Iringa: Basi la New Force la Mbeya - Dar, lapata ajali mlima Kitonga

Baringongo

Member
Dec 12, 2016
94
85
Kitonga Leo. Hawa wachina watatumaliza!

=====

Basi la kampuni ya New Force lililokuwa linatoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam limetumbukia katika mteremko wa Mlima Kitonga mkoani Iringa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ajali imetokea na RTO (mkuu wa usalama barabarani wa mkoa) anakwenda eneo la tukio. Lakini taarifa za awali kuna majeruhi tu.”

IMG-20181016-WA0008.jpg

Habari zaidi...

Watu kadhaa wamenusurika kifo katika Mlima Kitonga Mkoani Iringa baada ya basi la kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam kugongana na gari nyingine linalodaiwa kuwa ni la Kampuni ya Golden deer lilokuwa likitokea Dar kwenda Tunduma na kisha kuanguka chini ya mlima huo wenye mteremko mkali.

Kaimu Kamanda Polisi wa mkoa wa Iringa, Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa za awali zinasema kuna majeruhi tu.
1.jpg
 
Tupe Updates mkuu!
Chanzo cha ajari,Majeruhi wangapi na waliopoteza maisha wangapi?
 
Majuzi yenyewe mawili yaligongana ruaha mbuyuni leo kitonga hii kampuni hii haifai kwa kweli..Mungu awajalie abiria wasiwe wamepotexa maisha
 
Back
Top Bottom