Inyeee ndembendembe

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Hivi Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo huwa haina muda kupitia filamu zinazotengenezwa hapa nchini kabla hazijaingia sokoni? Hii staili ya kuzuia kuonyeshwa kwa filamu baada ya mauzo kufanyika uthibiti wake unakuwaje kwa mfumo huu wa utendaji wa Serikali yetu?
Kama suala ni ukiukwaji wa maadili na uzalilishaji wa wanawake wenye "makakio majaliwa " kwani waliocheza filamu kama ya InYeee ya Kingi Majuto ni wanaume? Au ni hao hao wanawake wenye makalio husika? Ikiwa muhusika ndie ameamua kuchezea maungo yake hadharani kwa nia ya kuonyesha yale anayohisi jamii inapaswa kuona, ni nani anaedhalilishwa hapa?. Ktk utaratibu huu, Wizara inalichukuliaje kundi kama la laki si pesa, khanga moko ndembendembe ambalo nalo linafanya maonyesho adimu ktk jamii yetu ya kudhihirisha hadharani kazi ya makalio ya kike( kwa wale wa Intercontinental)
-----------


?

Mtoto wa mama yapigwa stop

Thursday, 28 April 2011 19:04

?Mwandishi Wetu
WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza imezuia kuonyeshwa filamu 5 kati ya 45 zilizokaguliwa mwezi Februari na Machi mwaka huu kutokana na kutozingatia maadili ya Kitanzania.

Filamu zilizozuiwa kuonyeshwa hadharani na kwenye vyombo vya usafiri* ni Filamu ya Mtoto wa Mama, Inye, inye Plus, Inye Ndembendembe na Inye Gwedegwede kwa mujibu wa taarifa ilyotolewa jana na bodi ya ukaguzi wa Filamu na michezo ya kuigiza hapa nchini.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Sababu za kukataliwa ni pamoja na filamu hizo kutokuwa na maudhui na maadili ya Kitanzania.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Filamu hizo zinaonyesha vitendo vya Ushoga sambamba na kudhalilisha wanawake hasa wanene kwa kugeuza miondoko yao ambayo inaamsha hisia za kingono.

"Filamu ya Mtoto wa Mama ni ya daraja ‘R’ yaani hairuhusiwi kuonyeshwa mahali popote na wakati wowote nchini Tanzania kwani inaonyesha vijana wa kiume wanaovaa na kuishi maisha ya kike (mashoga).

"Filamu hii inakiuka maadili ya Kitanzania na pia inakiuka Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza ndio mambo yasiyoruhusiwa katika filamu ikiwemo kuigiza vitendo vya Ushoga katika filamu,"ilieleza taarifa hiyo ya Bodi.

"Hali kadhalika filamu za Inye, Inye Plus, Inye Ndembendembe na Inye Gwedegwede zipo katika daraja hilo hilo kwani zinahusu vichekesho vinavyozingatia sana maumbile ya miili ya wanawake na miondoko yao ambayo inaamsha hisia za kingono.

Wakati huo huo; taarifa hiyo ilieleza kuwa Wizara hiyo imeridhia marekebisho yaliyofanywa na filamu ya Shoga Yangu ambayo hapo awali ilikuwa ikiitwa Shoga.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Marekebisho hayo yaliwasilishwa tarehe 8 Aprili 2011 na filamu hiyo baada ya ukaguzi kupewa daraja‘A’.18.

"Muonekano halisi wa kasha, matangazo na filamu yenyewe viliwasilishwa Aprili 27 na vimeridhiwa* na Wizara, filamu hiyo sasa inafaa kuangaliwa na watu wazima kuanzia miaka 18 na kuendelea,"ilieleza taarifa ya Bodi.

Taarifa hiyo pia ilieleza,"Marekebisho yaliyofanyika katika filamu hiyo ni pamoja na kipande cha bafuni kilichokuwa kikionyesha mashoga wakiwa wanaoga."

"Maneno makali yaliyotamkwa kiuhalisia yalitakiwa kutafutiwa maneno mbadala pia jina la filamu (Shoga) lilitakiwa kubadilishwa kwa kuwa halikuwa linaendana na maadili ya Kitanzania," ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa filamu hiyo ilifungiwa hapo awali kwa kuwa haikuendana na maadili ya kitanzania kwa mujibu wa Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na 4 ya mwaka 1976 na kutozingatia hatua za utengenezaji.

"Mtengenezaji haruhusiwi kuongeza wala kupunguza jambo katika marekebisho yaliyoridhiwa kama inavyoelekezwa katika Sheria 4/76* kifungu cha 19(2) a-b," ilifafanua taarifa hiyo.

Bodi hiyo ilisisitiza watunzi na watengenezaji wa filamu kuacha kutengeneza filamu bila kuwa na kibali cha Waziri mwenye dhamana ya masuala yanayohusu filamu na michezo ya kuigiza na kutoonyeha filamu yoyote bila kukaguliwa na kupewa daraja.
 
Back
Top Bottom