Iramba tuache unafiki - Tusimfitini Dkt. Mwigulu kwani bado ana nafasi ya kuisaidia Iramba

Lyambalyetu

Member
Apr 6, 2021
27
45
Bahati nzuri Ndugu yangu ni mmojawapo wa madiwani wa viti maalum Iramba. Katika udiwani wake huu ni muhula wa pili na anakiri isingekuwa Dr. Mwigulu asingeshinda mwaka jana kwani upinzani ndani ya Chama ulikuwa mkali sana.

Ndugu yangu anabaisha bayana kuwa Mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi Dr. Mwigulu alikuwa mnyenyekevu sana kutetea nafasi yake ya ubunge kwao hasa baada ya kukosa nafasi ya kuwania URais.

Mara baada ya kufanikiwa kuwa Mbunge akawasahau wananchi kwa kiasi kikubwa mno. Hata wale ambao alisoma nao shule ya msingi kwa kurudia rudia wakaanza kumsema vibaya na hatimaye hadi ikafikia na JPM akampumzisha UWaziri.

Dr Mwigulu alivyopumzishwa UWaziri basi akarudi tena kuwa mnyeneyekevu kwa wananchi huku akipambana vikali kwenye media kujipendekeza kwa JPM na hatimaye JPM akajifikiria na kuamua kumrudisha kwenye UWaziri. Dr. Mwigulu.

Mwaka jana Dr. Mwigulu akajirudi kwa unyenyekevu Mkuu kwa wapiga kura - akawa anawasemehsa KiNyiramba tu kila akipita. Haongei Kiswahili wala nini. Katengeneza chenji chenji za elfu mbili mbili nyingi. Kila akipita vijijini akikusalimia na kaelfu mbili juu.

Anakuangalia hadhi yako - anakuona unafaa kwa elfu 2 au kwa elfu tano au elfu kumi au hata hamsini. Mie mama yangu mwenyewe alimpa elfu 20 - kumsaidia mchango wa kanisani kwa sababu mama ni mwimbaji wa Kwaya kweli kweli. Wachungaji wengi aliwachangia wao wenyewe kwa sadaka kedekede na hata pale madhabahuni walipata misadaka ya category zote. Iwe ni ujenzi au kuchangia vyombo vya muziki au safari za watumishi Dr. Mwigulu sadaka yake ilifika hata yeye pasipo kuwepo.

Mwezi mmoja baada ya Uchaguzi - Dr. Mwigulu hapokei tena simu za wapiga kura wake. Bahati nzuri juzi hata diwani wake ambaye ni Ndugu yangu mimi na walisoma wote kampigia simu Dr. Mwigulu hapokei tena. Kweli sisi wa vijijini sometimes tunasumbua sana lakini sio kivile kwani sio kila simu ni ya kupiga mzinga. Kuna simu zingine ni za kutoa tu taarifa muhimu - mfano kualikwa kwenye kikao cha Chama n.k.

Kwa ujumla Dr. Mwigulu hana cha kujivunua kuhusu Iramba. Kuanzia Wembere mpaka Maluga na kule Urughu au Kisiriri kote huko wananchi wanajituma wenyewe tu. Hamna wanachosaidika na Dr. Mwigulu - anakuja anaanzisha miradi strategic kwa ajili ya kutafuta kura na sio kwa ajili ya kuendeleza Iramba. Dr. Mwigulu amekuwa na kiburi kwa sababu ameiona Iramba kama ni mali yake na kama vile ana hatimiliki. Kwa sasa anaendeleza nyodo ukifika Uchaguzi anarudisha mikono nyuma kuomba kura.

Nimeandika hivi kwa uchungu na bila fitina kwa sababu ninaona wazi wazi wale watu wake wa karibu sasa wanaanza kumfitini - wanamsema vibaya pembeni na badala ya kumsema bayana ili ajirekebishe asaidie Iramba yetu. Dr. Mwigulu ni mchapa kazi lakini aache kuwapa nafasi watu wamfitini kutokana na kubadilika badilika. Anapotafuta uongozi kupitia wao anakuwa mnyonge anapoibuka kidedea anaacha kuwasaidia kwa yale aliyowaahidi. Eti inasemekana wapambe wake wanasema akifanya yote atakuwa hana umuhimu tena.
 

Kimbuge

Senior Member
Dec 28, 2019
106
225
Mleta uzi una jambo lako, na hujaonekana kuwa msemaji wa wanairamba, na kama wewe ndie msemaji wa wanairamba basi amejua udhaifu wenu na anautumia vizuri sana
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,399
2,000
IMleta uzi una jambo lako, na hujaonekanai kuwa msemaji wa wanairamba, na kama wewe ndie msemaji wa wanairamba basi amejua udhaifu wenu na anautumia vizuri sana
Mleta uzi atakuwa Mataga,sijui anaongelea Iramba ipi?
Hata aliyemtuma sijui Kama kichwani chake ni kizima.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom