IRINGA: DC Kasesela aahidi kupambana na wanaume wanaopiga wake zao

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
20,033
Points
2,000

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
20,033 2,000
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amepiga marufuku vitendo vya wanaume walio kwenye ndoa kupiga wake zao, akisema atakayebainika hatua kali zinachukuliwa dhidi yake.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari, Tagamenda wilayani hapa, Kasesela alisema amechukua uamuzi huo kutokana na baadhi ya familia kuchukulia vitendo hivyo kuwa ni vya kawaida.

Alisema hadi sasa ameshawachukulia hatua za kisheria wanaume watatu na kuwataka wanawake wanaopatwa na masaibu hayo kutoa taarifa kwake ili achukue hatua badala ya kuona kuwa vitendo hivyo ni sehemu ya maisha yao.

Hata hivyo, hakutaja majina ya wanaume hao aliowashughulikia kwa kupiga wake zao.

"Ninatangaza vita na wanaume wote wanaopiga wake zao. Mimi sitaki kubeba dhambi zenu, yeyote anayemtwanga mke wake nitapambana naye", alisema Kasesela.

Alisema hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana katika familia endapo mama na baba wanaingia katika ugomvi na hata kuumizana.

Hatua ya Kasesela kuwataka wanawake kutoa taarifa ilipokewa kwa furaha na wanawake waliohudhuria mkutano huo ambao walisema itasaidia kurejesha amani katika nyumba zao.

Chanzo: Mwananchi
 
cocochanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
24,402
Points
2,000

cocochanel

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
24,402 2,000
Usipo niona unanimiss inaelekea unaniwazaga sana.Naona unabadilisha badilisha picha kila kukicha ni ili upendwe au unatafuta bwana kwa speed??????
Eeeeeeeeh
Unajua sikuwazi bali inabidi nikuvute uninukuu jamani.

Kuhusu kubadilisha.. ile ilikuwa ya sikukuu.. sasa ni kupiga kazi likizo imeisha. Na unajua kama ni kusaka unaosema basi ningeshawavuta tangu zamani ila sio zangu.. naomba usiniwazie hivyo tena.. labda kama unafikiria nakuvutia wewe.. eeeeeh joke
 
chuma cha mjerumani

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2013
Messages
7,460
Points
2,000

chuma cha mjerumani

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2013
7,460 2,000
Eeeeeeeeh
Unajua sikuwazi bali inabidi nikuvute uninukuu jamani.

Kuhusu kubadilisha.. ile ilikuwa ya sikukuu.. sasa ni kupiga kazi likizo imeisha. Na unajua kama ni kusaka unaosema basi ningeshawavuta tangu zamani ila sio zangu.. naomba usiniwazie hivyo tena.. labda kama unafikiria nakuvutia wewe.. eeeeeh joke

Naona unanivutia kwa picha moto moto SIDANGANYIKI.
 
josephat manyenye

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2017
Messages
539
Points
1,000

josephat manyenye

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2017
539 1,000
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amepiga marufuku vitendo vya wanaume walio kwenye ndoa kupiga wake zao, akisema atakayebainika hatua kali zinachukuliwa dhidi yake.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari, Tagamenda wilayani hapa, Kasesela alisema amechukua uamuzi huo kutokana na baadhi ya familia kuchukulia vitendo hivyo kuwa ni vya kawaida.

Alisema hadi sasa ameshawachukulia hatua za kisheria wanaume watatu na kuwataka wanawake wanaopatwa na masaibu hayo kutoa taarifa kwake ili achukue hatua badala ya kuona kuwa vitendo hivyo ni sehemu ya maisha yao.

Hata hivyo, hakutaja majina ya wanaume hao aliowashughulikia kwa kupiga wake zao.

"Ninatangaza vita na wanaume wote wanaopiga wake zao. Mimi sitaki kubeba dhambi zenu, yeyote anayemtwanga mke wake nitapambana naye", alisema Kasesela.

Alisema hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana katika familia endapo mama na baba wanaingia katika ugomvi na hata kuumizana.

Hatua ya Kasesela kuwataka wanawake kutoa taarifa ilipokewa kwa furaha na wanawake waliohudhuria mkutano huo ambao walisema itasaidia kurejesha amani katika nyumba zao.

Chanzo: Mwananchi
Yaani kati ya mambo yote anayopaswa kumwakilisha rais wetu hilo ndiyo ameona la msingi sana?
 
Forum statistics

Threads 1,391,507
Members 528,420
Posts 34,083,117
Top