Huu mjadala hauna tija, hatuwezi kuwa sawa, si kila kitu ni kwaajili ya kila mtu, pengine DSTV hawajafungua biashara yao kukulenga wewe, acha kulalamika, mbona Toyota Motors wanauza magari mazuri na mapya haulalamiki kwanini hawaweki magari rahisi ya mitumba japo hauna uwezo wa kununua? Hali kadhalika yapo maduka yanauza mashati na suti nzuri tu kwa bei ghali sana mbona haulalamiki bei yao ishushwe kama mitumba ya ilala ili watanzania wote waweze kuvaa mashati nadhifu na mapya. Acheni mambo ya wivu, ridhika na hali yako ya maisha, hao DSTV hawajafungua biashara yao hapa nchini kwaajili yako, tafuta king'amuzi unachoweza kulipia. EPL kwanza siyo ligi ya kizalendo na kuangalia EPL siyo jambo lenye maslahi ya Taifa