Hakuna habari nisizo zipenda JF kama za migongano ya kidini. Hili ni bomu la akiba la wazungu ambalo wamelitegesha kwetu. Siku wakitaka kutulipua watakachofanya ni kumtengeneza mtu akaenda kilipua ama nyumba ya ibada au rasilimali ya dini yoyote halafu inaundwa mitandao na inatangazwa kwa nguvu sana kua huyo kafanya hivyo kwa kua anaichukia dini husika. Kitakachofuata ni wafuasi wa dini iliyoshambuliwa kulipiza kisasi kwa maneno na vitendo. Mungu atunusuru
Kuja kwa thread hizi, ile ya alexielias kuhusu udini kwenye kampuni ya Bakhresa na hii ya byembalilwa kuhusu udini IPP ni mifano halisi na naona ni mkakati wa kuwamisha watu kutoka kwenye ajenda flani sijui ya tarehe ngapi mwezi wa nne(japo siiungi mkono) waanze kushambuliana wenyewe kwa wenyewe, na kupitia dini mkakati utafanikiwa