Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 5,808
- 13,422
Wazigua wenzangu kutoka Tanga wanasema "live only one day at a time"
Hivi unajua kwanini huwa tunapata sana stress au msongo wa mawazo? Kwasababu hatuishi katika siku moja kikamilifu,bali tunaishi jana,leo na kesho kwa wakati mmoja,,je amani utaitoa wapi? Furaha utaitoa wapi?
Yaani unaishi leo lakini unajilaumu kwa jambo lililo tokea jana? Leo hii unasema "laiti ningejua nisingemtamkia mpendwa wangu kauli ile" au "lau ningeifanya kazi yangu vizur naamini nisingesemwa na boss?"
Na hapo ndipo shida inapoanzia,,hakikisha kama ni majuto basi malizana nayo siku hiyo hiyo ,kama ni upuuzi uliufanya basi malizana nao siku hiyo hiyo ili siku inayofuata uanze na mambo mapya na uishi one day at a time na si unaishi leo huku jana yako inakusumbua
Kibaya zaidi wengine wanaishi jana,leo na kesho kwa siku moja! Yaan ana stress za jana,leo kuna mambo yanamsumbua na bado kama haitoshi analeta stress za kesho ambayo haijafika,,hivi mpo serious na afya zenu?
Kama kuna swali wallah silipendi na wala silitaki kulisikia ni "unajiona wapi baada ya miaka mitano ijayo?"
Haya ni maswali ambayo huwa yanatufanya kujipa stress za miaka mitano ijayo ambayo hatujui hata kama tutakuwa hai? Guys lets live today na kesho itajiseti yenyewe
Maisha ndiyo haya haya
Ni hayo tu!