Plancscale,
Ndiyo maana mimi nikasema kuna haja ya ku-rexamine hiyo designation ya "Islamic banking". Kama inahusu mambo ya no interest, bila ya kitu kingine ambacho kiko uniquely Islamic, basi iwe "No Interest loan".
After all kuna wakomunisti, wasoshalisti, wakristo etc, wanaamini interest katika mikopo ni exploitation/ unethical/ au hata dhambi fulani hivi. Na wanaweza kukupa misahafu yao invyosema.
Sasa swali langu ni, what is uniquely Islamic about these loans. I'm talking core issues apart from labelling and bismillahing here and there.
Maana unaweza kukuta tatizo ni labelling, Wakristo na sisi atheist hatutaki kutumia service inayoitwa "Islamic banking" wakati hatuamini uislam, lakini tunaona kabisa hii service itatufaa kwa imani zetu kwamba interest ni exploitation.
Kama ni hivyo unaondoa label tu, unaondoa tatizo.
Tatizo sasa kila mtu atataka no interest banking, banking system inaweza ku collapse hivi hivi.
Kulikuwa hakuna benki ya aina hiyo na huwezi jua pengine walikuwa hawachukui riba inawezekana viongozi wa jamii za dini hiyo ndiyo waliyoshindikiza kuwepo na account za aina hiyo. Siyo vizuri kujudge bila ya kuwa na data kufanya hivyo ni udaku
mwanamayu ......hebu tuwekee wazi kipengele katika kanuzi za BOT ambacho kimevunjwa.
hapa naona ni kuvutiana mpira tu ...............kundi moja linasema imevunjwa moja linasema haijavunjwa.
sheria imevunjwa vipi? isitoshe sidhani kama hiyo huduma imewekwa kutokana na shinikizo la mufti ( he is a nobody......sasa tu anakula ujiko utasema kaiomba yeye). .....kama nawewe hutaki kulipa riba jiunge kwenye islamic banking au ndio hatuwezi kujiunga japo kama ina faida as long as imeitwa islamic banking? kama ni hivyo we have a long long way
Mimi ninadhani baadhi yetu tunachangia bila kufahamu undani wake. Kwa maoni yangu mtu awekapo pesa benki anatarajia faida itokanayo na benki kuifanyia biashara pesa za mteja. Benki hiyo inaweza kukopesha ujenzi wa viwanda vyo vileo na vitu vingine ambavyo kwa waislamu ni haramu, pili hata kama benki haitowekeza kwenye mambo ya vileo, katika uislamu riba[interest] ni haramu. Kutokana na hali hiyo baadhi ya benki zimegundua namna ya kupata faida zaidi kwa kufungua account za aina hizo kwa waislam ili wapate faida mara mbili kwani muislamu akiweka pesa zake katika account za namna hii hatarajii faida yoyote ile. Kimantiki hata mkristo au dini yeyote ile akitaka kuweka pesa zake kwenye mfumo huu anaweza lakini asitarajia faida yoyote inayotokana na akiba yake iliyo kwenye account za aina hiyo.
Kama DECI ingekuwa inamilikiwa na waislamu..nadhani humu ndani ya JF kungewaka moto.Lakini kwa sababuilikuwa inamilikiwa na kanisa, sijaona criticism ya kiwango hiki.Wabongo kweli ni wabaguzi,yani chuki inatufanya tushindwe hata kuona ukweli???poleni wakorintho na wagalatia maana mnashindwa kuelewa kuwa hata ninyi mnaweza kuwa wateja wa huo mfumo endapo mkitaka.ukitaka kufungua account ya aina hiyo, huulizwi dini yako.hint...mke wangu ana account katika moja ya benki za kanisa,naye ni muislamu.na wakati anafungua hakuulizwa swali linalohusiana na dini yake.....LOL
Sasa kama ni hivi, Shariah Advisory Authority ya Masheikh na Maimamu inakujaje hapa kama lengo ni kuendesha tu benki ? Hapa naamini kuna kitu kimejificha na ndiyo maana wengine twasema ni chombo chenye harufu ya udini na kwa maana hiyo kiendeshwe wazi wazi kama taasisi ya kidini kwa kutumia sheria za kidini, shariah, bila serikali kujihusisha moja kwa moja ? Lazima tukubali kuwa kuna Watanzania ambao hilo neno tu shariah linawakwaza na hawatako tayari kabisa kuhusishwa nalo.
Mkuu kuwepo kwa riba ktk Bank za kikristu hapa nchini haina maana kuna Uhalali.. Hapana mkuu, ukweli ni kwamba Hata Bank ya Vatican waliwahi kujiingiza ktk biashara za Mafia mob huko Italy (money laundry) ikawa noma kichizi kufikia watu walitaka Pope ajiuzuru... Hii haikuwa nam maana Ukristu unaruhusu money laundry.. Hizi ni tamaa za kibiadamu ambazo sote tunajaribu kupambana nazo na wapo watu baina yetu wanaoshindwa kuokoka kiroho hata ndani ya madaraka makubwa, tuwahukumu wao na sio dini..Kwa kweli sijawahi kuwasikia wakristo wakikataza hiyo riba. Na majuzi makanisa ya waluteri na wakatoliki wamefungua benki zao za biashara, nakumbuka ile ya wakatoliki kule Dar nadhani inaitwa Mkombozi au Ukombozi, ilizinduliwa na rais mstaafu mzee Ruksa. Benki ya waluteri iko makao yake makuu Moshi pale Lutheran Centre. Huko kote riba ni kwa kwenda mbele, yaani wanaangalia mafao tu jamaa hawa.
Section 3 hiyo hiyo ikaja ikasema kuwa business of banking nanukuu , "means the business of receiving funds from the general public through the acceptance of deposits payable upon demand or after a fixed period or after notice, or any similar operation through the frequent sale or placement of bonds, certificates, notes or other securities, and to use such funds, in whole or in part, for loans or investments for the account of and at the risk of the person doing such business".
Mkuu wangu unazungumza pasipo kufikiria biashara zote zinafanyika vipi.. Mathalan, wewe unayekwenda kununua Bia yako Bar hivi umewahi kufikiria unaibiwa?..Bia hiyo inatengenezwa na Breweries na wanaiuza kwa Tsh700 lakini ili ikufikie wewe, mwenye bar anainunua na kukuuzia kwa Tsh1,200. Maadam wewe unaikubali bei ya Tsh 1,200 sidhani kama mwenye bar atahukumiwa kwa sababu origin bei ya TBA ni Tsh700. Huwezi kuhukumu mtu pasipo kuchukua kwanza gharama zake na kuijua faida yake.. msichukulie vitu at face value.So how does the Murabaha Mortgage work?; When you find the house that you wish to buy, you arrange a sale price with the vendor as normal, however the bank pays the purchase price, then immediately sells the house to you at a higher price - the higher price is determined by the original price of the property, and the repayment period that you will have agreed with the lender minus the percentage you pay as deposit.
Sasa kama ni hivi, Shariah Advisory Authority ya Masheikh na Maimamu inakujaje hapa kama lengo ni kuendesha tu benki ? Hapa naamini kuna kitu kimejificha na ndiyo maana wengine twasema ni chombo chenye harufu ya udini na kwa maana hiyo kiendeshwe wazi wazi kama taasisi ya kidini kwa kutumia sheria za kidini, shariah, bila serikali kujihusisha moja kwa moja ? Lazima tukubali kuwa kuna Watanzania ambao hilo neno tu shariah linawakwaza na hawatako tayari kabisa kuhusishwa nalo.
By the way, pengine umesoma haraka haraka ujumbe wako pasipo kuelewa kwamba huyo Farzana Hassan ambaye tunaambiwa ni President wa MCC ndiye Chief Executive Officer of the Canada Mortgage and Housing Corporation (CMHC). Sasa inakuwaje huyu President wa MCC chama alichoikanzisha yeye kuandika barua CMHC ambako yeye tena ni Chief Executive kupinga ujio wa Islamic banking system na akizungumzia sekta ambayo yeye ameajiriwa na serikali...
Ndjabu,
Hiyo ni popote unapowekeza mkuu. Ukinunua nyumba kwa mkopo na bahati mbaya ikashuka bei baada ya kununua, bank hawapo responsible na hasara hiyo. Unapowekeza fedha yako au kununua shares ktk orodha yao kama kutatokea kushuka kwa thamani, hasara itakuwa yenu nyote kwani kushuka kwa soko ni hasara kwa pato lako na la Banki waliowekeza. Tofauti ya hizi bank ni wapi fedha yako itatumika ktk uwekezaji..watanunua dhahabu, Oil, electronics n.k na sio Pombe, sigara na Viagra..