Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari, Tagamenda wilayani hapa, Kasesela alisema amechukua uamuzi huo kutokana na baadhi ya familia kuchukulia vitendo hivyo kuwa ni vya kawaida.
Alisema hadi sasa ameshawachukulia hatua za kisheria wanaume watatu na kuwataka wanawake wanaopatwa na masaibu hayo kutoa taarifa kwake ili achukue hatua badala ya kuona kuwa vitendo hivyo ni sehemu ya maisha yao.
Hata hivyo, hakutaja majina ya wanaume hao aliowashughulikia kwa kupiga wake zao.
"Ninatangaza vita na wanaume wote wanaopiga wake zao. Mimi sitaki kubeba dhambi zenu, yeyote anayemtwanga mke wake nitapambana naye", alisema Kasesela.
Alisema hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana katika familia endapo mama na baba wanaingia katika ugomvi na hata kuumizana.
Hatua ya Kasesela kuwataka wanawake kutoa taarifa ilipokewa kwa furaha na wanawake waliohudhuria mkutano huo ambao walisema itasaidia kurejesha amani katika nyumba zao.
Chanzo: Mwananchi