Ipo siku CHADEMA itashika dola

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,247
Hata kama siyo kwa sasa ila ipo siku CHADEMA itashika dola tu hizi facts za kweli, CHADEMA ni chama ambaco kimeonyesha upinzani wa kweli, vyama vingine vinazaliwa, kudhoofika na kufa lakini CHADEMA kipo tu pamoja na fitna zote.

CHADEMA hakijafanya hata mikutano ya ndani acha mikutano ya nje kwa miaka 5 lakini bado kipo na nguvu sana.

Inanyanyaswa na jeshi la polisi, kutekwa, uhuni wa kila aina wenye mkono wa CCM ila bado kipo hata kisiposimamisha mgombea,ni ukweli mchungu CCM haiwezi kutawala milele na mbadala utakuwa chadema watake wasitake.

CHADEMA kipo tu, leo hii ukizungumzia upinzani unazungumzia CHADEMA, sasa mtaikwepa vipi na mtaendelea na uhuni hadi lini?
 
Kweli suala la ofisi inatia aibu sana na wameshauriwa mda mrefu wala hawahangaiki na ofisi ,haya magari yenyewe hamna hata mikutano ya nje ni kwa ajili ya kampeni tu,kwenye ofisi hawapo smart kabisa
Chadema wapo vizuri lakini kuna mambo machache wanachemka, mfano kutokuwa na ofisi ya maana makao makuu na kung'an'gania kununua magari kila siku na kupitia wagombea ubunge baadhi ambao hawakubaliki kwa wananchi.
 
Chadema wapo vizuri lakini kuna mambo machache wanachemka, mfano kutokuwa na ofisi ya maana makao makuu na kung'an'gania kununua magari kila siku na kupitia wagombea ubunge baadhi ambao hawakubaliki kwa wananchi.
Una hoja lakini magari ni muhimu kueneza chama. Ila sasa nguvu ielekezwe kwenye kujenga ofisi!

Wagombea wasiokubalika ni wapi? wataje
 
Mkuu magari sasa hivi hamna hata mikutano ya nje wala ndani ni figisu ,kwani kujenga ofisi inachukua mda gani na gharama gani ,millions zaidi ya 300 inawekezwa kwenye magari wakati ofisi ni aibu
Una hoja lkn magari ni muhimu kueneza chama. Ila sasa nguvu ielekezwe kwenye kujenga ofisi!..
Wagombea wasiokubalika ni wapi? wataje
 
Mkuu kuhusu vitega uchumi si kwa awamu hii,lazima serikali iwafungie vitega uchumi kama uhuni aliokuwa anafanyiwa mbowe
Kwa kuongezea waweke vitega uchumi sio kutegemea ruzuku pekee
 
Mutation itokee kwanza si cdm hii ya viongozi hawa Lissu na Mbowe na waaina yao. Mnyika anaburuzwa tu mwili, nafsi na akili yake havitaki.
 
Mkuu bila shaka unajua chadema kinachopitia ,taarifa zao hata kwenye tv hizi hazitakiwi juzi tu Sahara media wamepigwa faini kubwa kisa mahojiano ya lissu ,

Yaani hizo tv na redio lazima zitafungwa tu ndo tatizo lilipo
Waanzishe TV na radio yao,-..itasaidia kusambaza awareness na propaganda.
Ccm wanatumia dola na serikali kuminya uhuru was vyombo vya habari.
 
Hata kama siyo kwa sasa ila ipo siku CHADEMA itashika dola tu hizi facts za kweli,CHADEMA ni chama ambayo imeonyesha upinzani wa kweli,vyama vingine vinazaliwa, kudhoofika na kufa lakini CHADEMA kipo tu pamoja na fitna zote....
Dola ya pesa au, hiyo mbona mnaishika kila siku
 
Ogopa sana mtu mwenye njaa. Njaa tuliyonayo sasa, kikiwaka tu makaburi yatafukuliwa na kupigwa mabomu. Nakuambia wengine hamuamini mpaka muone.
 
Hakuna Sikh CHADEMA dola. Labda wabadikishwe Mwenyekiti was Chama. Nchi hii Ione hivi hivi tu, wanajua siku dola ikikamatwa na hawa jamaa ni ukaskazini kwa kwenda mbele.
 
Hizo propaganda zenu za ukaskazini ni ushamba kwa kwa sasa tafuteni kitu kingine
Hakuna Sikh CHADEMA dola. Labda wabadikishwe Mwenyekiti was Chama. Nchi hii Ione hivi hivi tu, wanajua siku dola ikikamatwa na hawa jamaa ni ukaskazini kwa kwenda mbele
 
Hakuna siku ambayo CHADEMA itashika dola. Labda wabadilishe Mwenyekiti wa chama. Nchi hii Ione hivi hivi tu. Watanzania no waelewa sana, wanajua fika kuwa nchi hii ikikamatwa na hawa jamaa ni ukaskazini kwa kwenda mbele.
Hakuna Sikh CHADEMA dola. Labda wabadikishwe Mwenyekiti was Chama. Nchi hii Ione hivi hivi tu, wanajua siku dola ikikamatwa na hawa jamaa ni ukaskazini kwa kwenda mbele
 
Back
Top Bottom