Ipi ni tafsiri sahihi ya Usomi na Elimu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,269
33,872
Wakati fulani hapa JF watu husema kusoma si kuelimika, hivi tofauti ya Elimu na usomi ni nini. Unawezaje kutofautisha msomi ambaye hajaelimika na mtu aliyeelimika lakini ambaye si msomi?
 
Msomi ni mtu aliyejifunza kitu katika fani fulani lakini hana uelewa wa fani zingine.

Elimu ni mchanganyiko wa fani nyingi mtu mwenye elimu anaweza kuwa aliishia darasa la saba

Lakini ana uwezo wa kutengeneza gari la mtu mwenye degree nne so elimu ni pana kuliko usomi.

Ndio maana unakuta doctor hana ujuzi wa kuendesha gari ila kijana mwenye elimu ya darasa la saba anaendesha gari kwa ustadi mkubwa.

Elimu inaunganisha vipaji vingi na mtu anayejua mambo mengi ila msomi ni matokeo ya kufundishwa kitu kimoja.

Kiufupi elimu ni kujifunza ila usomi ni kufundishwa.

Wajuzi watanirekebisha zaidi.
 
Asilimia 90 ya waliosoma Tanzania huwa hawaelimiki nililigundua hili nilipo enda TRA

Kodi yangu ya mwaka mzima ni tshs 150000 lakini mimi biashara nimeanza mwezi wa 9 nikaambiwa nilipe kodi yote ya mwaka haijalishi biashara nimeanza lini

Kanuni za kodi duniani kote inatakiwa mtu afanye biashara na apate faida ndio alipe kodi

Sasa wao walipo niambia nilipe kodi hadi ya miezi ambayo biashara haikuwepo yani mwezi January -- August wao mambo haya wameyasoma wapi

Nikaona kabisa hawa jamaa wamesoma lakini hawajaelimika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
technically umetoa maelezo yenye kufikirisha sana. Ila sijaelewa tofauti ya kujifunza na kufundishwa. Ina maana mtu anayefundishwa hawezi kujifunza kama yule anayejifunza mwenyewe bila ya kufundishwa?

live on mfano wako nimeupenda sana. Lakini hao wasomi wameshindwaje kujua kwamba haitakiwi mtu kulipa kodi kwa biashara ambayo hajaifanya? Walipokuwa vyuoni wakisomea mambo ya kodi hilo hawakujifunza?
 
Schooled (msomi) mtu aliyepitia mafunzo na ana ithibati ya hayo mafunzo
Educated (aliyeelimika) mtu aliyepitia mafunzo na mafunzo hayo yanamsaidia yeye au jamii yake au wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom