Ipo wapi Zanzibar kwenye vyombo vya dola?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Si hoja ya kikatiba Wala ya kisheria ni hoja ya fikra juu ya utekelezaji wa Yale ambayo hayajaandikwa na si kwamba yalisaulika kuandikwa bali ni magumu kuyaweka kwenye makaratasi.

Hakuna sehemu Katiba wala sheria inaposema wakuu wa vyombo wabadilishane kutoka na pande mbili za Muungano. Aidha hakuna sehemu ilipoandikwa Rais akitoka bara Makamu atoke Zanzibar ila tamadumu zimezoea kuweka usawa wa Muungano kwenye teuzi na chaguzi.

Kwa muktadha huo naomba kujua kwanini Wazanzibar ni wachache sana kwenye vyombo vya ulinzi hasa nafasi zinazotokana na uteuzi wa Rais?

Je si wakati muafaka sasa Mama Samia anapokwenda kupangua viongozi wa vyombo vyetu akateua baadhi ya wakuu wa taasisi hizi kutoka Zanzibar?

Jana nilifungua mjadala wa nafasi ya wanawake kwenye majeshi yetu, Leo nafungua mjadala wa nafasi ya Zanzibar kwenye uteuzi wa wakuu wa vyombo. Nafungua mjadala huu baada yakuona top officials wa vyombo vyetu wanatoka bara. Sijui wazenji labda mwamko wao kwenye vyombo ni mdogo au tatizo ni uwezo?

Tuone polisi chini ya Mzenji, Uhamiaji chini ya Mzenji, TISS chini ya Mzenji, JW pia.

Tunapojadili hoja Kama hizi zinatusaidia kujua aina ya mawazo ya kwenda nayo kwenye Katiba mpya endapo tutapata hii fursa. JF iwe moja ya sehemu zakuchukulia hoja za kitafiti kuijenga Tanzania tuitakayo.

WERIKAMU
 
Ndio sawasawa kwani WaZenji hawautaki Muungano hata kuuwona subiri kura ya maoni tu, mambo yapo UN, fyi..Tuna jeshi letu na vyombo kibao vya ulinzi na usalama.
 
... kuna kitu kimoja tu kuuhusu muungano ambacho ni cha lazima; "Rais akitoka upande mmoja wa Muungano, Makamu atoke upande wa pili". Mengine yote kuuhusu Muungano ni discretion ya mwenye maamuzi. Kesho wakiamua Ikulu ya Tanzania iwe Chake Chake nayo poa tu maana Katiba haisemi chochote.
 
Back
Top Bottom