Ipo wapi zamani

Ipo wapi zamani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,659
Reaction score
870,343
_*Zamani Nyumba Zetu Zilikua Vyumba Kidogo na Sehemu ya Kukaa tu, Tunakutana Ndugu, Jamaa na Majirani*_.
_*Lakini Leo Nyumba Zetu Kubwa na Zina Vyumba vingi, isipokuwa Hazina Watu ila Ardhi na Kuta tu*_.

_*Zamani Chakula Chetu ni Wali, Mihogo, Ndizi, Magimbi, Dagaa la Kitonge, au Ugali kwa Chukuchuku*_.
_*Tunatandika Mkeka au Jamvi Chini na Tunakula Sahani Moja Sote, Tunacheka kwa Furaha Mpaka Jirani Wanatusikia.*_

_*Lakini Leo hii Sufuria au Hotpot Imejaa Nyama, Kuku na Minofu ya Samaki na Kila Mmoja na Sahani Yake ya Aina Tofauti*_ .

_*Zamani Tulikuwa Tunakwenda Shule kwa Kupitiana Nyumba Hadi Nyumba*_, _*Mnafika Shule Mnahesabu Namba na Kukimbia Mchaka Mchaka*_
_*Lakini Leo hii Watoto*_ _*wanapitiwa na school Bus Wakifika Shule Hakuna Mchaka Mchaka, Hakuna Kuhesabu Namba..*_

_*Zamani Tunakaa Uwani na Babu, Anatuhadithia Hadithi, Tunakunywa chai kwa upendo na Kucheka kwa Pamoja kwa Tabasamu Mpaka Meno Yetu Yanaonekana.*_

_*Lakini Leo hii Kukaa Kwetu ni Kwenye Simu za Mkononi, Internet na Kuchat tu Kwenye Whatsapp, Wechat, Instagram, Facebook na Mitandao Mengine ya Kijamii, Tumekua Tupo Kwingine Kabisaa.*_

_*Zamani Tunauliziana, Kujuliana Hali, kutembeleana, na Tunakutana kwa Furaha na Kukumbatiana.*_

_*LAKINI Leo Hii ni Sikukuu Mpaka Sikukuu au Harusi had harus au Mpaka Kuwe na Maziko Ndio Tunatembeleana au Kuonana Tena Kwa Kujilazimisha*_

_*Zamani Mtu Akiumwa Kati Yetu, Tunakusanyika Ndugu na Majirani.*_

_*Lakini Leo hii Ndugu Hakujali, hana Muda na Wewe.*_

_*Zamani ilikua Ndugu Anamuenzi Ndugu Yake na Dada Yake, Kwa Kila Alichonacho Hata Kama Kachoka au ana Msongo wa Mawazo.*_

_*Lakini Leo hii Unamkuta Mtu Hapati Kula na Ndugu Yake Yupo Kazama katika Neema, Anajifanya Kakasirika kwa Sababu Zisizoeleweka, na Kukata Mawasiliano kwa Miaka. Hajali Ndugu Wala Jirani, UTU Unapotea Anasahau kama Kuna Kufa au Dunia ina Mwisho*_

_*Mpo Wapi Watu wa Zamani Mje Muone Mioyo ya Watu ilivyobadilika!!*_

_*Miaka na siku Hazirudi NYUMA , TENDA Wema Uende Zako Usingoje Shukrani.*_

_*Hamna tena undugu wa kuwakusanya pamoja kama zamani, hamna mapenzi na upendo ndani ya mioyo, (Hata heshima kwa mkubwa kama zamani hamna).*_

_*Iko wapi zamani? Mola awarehemu wa zamani waliotangulia. Waliojenga upendo undugu ktk jamii, waliondoa udini, tuliishi kwa furahaa na Amani, sikukuu zote tulikuwa tunashirikishana Pamoja*_

*Mwenyezi MUNGU Atujaliye Tuwe Wenye Kupendana na kushikamana kwa Kila Hali kama ilivyokuwa ZAMANI.*

*UMOJA WETU NDIO UNDUGU WETU....!*

Jr[emoji769]
 
Zamani ilikuwa hovyo sana

Leo sipo kwa ajili ya kubishana
 
Umenikumbusha mbali sana, enzi zile mkitoka Shule jioni mnajikusanya kucheza rede, mdako, mnapitiana kwenda Kisimani, bila kusahau mtongozano mzuriiiiiiiiiiii wa kuandikiana barua halafu unaificha chini ya Godoro ukimkumbuka mwenzako unaitoa unaisoma unatabasamu huku mkiwekeana masharti ya kutogegedana hadi ndoa, namiss hizo siku aisee, namkumbuka bibi yangu kila jioni ilikuwa lazima atusimulie hadithi nzuriiiiiiiiiiii za kupendeza na historia za mababu zetu, siku hzi mambo yanaenda kasi sana, sioni uzuri ule wa zamani tena
 
Hata Leo ni Zamani ya Kesho.

Bora Leo kuliko kesho Ambapo hata kwenye misiba ndugu hawatajitokeza kushiriki Msiba, kuna kampuni za kuzika na kuombeleza zinakuja.

Kesho huu Upendo mdogo uliobaki utatoweka, Ndoa zitakuwa za mikataba, wanaume kwa wanaume wataoana hali kadhalika wanawake.

Kesho ndugu wa tumbo moja ataishi Kama mtu baki, hakutakuwa na msemo wa,
"undugu ni kufaana"

Bora Leo kuliko kesho ambapo Leo itakuwa zamani.

Natanguliza Salamu




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wakizamani tulikuwa tunacheza kwa furaha mnoo "ukuti ukuti" "kombolela" "rede" kutengeneza midoli ya udongo,tulikuwa tunajua kutengeneza hadi magari ya box na kurusha tiara,.lakini siku hizi watoto wanacheza michezo ya kwenye computer na tablet tuu,.hawakutani kama zamani na kucheza kwa pamoja mpira wa miguu au wa kikapu au hata "mdako"

Zamani imeenda na zama zake.
 
zamani ilikuwa rahisi kumwambia mwenzio 'ntakufunga au nitakupoteza' lakini sasa hivi ni 'tutagawana majengo ya serikali'
 
''Hapo zaman
Hapo zamani,
Mambo mengi yalikuwa shwari,
Kinyume na sasa
kinyume na sasa
Mambo mengi yamebadilika''(
chorus)- Joseph Mbilinyi
 
Huko tunapoelekea ndo kubaya zaidi. .me namiss tu kukutana familia yotee mnakaa mnapiga story lakn sahv kila mtu anajidai ana majukumu yake[emoji21]

Bora ata wachaga wanakutana december
 
nadhani ndo ile tuliizika kabla ya Kikwee kuingia madarakani
 
Huko tunapoelekea ndo kubaya zaidi. .me namiss tu kukutana familia yotee mnakaa mnapiga story lakn sahv kila mtu anajidai ana majukumu yake[emoji21]

Bora ata wachaga wanakutana december
ni kujidai au majukumu ya kweli Inna?
 
Jamani ata sikukuu kama xmass kuna majukumu gani wakt dunia nzima inajua ni mapumziko
majukumu yapo ya aina nyingi,
moja kuna ile ya watu kuishi mbali mbali....mtu akiwazia cost anashindwa kutoka anakupa kisingizio kingine,

ila wapo ambao bado wanakutana mara kwa mara pamoja na majukumu hayo.
 
Back
Top Bottom