Swali langu sikuzote ni hili kabla ya wakoloni kuja hawa waarabu waliokuwa ukanda waote wa Pwani waliwaendeleza waislamu wa nchi hii na kuwatengenezea fursa kiasi gani? Je waliingia Pwani ya Tanganyika lini na walikaa muda gani? Ukweli ni kuwa hawakuwa na lengo au nia ya kutuendeleza. Na je ndugu zetu waliopelekwa huko kwao wakasilimu na kuwatumikia trace zao ziko wapi? Mbona Amerka kuna weusi waliopelekwa huko? <br />
<br />
Sasa kama hao waarabu waliokuja na dini ya kiislamu walikaa muda mrefu kuliko hata wakoloni na wakawazalisha tu waafrika bila kuwaletea mashule, wasijenge hospitali, wasipeleke waafrika Uarabuni ili wasome. Leo Wamisionari wanalaumiwa kwa kuwa wao walifanya yaliyoleta maendleo kwa wafuasi wao? Je waislamu wangekuwa wametendewa haki na wangeridhika kama na wamissionari wakikirsito wasingefanya lolote la kuedeleza wakristo? Je kutoendelea kwa wote ndiyo furaha ya waislamu. Nani aliwazuia masheikh wa kiarabu waliowahi kuja hapa nchini kuleta maendeleo kwa weneyeji? Na sultan je si alitawala nani alimzuia kuendelza watu wake badala ya kuwanyonya tu! Na leo je nani anayewazuia waislmu kufanya maendeleo?