Msomi ni nani

wanabodi salaam sana.
Kuna swali kila siku najiuliza nafikiri nikiwashirikisha majibu nitayapata leo.
Jana kwenye Taarifa ya Habari ya saa mbili Usiku wanafunzi wa Vyuo vikuu ambao ni wanasisiem walikuwa wakiongea na Bwana January Makamba wakitoa matamko mbalimbali kuhusu chama chao cha CCM.ku
na neno waliokuwa wanalitumia sana kuwa " eti wao Wasomi" hawaridhishwi na mwenendo mzima wa Chama Chao.
Neno wasomi ndo linanipa shida kidogo.
Hivi watu kama Dr. slaa,Dr. Harison Mwakyembe,Tundu Lisu,Issa Shifji na wengine wengi ambao leo tunajivunia matunda ya elimu zao tutawaitaje!. Kama watu waliopo shuleni ambao bado hawajahitimu na kuonesha product za elimu yao nao wanajiita wasomi?
MI naona hawa tuwape jina linalowastahili yaani WASOMAJI. Je Wewe utawaitaje? natoa hoja
 
usomi ni kiswahili ikiwa na maana ya Elite kwa kiingereza ..hawa wanafunzi wa elimu ya juu kwa nchi maskini kama yetu ambayo wananchi wengi hawapati fursa ya kufika huko wanawekwa kwenye kundi la watu elite kwenye jamii na hapo ni wasomi..

usishangae ukiongea na Prof Baregu, Mvungi, Mwandosya, au Dr Mwaky wakakueleza kitu cha kijamii kisicho na utaalamu mahsusi na ukawa huelewi wakasema wewe unashindwa kuelewa na usomi na upeo wako wote..
 
Wasomi ni wale waliofunuliwa ufahamu. Sio lazima uwe umesoma degree. Watu kama kina Rejao , Tume ya katiba , ritz sio wasomi kwakuwa hawana ufahamu.
 
wangekua wasomi wasingekua CCM hao,huwezi ukajiita msomi alafu una kadi ya ccm.hao ni wakamilisha ratiba vyuoni.
ebu tujue perfomance yao kama inawezekana
 
Nadhani msomi, ni yule aliye ktk mchakato mzima wa kusoma. Tofautisha na mhitimu. Kubwa kabisa. Yule aliejaaliwa kuwa msomi wa kiwango cha kutukuka huwa na sifa ya kutokuwa na dharau. Hususan kwa watu ambao hayuko nao ktk taasisi yake anayofanyia mchakato wake wa kusoma, akitambua kuwa kusoma kwa kiasi kikubwa ni kujifunza kwa kuishi.

Anayetambua, msomi ni yule anaeishi maisha yake yote, akijifunza. Hususan mwenyewe, na akiheshimu wasomi wengine wanaojifunza wenyewe na kazi zao. Shaaban Robert wa Tanzania, ni mfano mmoja, na wengine wengi wapo, msomi hana kibri. Ana heshima, ana ushujaa wa kuukubali ukweli. Kinyume cha hapo, ni kinyume cha msomi. Tuseme ni limbukeni wa kitu kidogo alichomaliza kujifunza na nachobakia anakimiliki kwenye mawazo yake tu.
 
Wasomi ni wale waliofunuliwa ufahamu. Sio lazima uwe umesoma degree. Watu kama kina Rejao , Tume ya katiba , ritz sio wasomi kwakuwa hawana ufahamu.
UMEMSAHAU ALLY KOMBO AMBAYE AMEJAA ELIMU AKHERA KICHWANI hahahahah
 
.....mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii(huyo ndiye Msomi).
 
Msomi ni mtu yeyote anayeweza kuweka sahihi yake sehemu fulani (ktk karatasi).
 
ni mtu aliyepata maarifa fulani ambayo yanamuwezesha kurun maisha yakila siku kwa urahisi zaidi
 
Back
Top Bottom