Iringa ni pazuri kuliko Dodoma

Ila Dodoma mmh pagumu sana, muda nilioishi pale niliona shida sana yaan ilifikia kipindi ukifika Dar unahisi tofauti ya ngozi
 
Dodoma hii hii au, Dom city patamu kwa kweli labda kama mtu ulikuja miaka ya nyuma ila sasa hivi ku compare na Iringi sio haki labda kwenye usafi iringi iko vizuri
 
Kwanza kabisa tutambue kwamba uzuri wa sehemu kwa binadamu yoyote yule huangalia vyanzo vya mapato binafsi na shughuli gani zitamwingizia kipato. Kiuchumi na ukitaka kutoka kimeisha kwa malengo ya muda mfupi na mrefu basi nenda Iringa ila kama kuzurula na kuangalia majengo ya serikali nenda dodoma. Dodoma inabebwa na UDOM na vyuo vingine na ukitaka kulijua hilo nenda mwezi wa 8 utapachukia siku moja tu
 
Kuna Watu wapo rigged sana. Yaani Dodoma ulinganishe na Iringa.

Kuna residential area Iringa unayoweza kulinganisha na Kisasa au Uzunguni Dodoma?
Kuna hotel gani Iringa unayoweza kulinganisha kihadhi na Morena, Rafiki hotel?
Je, airport ya Iringa unaweza kulinganisha na ya Dodoma?
Stand kuuu ya mabasi Iringa unaweza kulinganisha na ya Dodoma?
Maeneo ya starehe yanaweza kulinganisha na ya Dodoma?
Urefu wa barabara zilizotiwa lami unaweza kulinganisha na Iringa.
Kuna taa za barabarani maeneo ya Kisasa, Ilazo, nk

Uwezo wa kufifika wa Dodoma. Dodoma kuna mabasi yanayoanzia safari zake kuelekea Dar, Arusha, Mbeya, Tunduma,
Mwanza, Kigoma, Bukoba, Songea. Hii ina maana idadi ya abiria ni kubwa sana hence uchumi unaoletwa na biashara ya usafiri ni mkubwa sana.

Ni kweli Iringa ni mji mzuri lakini bado mdogo sana.
Achana nao hao mimi nipo iringa hakuna kitu kuna mtu anaifananusha moshi mjini na iringa mjini huwezi kbsa kbsa kuifanya iringa mjini kuwa kama moshi
 
Back
Top Bottom