HAhahahaaaa, kweli ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu asante sana mkuu hapo kwenye Red!Bavicha wameishiwa hoja sasa hivi ni mwendo wa uchochezi tu ndicho ninachoona!
Nadhani badala ya ukiwa unashabikia upande mmoja kwenye mambo ya UTAIFA kuwa neutral itasaidia watanzania wote kupata HAKI zetu za msingi.
Issue jana basi la Nganga Limekamatwa na sababu waliokuwa ndani ya basi wamezielezea,jioni vijana 100 wa CDM wakiwa kwenye mikutano yao ya ndani walipigwa na kukamatwa kupelekwa polisi.Ni issue tu ya kuuliza ili upate full information.
Ni kweli na wala si uwongo kwamba Polisi wetu wanatumia nafasi zao vibaya,watu hawa wamepewa mafunzo kwa pesa nyingi za mlipa kodi ili waweze kuepuka haya wanayoyafanya.Polisi wanatakiwa kufanya kazi kiitaluma na si kwa kutumiwa na chama chochote cha siasa.
Wiki lilokwisha polisi wanatuhumiwa kuua mtu kwa kipigo,hivi hizi damu za watanzania hazina thamani kwa kiasi hicho??
Waheshimu RAIA ili na wao waheshimiwe,Bila raia polisi hawawezi kufanya kazi zao kwa usalama.
Mwangosi yalikuwa haya haya.Tanzania yetu sote,tusibaguane kwa misingi ya ITIKADI,baada ya UCHAGUZI kuna maisha,lakini naona baada ya UCHAGUZI kuna watu wanatulisha sumu ya kuchukiana,jamani Tanzania yetu sote,na Mungu hakutuweka huku kwa bahati mbaya,tuvumiliane,tutofautiane kwa hoja,na pale taasisi yoyote inapovuka mipaka yake tuikemee pamoja.Umoja wetu ndiyo nguvu yetu.