Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Sijui maana ya neno Aristocracy kwa Kiswahili, lakini kama nitalielezea nitasema linamaanisha utawala wa kurithishana. Akitoka baba anatawala mtoto na kuendelea.
Nimeangalia dunia nzima kwa ukaribu nimeona masuala ya familia zilizoko kwenye uongozi kubaki kwenye uongozi ni kubwa sana, achana na utawala wa malkia.
Kwa nchi za kiafrika ndio shida kubwa zaidi kwa jina la hicho kinachoitwa democracy, watoto wa masikini au wasio na connection na damu ya kiutawala, ni aghalabu sana kuingia katika nafasi za juu za kiutawala au kiuongozi. Wengi wao huanza kama wanaharakati, wakapigana na polisi ndipo hujipatia umaarufu wao kisiasa na kuja kwenye game, mifano mnayo.
Je democracy iko wapi kama aristocracy inaendelea kushika hatamu ya siasa nyingi za dunia yetu.
Kwa nchi za kiafrika utaona kama mtoto asipokuwa rais basi ukuu wa wilaya, ubunge nk utamuhusu. Na hata sasa tunazijua baadhi ya familia ambazo zina misingi mizuri kiutawala na kiuongozi.
Are we democratic or aristocratic?
Kwa wenzetu Kenya iko wazi…Kenyatta, then Kenyata. Kule Kongo alikuwa Kabila baadae akaja Kabila. Hapa bongo mnawajua kina nanii.
#Ends