Isaya Mwita kuendelea na majukumu ya umeya Dar. Nywila za Ofisi yake zarejeshwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,762
4,313
1579079805674.png

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema ataendelea kutekeleza majukumu yake ya ofisini kwani halmashauri hiyo imerejesha nywila (password) zilizokuwa zikitumika.

Baada ya ofisi hizo kufungwa na kubadilishwa nywila na kuweka mpya, Mwita alisema halmashauri hiyo imerejesha nywila za zamani hivyo, ataendelea na kazi zake. Akizungumza na gazeti hili jana, Mwita alisema anachoamini kuwa yeye bado ni meya wa jiji hilo na kwamba kuna majukumu ya kuendelea kuyatekeleza.

Mwita alisema kanuni ya 84 (1) ya halmashauri inaelekeza ili kumwondoa madarakani inapaswa kuwepo kura theluthi mbili ya wajumbe wote wa halmashauri na makosa yatakayosababisha kuondolewa yameainishwa kwenye kanuni hiyo kuwa ni rushwa, kutumia madaraka vibaya na kubaka.

Alisema kanuni hizo hazikutimizwa katika kikao cha Januari 9, hivyo ataendelea kutekeleza majukumu ya umeya mpaka muda wake utakapokwisha.

“Nilipewa barua Januari 10 ya kukabidhi ofisi na Mkurugenzi wa jiji, nilimjibu kuwa mimi ni meya halali kwa sababu akidi haikutimia siku ya kikao na nikamkumbusha kanuni zetu. Kuhusu ofisi tayari wameshabadilisha nywila ya kuingia hivyo naweza kuendelea na majukumu yangu,”alisema Mwita.

Aliongeza kuwa wajumbe wa halmashauri ni kama wabunge ambao wakitaka kumuondoa Rais, Waziri Mkuu au Spika wanatakiwa kupata theluthi ya kura zote hivyo, kilichotokea ni kushindwa kutafsiri kanuni hiyo.

Alisisitiza kuwa wajumbe walikuwa na uwezo mzuri wa kumuondoa kwenye nafasi hiyo endapo watakaporubuni mmoja wa wajumbe ili kukidhi akidi na kwamba siku 45 bado za kufanya hivyo zipo hivyo, wangepata kura 17 za kumtoa na kwamba wajumbe wasipohudhuria vikao mara tatu baraza hilo litavunjwa na kumkosesha nafasi.

“Nimekuwa mwaminifu kwa kuleta maridhiano kwenye halmashauri yetu, sikuwahi kumvunjia mtu heshima wala kumdhalilisha mtu hivyo, haya ninayopitia nashangaa sana kwani nimedhalilishwa,”alifafanua Mwita

Aliongeza kuwa “Kama theluthi ingepatikana nisingeendelea kung’ang’ania kwa sababu ni ujinga tena ingefaa kukamatwa na vyombo vya dola lakini pia ningetakiwa kukata rufaa kwa Waziri husika wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na ingekuwa nafasi yangu ya mwisho lakini sijaondolewa,” Meya huyo alieleza kuwa akiendelea kupiga kelele atamzuia Rais kufanya kazi kwani anampenda na ni rafiki yake kwani ndiye aliyemfanya awepo hapo mpaka sasa.

Kwa upande wa wakili wake, Hekima Mwasipu alisema Mwita akiondolewa madarakani kisheria hawezi kunufaika na mafao yake kwa sababu atakuwa amepoteza sifa kwa mujibu wa taratibu.

“Endapo watamzuia kupata mafao yake, sisi tutafungua kesi nyingine mahakamani ili aweze kupata haki zake hata kama sio mwaka huu atazipata mwakani kwani bado ana sifa,” alisema.


Habari Leo
 
Mmmh kirahisi tu hivyo wameamua kumrudishia ili hali walidhamiria kumuondoa na gari kanyang'anywa hii huruma imetoka wapi? Na kwanini walifanya vile?
 
Mmmh kirahisi tu hivyo wameamua kumrudishia ili hali walidhamiria kumuondoa na gari kanyang'anywa hii huruma imetoka wapi? Na kwanini walifanya vile?
kuna kitu najiuliza sipati majibu kabisa, adui akikuletea keki ichunguze vizuri kwanza usiibugie
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom