Iran: Hatimae rais mpya apatikana

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,539
32,450
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais na Mabaraza ya Miji na Vijiji nchni Iran yanaonyesha kuwa Seyyed Ebrahim Raeisi amepata ushindi wa kishindo katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Jamal Orf, Wairani milioni 28.6 walishiriki katika uchaguzi na hadi sasa baada ya asilimia 90 ya kura kuhesabiwa, Seyyed Raeisi amepata zaidi ya kura milioni 17.8.
Anafuatiwa na Mohsen Rezaei aliyepata kura milioni 3.3, Abdulnasser Hemmati kura milioni 2.4 na Amir Hossein Ghazizadeh Hashemi takribani kura milioni moja.

Orf amesema zoezi la kuhesabu kura linaendelea na pindi litakapokamilika matokeo rasmi yatatangazwa.

Wagombea wote watatu wa urais tayari wameshampongeza Ebrahim Raeisi kwa ushindi wake huo mkubwa katika uchaguzi huo uliofanyika jana Ijumaa.
Uchaguzi huo wa urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulimalizika mapema leo Jumamosi baada ya upigaji kura wa masaa 19 ambapo mamilioni ya wapigakura walijitokeza.

Zoezi la kupiga kura lilimalizika Jumamosi (Juni 19) saa nane usiku, masaa 19 baada ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa saa moja asubuhi Ijumaa, Juni 18.

Muda wa zoezi la kupiga kura uliongezwa mara kadhaa ili kuhudumia idadi kubwa ya wapiga kura na pia kutokana na uzingatiaji wa kanuni za kiafya za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Zaidi ya Wairani milioni 59 walikuwa wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi ambao ulikuwa wa wagombea wanne baada ya Wagombea wengine watatu kujiondoa katika mchuano huo Jumatano.

Jana pia kulifanyika uchaguzi wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji na halikadhalika uchaguzi mdogo wa bunge na baraza la wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.

images (33).jpeg

Seyyed Ebrahim Raeisi rais mtarajiwa
 
Safari hii uchaguzi wa Iran umeenda Kimya Kimya Sana. Ule wa 2012 Kama sikosei ulikuwa wa kelele nyingi Sana. Walimwengu wakasikia kelele za uchaguzi hata waliokuwa hawataki.
 
Iran imejiingiza kwwnye trouble raisi wamechagua aliyewekewa vikwazo na mwenye damu mikononi... Alikuwa judge ambaye record yake hatari kuhukumu watu kunyongwa zaidi ya elfu 30 kudadeki waeza muita Shetan mdogo
 
Iran imejiingiza kwwnye trouble raisi wamechagua aliyewekewa vikwazo na mwenye damu mikononi... Alikuwa judge ambaye record yake hatari kuhukumu watu kunyongwa zaidi ya elfu 30 kudadeki waeza muita Shetan mdogo
Watu kama hao huwa wanaendaga mbinguni
 
Iran imejiingiza kwwnye trouble raisi wamechagua aliyewekewa vikwazo na mwenye damu mikononi... Alikuwa judge ambaye record yake hatari kuhukumu watu kunyongwa zaidi ya elfu 30 kudadeki waeza muita Shetan mdogo
Kama judge alikuwa akitekeleza majukumu yake kikatiba akifuata sheria, sidhan kama katika huku zake alisha wahi kumuonea mtu.
Hao walio muwekea vikwazo wameua na wanaendelea kuua mamilioni ya watu kimya kimya. Hongera Wairani
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom