Iringa: Basi la New Force la Mbeya - Dar, lapata ajali mlima Kitonga

Iringa: Basi la New Force la Mbeya - Dar, lapata ajali mlima Kitonga

Nimehairisha safar leo ili nisafir kesho from mbeya uyole to dar ningedaka bus lolote (probability ya kulidaka new force ilikua n 80%)
sasa nahairisha ad huu mwez ukatike
SIFI LEO
Ajali popote mkuu, acha uoga
 
Pole sana ndugu , jamaa na marafiki pole jwa ajali mbaya mtapata nafuu, msijali.
 
Hayo mabasi siwezi kupanda tena, nilipanda siku moja ilikuwa roho mkononi, yanakimbia sana
 
Siwezi sema ulaya, marekani na china au japan ajali hazitokei ila ni kidogo.
Nadhani Afrika tuna akili ndogo, tuna mabasi mabovu na barabara mbovu yani lazima mabaya yatokee tuu.
Wenzetu wako mbele kifikra, kiteknolojia na kimiundombinu.
Barabara iliyopita eneo la hatari kama kitonga halafu anaeliendesha ni duanzi na gari lenyewe ni mchelemchele unategemea nini?
Kuna haja ya kununua magari imara na hii inaenda moja kwa moja kwa vifaa vingine vinavyoingia nchini.
 
Haya magari nilikuwa napenda sana kusafiri nayo lakini naona mwisho wa kuyapanda ushafika
 
Watu kadhaa wamenusurika kifo katika Mlima Kitonga Mkoani Iringa baada ya basi la kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam kugongana na gari nyingine linalodaiwa kuwa ni la Kampuni ya Golden deer lilokuwa likitokea Dar kwenda Tunduma na kisha kuanguka chini ya mlima huo wenye mteremko mkali.

Kaimu Kamanda Polisi wa mkoa wa Iringa, Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa za awali zinasema kuna majeruhi tu.
Abiria kadhaa wanusurika kifo??????????
 
Ukiona kila siku magari ya kampuni moja yanapata ajali kila siku kaa nayo mbali sana.
Waswahili wanasema mwenye macho haambiwi tazama.
 
Yes nimepazoea nkiwa na gari ndogo tena hasa manual ah unapita fasta tu chap,
Nyang'oro naona ndio danger zaidi kuliko kitonga
Usicheze na kitonga mkuu kuna mteremko mkali sana ndo maana kila ukipita uwezi kosa kuta ajali
 
haya magari ya New force asilimia kubwa wanapanda wafanyabiashara hasa wanaotoka zambia na tunduma wanaenda Dar, wameyazoea sana. na wanafurahia sana speed ya dreva. likisismama kidogo km wamepanda abiria wa njiani wakati wa kushuka watampigia kelele ashuke haraka eti anawachelewesha. na kuacha abiria sehemu za kula ni kawaida kwao, tena hao abiria wengine wanamforce dreva twende bwana atapanda la nyuma. niliwahi panda mara moja nilijuta! mmesimama dkk mbili lishapiga honi linaondoka. nimezoea magari yenye wahudumu hili halina, ni ubabe tu kwa kwenda mbele. mnasafiri kijeshijeshi.
 
Watu kadhaa wamenusurika kifo katika Mlima Kitonga Mkoani Iringa baada ya basi la kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam kugongana na gari nyingine linalodaiwa kuwa ni la Kampuni ya Golden deer lilokuwa likitokea Dar kwenda Tunduma na kisha kuanguka chini ya mlima huo wenye mteremko mkali.



Kaimu Kamanda Polisi wa mkoa wa Iringa, Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa za awali zinasema kuna majeruhi tu

Source: BREAKING: Basi la New Force latambukia Mlima Kitonga | MPEKUZI
 
Jana nilikuwa natokea Mbeya na Basi la DAR LUX tuliondoka Stendi ya 88 na kuliacha NEW FORCE Stendi... Tulipofika eneo la Inyala au Maarufu kama PIPELINE lilitupita kama tumesimama... Kufika Kitonga tulikuta Nimepata ajali li-saa limoja kabla... Kwakweli abiria walisusie hilo basi.
 
Usicheze na kitonga mkuu kuna mteremko mkali sana ndo maana kila ukipita uwezi kosa kuta ajali
ila kumbuka kitonga magari yanayopita hapo ni mengi kwa siku ukilinganisha na nyang'olo
 
Roho mbaya usikute hata mokoteni huna
hapa Kama kuna binadamu mnafiki Wewe unaongoza yani mabasi yanayopata ajali kila kukicha unayatetea hebu hesabu katika kipindi cha miezi sita new force ngapi zimeanguka!???watu wangapi wamekufa na kuumia!???mbona city boy ilifungiwa!???tungekua tuko makini tuneyasimamisha hatamabasi tujue chanzo ni ninii???

Inawezekana madereva hawana uwezo!!!
Inawezekana magari mabovu!!!!
Kwanini ni wao tuuu!!!!!anyway endeleeni kuwatetea ila wanawamaliza Kwa ujinga wenu
 
Back
Top Bottom