Mkuu Tumain heshima mbele.
Kabla ya kuomba vita itokee inakupasa kwanza kujua historia ya vita baina ya Israel na waarabu.Hapa jamvini linapokuja suala la misimamo kuhusiana na mambo ya waarabu au dini Tumain unajulikana uko upande gani.Bila shaka vita ikitokea baina ya Israel na Iran utapenda Iran ishinde vita kitu ambacho hakiwezekani.
Bwana Tumaini usiombe vita itokee kwasababu utabaki na majozi moyoni,ngoja nikupatie historia fupi ya vita baina ya Israel na waarabu muzee.
[1] Six day war ilianza mwaka 1967[vita ya siku sita].Nchi tisa za kiarabu [Syria,Misri,Jordan,Iraq,Saudi Arabia,Sudan,Morroco,Tunisia na Algeria] kwa pamoja ziliishambulia Israel lakini mwisho wa vita vilivyochukua siku sita Israel iliibuka mshindi.
[2]Yom Kippur war ilianza mwaka 1973,Misri na Syria ziliishambulia Israel na baadaye nchi za Saudi Arabia,Kuweit na Libya zikajumuika kuishambulia Israel.Kwa mara nyingine tena mwisho wa vita Israel ilibuka mshinda tena ikateka maeneo muhimu kama Golan Heights mpaka leo Syria wamebaki wanalilia kurejeshewa eneo hilo muhimu katika medani ya vita.
Mkuu Tumain nimekumegea mifano miwili tu ambayo imeonyesha wazi jinsi Israel ilivyoweza mara zote kuzishinda nchi za kiarabu tena zilizoungana dhidi yake sasa kama una akili nzuri nchi ya Iran pekee yake ikijaribu kutia pua Israel bila shaka matokeo utakuwa umeshayajua kabla vita unayomba itokee.
Israel si taifa lelemama laiti lingekuwa taifa legelege mbele ya mataifa ya kiarabu yenye utajiri mkubwa wa mafuta lingeshafutwa siku nyingi katika uso wa dunia.Jaribu kufungua atlas utaone Israel ni taifa lililozungukwa na waarabu kila upande lakini bado limeweza kujitetea na hii ni sababu tunaona watu wajinga kama Mahmoud Ahmedinejad hawataki kujifunza historia ya mashariki ya kati.