Ishu ya Njombe na kichaa cha kuolewa

Ishu ya Njombe na kichaa cha kuolewa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,917
Reaction score
868,470
Pengine hii habari itarushwa na vituo vyetu vya habari usiku wa leo au pengine haitarushwa lakini iko hivi....
Binti mmoja mwenye mtoto huko Njombe alipata mwanaume wa kumuoa lakini sharti la huyo mume mtarajiwa likawa moja! Hataki huyo mtoto, hivyo binti afanye awezavyo asiingie kwenye ndoa na huyo mtoto wake wa kuzaa mwenyewe kwa baba mwingine
Binti akaona isiwe soo , baada ya kutafakari na kujishauri sana akaona hakuna njia nyingine bora zaidi ya kumnyonga mwanae mpaka afe ili yeye apate kuolewa na la azizi kinyuli
Ishu imebumbuluka na shauri liko mbele ya pilato, kakosa mwana na mmea!
La kujiuliza.. ! Hivi Ndoa zimekuwa za thamani kiasi hiki? Mbona waliomo wanatamani kutoka? Dunia inaelekea wapi?[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Mshana Jr, hapa ataweza kutusaidia, matukio mengine yanatokea siyo kwa sababu za kawaida, ila zinakuwa na namna.

Habari haijasema mtoto alikuwa na umri gani, kama ni miezi michache tu tokea azaliwe, hapo kuna kitu kinaitwa 'Kichaa cha mimba', kitahusika. Maana husababishwa na mengi, kama vile kubakwa na kupata huo ujauzito uliosababisha mtoto, ama aliyempa mimba alimkana kama siyo kumkataa. Wataalamu wa afya hapa na wale wa sheria wanaweza kulifafanua hili vema.

Ila inawezekana pia nguvu za giza zikahusika endapo mtoto alikuwa mkubwa kiasi, mfano nadhani mlishawahi kusikia mtu anarogwa na bila kujijua anajitupa tu barabarani na kugongwa na gari ama anajinyonga tu bila sababu yoyote ile ya msingi. Na ndiyo maana hapo juu nimesema, mleta maada hii ambaye pia ni mdadavuaji kama siyo mtaalamu wa mambo haya ndugu Mshana Jr, anaweza kutusaidia hili.

Akipata mtetezi (wakili) mzuri, na kama mtoto alikuwa ni mchanga sana, unaweza shangaa akaachiwa huru.

Siyo ya kuwa namtetea, HAPANA, ila tusiwe wepesi wa kulaumu bila kuuliza ama kuchambua vyanzo vya MIKASA Maishani.

Naruhusu Kukosolewa ama kusahihishwa.

Ahsante!
 
Great thinker nimeupenda uchambuzi wako ngoja tusubiri taarifa za habari usiku huu then tutarejea hapa
 
Kweli kuna wanawake wana roho ya kikatili yani kuua mtoto alomzaa mwenyewe kisa ndoa,hakika malipo duniani atapata kulingana na alichofanya.
 
Ndoa ndoa ndoa kunani huko mpk mtu anaamua kuua mtoto wake mwenyewe aliyekaa kwenye tumbo lake kwa miezi 9
Naamini hakuna mtu kama mama lakini kwa mama huyu mmmm! HAPANA
 
Yani kaona ndoa ina thamani kuliko kiumbe chake
 
Ewe mwanaume ogopa mwanamke anayeweza kumuua mtoto wake, siku ukimzingua hatajiuliza mara mbili kukulisha sumu ya panya.
 
Back
Top Bottom