Iran imejichokea kupitiliza

Iran imejichokea kupitiliza

Mtoa mada. Watu wamekusakama sana.Ulijipanga kwa hii vita au ulipitiwa tu ukaamua kuanzisha uzi??
Report ya Jaji Chande ilinichanganya.
Ila Viongozi wa Iran wameuwawa kama Nzige.
Mojtaba nasikia miguu kwishey uso umesambaratishwa kama yuko hai ni bahati sana.
 
Heshima sana wanajamvi.
Si kawaida yangu kuchangia jukwaa hili lakini leo imenibidi nishiriki japo kwa uchache.

Iran ya Ayatollah ya mwaka 1979 hadi mwaka 2025 imeharibiwa vibaya mno.

Iran iliyoweza kumudu kuishi na vikwazo kwa muda mrefu sana kiasi miaka 47 sasa imefikia tamati.

Vita ya Iran na USA & Israel si vita vya kidini kama Watanganyika wengi wanavyofiki including Mohamed Said .

Vita vya Iran na USA & Israel unaweza kuviweka katika sehemu mbili kuu.
USA anaitazama vita hivi kiuchumi zaidi,hasa maslahi yake dhidi ya China inayotaka kuondoa ukuu USA.
Israel ni suala la usalama wake wa kuendelea kuwepo.

Uimara wa Iran kiuchumi,science & technology ni kitisho eneo lote la mashariki ya kati.Makundi mengi ya kigaidi kama Hizibullah & Hamas yalikuwa yakitegemea msaada ya kijeshi na fedha kutokea Tehran.Iran ikitetereka makundi yote ya kigaidi yatajifia taratibu kwakuwa hayatakuwa yakipata tena ufadhili kutokea Tehran.

Iran imara ni kitisho kwa mataifa yote ya middle east ndio maana mataifa yote ya mashariki yakati yakumbana na makombora ya Iran.Sasa hapo ukitia udini ni kijizima data na kuendeleza ushabiki wa kijinga.

Iran ya sasa imesambaratishwa vibaya mno.
Wananchi wa Iran walikuwa na uhaba wa maji kabla ya vita.
Ayatollah aliwekeza zaidi katika masula ya ulinzi na usalama.Badala ya kujenga miundombinu ya maji na umeme wa uhakika ilijikita zaidi kujenga makombora na mitambo ya nyuklia.

Iran inakwenda Islamabad ikiwa haina kadi ya maana labda mlango wa Hormuz ambayo pia USA kashauziba.
Iran ya Ayatollah 1979 imejifia kifo cha Mende.kauli mbiu yake kifo kwa Israel kifo kwa USA imegeuka kichekesho imewarejea wenyewe.

Mashabiki wa Iran ni wakati wa kukubali bila hiyana zama za kutamba na kufadhili makundi ya ugaidi umefika mwisho wa mwisho.
Iran ijayo itakuwa kama Iraq.

Ngongo kawasasa Tehran.
Iran wanajipa moyo tu, kiukweli uma-much know waliokuwa nao toka 1979 mpaka 2025 umepotezwa wote. Ile combination ya myahudi na mmarekani katika kumtwanga imewapotezea sana mwelekeo wa maisha yao. Leo hii ikitangazwa kwamba vita imeisha ndipo watakapoanza kusikilizia maumivu yaliyotokana na vita kwenye maungo yao.
 
Iran wanajipa moyo tu, kiukweli uma-much know waliokuwa nao toka 1979 mpaka 2025 umepotezwa wote. Ile combination ya myahudi na mmarekani katika kumtwanga imewapotezea sana mwelekeo wa maisha yao. Leo hii ikitangazwa kwamba vita imeisha ndipo watakapoanza kusikilizia maumivu yaliyotokana na vita kwenye maungo yao.
Hasara hii waliyopata ni ndogo kuliko ya vita ya Iraq iliyopiganwa miaka nane.
Usisahau Marekani ana balozi zake 5 zimeteketezwa mashariki ya kati,kambi 27 zimeunguzwa,uwekezaji mwingi wa kiuchumi mashariki ya kati wa Marekani umeharibiwa.
Kiufupi White house wenyewe wamedai uwekezaji wa miaka 50 walioufanya mashariki ya kati umeteketea.
Wakati wewe unaropoka Iran imepoteana wenzako wanarudisha hasara kwa kutoza ushuru mfereji wa hormuz na kuzidisha biashara kupitia Caspian sea na corridor za Pakistan. Hivyo upunguze kuropoka.
 
Iran wanajipa moyo tu, kiukweli uma-much know waliokuwa nao toka 1979 mpaka 2025 umepotezwa wote. Ile combination ya myahudi na mmarekani katika kumtwanga imewapotezea sana mwelekeo wa maisha yao. Leo hii ikitangazwa kwamba vita imeisha ndipo watakapoanza kusikilizia maumivu yaliyotokana na vita kwenye maungo yao.
Kwahio tuwape muda gani ili kusadikisha huu utabiri wako ewe yahaya hussein
 
Baada ya kuuwawa zaidi ya viongozi 60 wa Iran leo mgao wa umeme umeanza rasmi.

VIongozi wa Iran waendelee kukaza fuvu huku nchi ikiendelea kuangamia.
 
Mgao wa chakula umeshika kasi.
Maji yameadimika kama almasi.
 
Iran lita ya mafuta sh 61 za Tanzania, Unit moja ya Umeme sh 10 ya Tanzania, unit moja ya maji (lita 1000 aka mapipa 10) sh 8 za Tanzania, vyakula, Nyama, maziwa etc vyote bei rahisi kuliko Tanzania na GDP per capita yao ni mara 4 ya Tanzania. Utaskia MTU anakwambia Iran Wana shida.
Ya kweli haya?
 
Matokeo ya kuwa na one sided informations ndiyo kama haya sasa.

Umeongea kitu ambacho hata haukielewi.

Usichokijua ni kwamba Marekani amepoteza ushawishi hapo Mashariki ya Kati.
 
Back
Top Bottom