Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
IRAMBA: MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA TSH. BILIONI 7.8
Mwenge wa Uhuru 2025 Umeendelea na Mbio zake Wilayani Iramba Mkoani Singida ambapo Miradi Saba yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 7.8 imekaguliwa, Kuwekwa Mawe ya Msingi na Kuzinduliwa
Waziri wa Fedha ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amewashukuru sana wananchi wa Iramba kwa mapokezi ya kihistoria ya Mwenge wa Uhuru.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu amesema kuwa ataendelea kusimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kiwango kinachostahili.
"Kazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kubwa, na sisi tupo mstari wa mbele kuhakikisha huduma muhimu kama Maji, Barabara, Afya, Elimu na Umeme zinafika kila kona ya nchi." - Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Yusuph Mwenda aliongoza mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mnamo tarehe 20 Julai, 2025 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mosses Machali ukitokea katika Wilaya ya Mkalama.
Attachments
-
Screenshot 2025-07-22 at 11-34-16 Instagram.png801.4 KB · Views: 20 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-52-38 Instagram.png645.1 KB · Views: 17 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-53-06 Instagram.png219.7 KB · Views: 19 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-53-28 Instagram.png248.4 KB · Views: 16 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-53-36 Instagram.png630.3 KB · Views: 19 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-53-43 Instagram.png551.7 KB · Views: 17 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-54-12 Instagram.png645.1 KB · Views: 21 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-54-25 Instagram.png485.4 KB · Views: 18 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-54-34 Instagram.png241.4 KB · Views: 20 -
Screenshot 2025-07-22 at 11-54-40 Instagram.png671.4 KB · Views: 19