Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,606
Nyama ya nguruwe aka Kitimoto inauzika na kuliwa Iringa mjini sijawahi kuona. Karibu na ofisi ya CCM Mkoa kuna mabanda mengi sana zaidi ya 100 yanauza na kukaanga nyama ya kitimoto kila siku kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manane, na nyama inaisha aisee.
Unakuta bar moja imezungukwa na majiko mpaka 8 ya kitimoto, unakula lager, unatafuna mdudu kiroho safi kabisa , ukitaka na ugali au ndizi ni wewe tu.
Moshi, Arusha hawawafikii waHehe kwa kutafuna kitimoto aisee, siyo mbwa tena kama zamani.
Wanaikaanga vyema sana, makachumbari kama yote.
Na hali ya hewa ya Iringa ni kama imechujwa hivyo bia zinatembea tu.
Heko Iringa, watoto wa Mkwawa.