Wadau tunapoenda kwenye uchaguzi hebu tukubaliane kwa pamoja tuweke ushabiki pembeni kwa maslahi ya taifa letu. Ni ILANI IPI YENYE UBORA? Kati ya hizi mbili zipitie kisha toa jibu lako
Ilani haitusaidii kuitoa CCM madarakani. Ilani nzuri ni ya chama cha Jahazi lakini mwaka huu ni wa UKAWA na rais ni Lowasa. Ilani zitatusaidia nini wakati watekelezaji ni wale wale kwa sheria zile zile na ndio maana hata CCM hawahubiri ilani zao zaidi ya kusema yale yale waliyoyatangaza miaka nane iliyopita kuwa Lowasa ni Fisadi na wakashindwa kuitekeleza kwa kumkamata.
Sasa mwaka huu tunamtaka Lowasa waliyemshindwa ili yeye awakamate wao na kuwaaibisha kwa uongo wao.
Mwaka huu ni mwaka wa wanyonge waliopigwa mabomu na kudhalilishwa na waafrika wenzao kwenye taifa lao wote kwa kupitia mgongo wa CCM.
Tumeona Makonda na Nape a
Wakizawadiwa vyeo kwa kutukana na kudhalilisha wengine.
Huu ni mwaka wa kuleta usawa na utu. Kuwaachia wale waliodhulumiwa .
Mwaka wa kumwondoa mkoloni mweusi aliyeua na kutesa kwa miaka 50 ameleta madaraja kwa watanzania kwa muda mrefu. CCM ni tatizo kubwa hatubitaji sera tunataka Elimu bora kwa watoto wetu. Kama sio elimu dunia isingekua kijiji kwa Teknolojia . Wao CCM wanawekeza familia zao kwenye Elimu na mali lakini wanatuletea sera za kupambana na waiba madawa wakati wakuu wa sekta hizo ni watoto wao waliosoma. Bila Elimu hakuna maendeleo zaidi ya mabwana na watwana. Magufuli kwa kujua umuhimu wa Elimu alisoma tena akiwa waziri na kupata phd. Leo anadharau kipaumbele cha elimu.
Usawa kwanza sera baadae.
UKAWA na Lowasa ndio ukombozi na raha ya malofa oktoba kupumua.
Tunataka mtu wa kuunganisha watu sio kutugawa kwa makundi kwa manufaa ya CCM.
Ushindi wa Lowasa ni ushindi wa vyama vyote na watanzania wote.
Ushindi wa magufuli ni ushindi wa kakikundi kadogo ka watu ndani ya CCM kwa manufaa yao na familia zao kwa mgongo wa chama.
Tumeshtuka hatuichagui CCM wala Magufuli wala wabunge wao na madiwani wao.