Boutafrica
JF-Expert Member
- Dec 11, 2014
- 953
- 2,070
Wakuu nina kifahamu kiingereza vizuri tu japo si sana ila nina matatizo kidogo kwenye hii lugha ,matatizo yenyewe ni haya:
(1)Juzi kati nilibahatika kufanya interview katika kampuni flani hivi ya kigeni,ila interview ile iliendeshwa kwa njia ya skype,yaani me nipo dar nimekaa meza moja na watu wawili (interviwers)na wa tatu ni yule mzungu wa kwenye skype.Muuliza maswali mkuu alikuwa ni yule mzungu wa kwenye skype ambaye alikuwa anaongea kutoka denmark,sasa ilikuwa mimi ni lazima nicontact direct kwenye skype,sasa kitu ambacho kilikuwa kinanipa shida ni yule mzungu matamshi yake,yaani kusema ule ukweli nilikuwa siyapati/simuelewi kabisa matamshi yake yani alikuwa anaongea kama "kajaza mlenda kooni" ilikuwa kila akiniuliza swali lazima niwageukie wale wabongo wenzangu ambao nao pia ni interviwers wanifafanulie kilichoulizwa kule kisha ndiyo natoa jibu.Nashuru Mungu nilimaliza vizuri interview ile na nimebakisha hatua chache kupata hiyo kazi,ila changamoto niliyoipata ndiyo hiyo.
(2)Kila nikiongea na mzungu yeyote yule tukiwa face to face huwa naelewa vizuri sana kila anachokitamka ila huwa napata shida sana kumuelewa mzungu akiongea akiwa kwenye tv au radio hasa ninapokuwa najaribu kufuatilia international news kwenye bbc,aljazeera au kwenye movies nk...,yaani napata maneno machache sana ,sesntence yake moja naweza kukakamata neno la mwanzo na la mwisho.Lakini cha ajabu mwarabu,muhindi au muafrica akiongea kwenye tv yan hata nisipomuangalia nisikie tu hata sauti huwa namuelewa vizuri sana,shida ni hawa akina Trump na wenzie hawa....
Sasa tatizo ni nini na nifanye nini ili kumaster hii lugha kwenye mazingira ya aina zote?