokuwepo? Nataka ku gain kitu gani au itanifaidisha nini?

Kuhusu vyuo vikuu unazunguzia vyeti, mkuu wangu nchi gani wanaandika namba ya mtu kwenye cheti? Mbona nageuza maneo sisi tunazungumzia kusahihisha mitihani na utoaji wa majibu. Swala hili limezungumziwa toka enzi za Malima kwa nini tunatafuta visingizio badala ya kulitazama tunakosea wapi.

Tena siku hizi mwanafunzi anatakiwa kukaa mtihani na kuufanyia kupitia PC tu hasa haya maswali ya kuchagua ndio rahisi kabisa.Kila mahala penye mkono wa mtu mwenye njaa lazima zitakuwepo hila mbaya za magendo. Mkuu nafasi ni chache hata mimi naweza poteza Uzalendo kununua mtihani kwa ajli ya mwanangu ikiwa najua itanigharimu zaidi ya Mil 4 kwa mwaka kuingia Private.
Mkuu wangu nimnepitia report ya elimu nchini na kukuta kwamba wakati Mwinyi hadi Mkapa mwanzoni ndio elimu ilishuka zaidi ktk usajili kutokana na kuwekwa karo pia asilimia 5 kwenda sekondary na asilimia ndogo zaidi kwenda High schools, vyuo na University sasa hizi hadithi za Quntity zinaushahidi gani?Nipe hesabu ya wanafunzi waliokwenda UDSM tofauti na miaka iliyopita au iliyofuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…