Ipi siri ya Kipindi cha SHILAWADU kuanguka?

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,577
18,904
Hiki kipindi kilikuwa hot sana, kilibamba sana na kilikuwa kinapendwa na watu wengi sana. Kilikuwa kinarushwa kila Ijumaa ila kilianza kuyunga kuanzia mwaka 2017 mwishoni na hadi sasa hivi kimekufa kabisa.

Kila mtu amekuwa akisema lake kuhusu sababu za kufa kipindi, wengine wanasema kukosa Content za Diamond kwenye kipindi chao baada yakutokea bifu la Clouds na Diamond.

Sababu Diamond ndo msanii anayefuatiliwa na watanzania wengi, wengine wanasema kukosekana ubunifu kwenye kipindi chao, kifupi maneno ni mengi.

Je, wewe unaona sababu gani kuu imepelekea kufa kwa kipindi hiki?
 
Hoja kuu hapo Mkuu ni kwamba Shilawadu huwa wanaedit sana zile habari na kuzistiri sana hivyo sahizi watu wanapata habari zile kupitia mitandao ya kijamii zikiwa MUBASHARA (kumbuka video ya Gwaji boy).

Kwahiyo Mkuu suala la mitandak ya kijamii linapelekea vipindi vingi sana vya habari kusambaratika katika uso wa wafuatiliaji wa vipindi hivyo.
 
Back
Top Bottom