ZITTO VS MAFUTA ZANZIBAR:
Mimi ni declare interest, ni mzanzibar halisi lakini nimekuwa nikimfuatilia kupitia bunge na mijadala minigine zitto kabwe, kwa hakika ni mbunge ambaye anajua anachokizungumza na pia anajua kujenga hoja, hilo kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kulikataa iwe unapenda au hulipendi analoliongea.
Kuhusu suala la mafuta na gesi ya zanzibar kuwa ya muungano, hapo yupo sahihi kabisa. Unajua wenzetu wa tanzania bara (tanganyika) wamekuwa WAKIYAFUMBIA MACHO NA KUTIA PAMBA MASIKIONI kuhusu kilio cha muda mrefu cha kero wanazokumbana nazo wazanzibar kutokana na muungano. Kwa ufupi wazanzibar wengi hawaupendi muungano si kwa sababu ya dini au chuki dhidi ya ndugu zetu wa tanganyika, ispokuwa kutokana na serikali kutosikiliza kilio chao wameamua kutafuta njia ambayo dunia itasikiliza kilio chao. Sio kwamba naunga mkono vurugu la hasha ispokuwa wazanzibar wamefikia pahala wamesema sasa liwalo na liwe.
Hivyo basi kauli ya zitto ilikuwa sahihi kusema ukweli kuhusu zanzibar, kama kuna watu wanadhani kwa kutumia MABAVU kutasaidia kuzima kilio cha wazanzibar basi wajue wamekosea, cha msingi ni kutenda haki kwa pande mbili ili kila upande uweze kuishi kwa heshima na kuaminiana. Leo hii watanganyika waliopo zanzibar wanaishi kwa hofu, na pia wazanzibar waliopo bara wanaishi kwa hofu vile vile kutokana na serikali kutoa majibu mepesi kwa masuala mazito.
Watu wanaona kutumia nguvu ndio suluhisho, hapana kwa sababu unaweza kuwanyamazisha leo, kesho kwenye kura ya MAONI wanaweza wakapiga kura wakaikataa kwa hiyo tatizo liko pale pale LITACHELEWESHA KUPATIKANA KWA KATIBA MPYA jambo ambalo litakuwa ni kosa kubwa kwa demokrasia hasa katika uchaguzi mkuu ujao.
KAKA ZITTO UMETAHADHARISHA KWA HIYO ATAKAEKUBEZA ACHANA NAE HAPO ATHARI ZITAKAPOTOKEA WATAKUJA KUKUKUMBUKA.