Ishara za kukujulisha kuwa hujipendi

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,164
15,839
Wewe ni wawili hauko peke yako,kuna wewe ambae unafanya jambo na kuna wewe ambae unatathmini vipi umefanya jambo lile.

Ukichukua changudoa usiku kesho utajilaumu,wewe unaetathmini unamlaumu wewe uliyefanya jambo.

katika hatua hii sasa wewe unaetathmini ndio unakazi kubwa ya kuhakikisha unajipenda mwenyewe.

KUNA NJIA MBILI AMBAZO NAONA zinaweza kukujulisha kuwa HUJIPENDI.

1. Kujihisi upweke na huzuni pale unapokuwa peke yako kiasi kwamba ukaona unahitaji mtu wa kukuliwaza.

Wewe mupo wawili mnashindwa kuliwazana bila shaka haujipendi.

2. Kujilaumu kwa uliyoyafanya nyuma.unapojilaumu maana yake wewe mtathminiji unamlaumu wewe mfanyaji hii ni ishara kwamba wewe hamuelewani wenyewe hamkubaliani juu ya kilichotokea.jifunze kuwa kukosea kupo,piga hatua usikate tamaa.
 
HAYANA FORMULA HAYA MAISHA MKUU NA HAKUNA ALIEKAMILIKA NDO MANA HUWA TUNAFANYA KITU NA BAADAE KUJUTIA MAAMUZI
 
HAYANA FORMULA HAYA MAISHA MKUU NA HAKUNA ALIEKAMILIKA NDO MANA HUWA TUNAFANYA KITU NA BAADAE KUJUTIA MAAMUZI
Hutakiwi kujutia maamuzi.

Unachotakiwa kufanya ni kukiri umekosea na unasonga mbele sio kuanza kukaa na kujutia,maadamu uko hai unatakiwa ufanye kilichokuwa bora zaidi ya kile.

Kujutia maamuzi ni kujiathiri kwa gubu lako mwenyewe,hii tabia ndio inafanya watu wawe na gubu kukumbushia makosa na kusimulia namna alivyokosewa na mwingine kila wakati.

Songa mbeleeeee kaka
 
Naona unapiga kelele ndogo katikati ya kelele kubwa,,, upo sahihi bado.

Ila kumbuka tu mshauri wa ndani ana tabia ya kuugua mazoea na hatimaye kuwa kinyume na ujumbe wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom