Iringa: Basi la New Force la Mbeya - Dar, lapata ajali mlima Kitonga

Mmmhhh mbona kama "KITONGA YA DAR"? Maana ile kitonga yenyewe ya Iringa sio mchezo hata gari lingeonekana kwenye picha kama BAJAJI lakini naona umepiga picha zero distance.
Hapo kitonga mkuu kuna bahadhi ya sehemu hakuna bonde kubwa
 
Mhmm New Force Bues yamezidi kwa ajali sasa.
Mungu wajalie majeruhi wapone haraka sana na wape moyo wa matumaini na utulivu AMINAAAAA
 
Duuh aisee
 
jamani haya mabasi ya new force yana tatizo gani ?

ajali kila siku ?

mhhhhh
 
New Force kuna kitu sio bure maana si kwaajali hizi.
 
Kitonga ya kuanza kupanda na kuna kutinga ya karikati ndiyo yenye korongo la nguvu kama hili basi lingetumbukia hapo ni minofu tu ndio ingetolewa.
 
Mmmh Mungu awasaidie watoke salama, afu pia Kitonga ni kama madereva washapazoea hivi yaani hawaogopi kiivo hyo speed yake dah wakati ukiangalia hivi pembeni hayo makorongo yake si mchezo aisee, hasa ukiwa unashuka yan from Iringa.
 
Hii kampuni kwanini isifungiwe japo mwezi wakati wanachunguzwa?
 
Hakuna cha wachina wala nini, abiria ndiyo wanaendekeza hizi ajali kwa kuacha dereva afanye analotaka mpaka inafikia ajali Udreva wa enzi ya Facebook una Matatizo sana ukikimbiza na kuendesha kwa Fujo ndiyo unaonekana unajua kuendesha
 
Mapendekezo yangu ni hata
1) watanzania susieni haya mabasi ya kampuni ya New Force !!! Haiwezekani kila Sikh ni haohao wanasababisha ajali kunatatizo ndani ya hii kampunu
2) serikali isimamishe Kwa muda hii kampuni ifanye uchunguzi WA kitaalamu kwann hii kampuni inakua na ajali nyingi!??
 
Kama kawaida yao new force!
Ni mwendo wa ajali tu.
 
wachina hawana shida yoyote tayari inasemekena alikwepa gari dogo, ni kukosa umakini tu. madereva wanashuka pale utadhani yeye ni muweza wa yote hakuna kinachoweza kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…