International friendly: Tanzania (Taifa Stars) vs Ivory Coast (Les Éléphants)-Updates

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,754
Heshima mbele wakuu,leo Timu yetu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) inacheza na Timu ya Taifa ya Ivory Coast(Les Éléphants) katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.Ni vizuri tukawa tukipeana updates za nini kinaendelea katika mtanange huo...

Kila la heri Taifa Stars

Nawasilisha

================
================

Matokeo ya Mwisho: Tanzania 0 - 1 Kodivaa


BAO la nahodha Didier Drogba kipindi cha kwanza limeipa ushindi Ivory Coast wa bao 1-0 dhidi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Dakika ya 37, Drogba alipachika bao hilo kwa kichwa cha kuchupia kufuatia krosi ya kiungo Emerse Fae baada ya kumzidi ujanja beki Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye alicheza vizuri jana.

Awali, mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi akiwamo Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya mawaziri wake ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na kasi zikisaka mabao ya mapema.

Baadhi ya nafasi za kufunga ambazo Stars ilizikosa ni za dakika ya 23, kupitia kwa Mrisho Ngassa aliyekosa bao akiwa na kipa Barry.

Hata hivyo muda mfupi baadaye, beki Kolo Toure aliokoa mkwaju dhaifu wa mshambuliaji huyo wa Stars mwenye kasi aliyejaribu kumchambua kipa.

Dakika ya 12, Cannavaro alimzuia Drogba aliyekuwa akielekea langoni na pia katika dakika ya 14, lango la wenyeji lilikuwa tena katika msukosuko kutoka kwa wageni hao.

Mshambuliaji Solomon Kalou naye alijaribu kumtoka Kelvin Yondani, lakini beki huyo mahiri aliutoa mpira na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Dakika ya 36, shuti la Jerry Tegete lilipaa na kutoka nje na kufuatiwa na jaribio jingine la dakika moja baadaye baada ya kiungo Nizar Khalfan anayecheza soka ya kulipwa Canada kukosa nafasi nzuri ya kuandika bao.

Tukio pekee ni la dakika ya 31, kipindi cha kwanza baada ya taa za uwanjani hapo kuzimika kwa muda mfupi, lakini zikarejeshwa na kuufanya mchezo huo uendelee bila matatizo yoyote.

Kipindi cha pili, kocha wa Ivory Coast Vahid Halilhodzic aliwatoa wachezaji wake wote 11 wa kikosi cha kwanza cha dakika 45 za mwanzo na kuingiza wengine akijaribu kuipeleka puta Stars kwa mchezo wa kasi.

Kwa dakika 10 za kipindi hicho, vijana hao wa Ivory Coast waliipeleka puta Stars, lakini mabeki walikuwa makini na imara kuokoa hatari zote.

Nafasi pekee ya kipindi hicho cha pili ni ile iliyopotezwa na Jerry Tegete ambaye aliwachambua mabeki wa Ivory Coast pamoja na kipa wao, Boubacar Barry na kuachia mkwaju ambao uligonga mwamba na kurejea dimbani.

Kipa huyo anayecheza soka ya kulipwa nchini Ubelgiji alitolewa dakika za mwisho za mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Vincent De Paul Angban ambaye ndiye mchezaji pekee katika kikosi hicho cha wachezaji 23 wa Ivory Coast anayecheza ligi ya nyumbani.

Kocha Marcio Maximo alifanya mabadiliko katika kikosi chake kipindi kwa kumtoa Kiggi Makassi na kuingia Mussa Hassan Mgosi na Nizar Khalfan akamwingiza Stephen Mwasika ambaye alionyesha umahiri mkubwa.

Pia, Maximo alimtoa Henry Joseph na kumwingiza Nurdin Bakari, kipindi cha kwanza.

Baada ya mchezo huo, baadhi ya wachezaji wa pande zote mbili walionyeshana ubabe huku Drogba na Nsajigwa wakisukumana.

Naye kiungo Abdulhalim Hamoud akikaribia kukunjana shati na mchezaji wa Ivory wakati wakielekea vyumba vya kubadilishia nguo.

Baada ya mchezo, Cannavaro alisema Ivory Coast walipata nafasi moja na kuitumia vizuri kupata bao ikilinganishwa na wao waliopata nafasi kadhaa na kuzikosa.

Naye Vicky Kimaro anaripoti kuwa wakati wakitoka uwanjani, wachezaji wa Ivory Coast wanashangiliwa na mashabiki huku askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwatawanya mashabiki kwa virungu.

Lakini, mashabiki bado wamejazana uwanjani kwenye lango kuu wakiwasubiri wachezaji wa Ivory Coast watoke vyumba vya kubadilishia nguo huku Drogba akiendelea kuwa kivutio kikubwa.

Wakati wakitoka, Drogba anatia saini vitabu vya mashabiki mbalimbali waliokuwa na hamu ya kumwona.

FFU kwa upande wao wametanda kila mahali wakiwa na zana zao tayari kwa lolote linaloweza kutokea.

Ivory Coast ambao wanajiandaa kwa fainali za Afrika wanatarajiwa kushuka dimbani tena kesho dhidi ya Amavubi ya Rwanda katika mchezo mwingine wa kujipima nguvu.

Timu hiyo imepangwa dhidi ya Ghana, Burkina Faso na Togo zikiwa Kundi B katika fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Jumapili nchini Angola.


Source: Gazeti la Mwananchi.

 
Mliopo Dar, tupeni nini kimejili na kinachoendelea katika mechi ya kirafiki kati ya timu yetu na Ivory Coast.....
 
i1375_tanzaniavsivorycoastpicture.jpg

 
Game itaanza saa 1:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Nina imani TBC watairusha live
 
Mechi inaanza 1930hrs EAT yaani saa moja na nusu usiku kwa masaa ya Tanzania. Na ticket za mechi hiyo zimeandikwa muda huo.
 
Hivi TFF inakuwaje unanunua tiketi ya 10,000 unakaa VIP?Rushwa.....kibaooo hakuna anaokaa kulingana na tiketi yake .................
 
TFF si majizi tu haya hakuna kitu pale .na hivi mweakalebela anakusanya hela ya kampeni za ubunge Iringa mbona kazi ipo
 
Na cha kushangaza zaidi, sielewi kwa nini mechi zinazochezwa uwanja wa Taifa tiketi zake haziandikwi namba za viti na eneo la kukaa wakati viti vyote uwanjani vina namba..au ndio shamba la akina Tenga, Mwakalebela na wenzake kujivunia mihela? Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
 
Game moja na nusu kwa mujibu wa tiketi yangu, hivi na shut down nielekee uwanjani,
 
Wakuu any updates??,maana kipute kinaanza kama dakika 15 zijazo
 
waungwana hizo live streaming ni kweli? mbona sioni kitu zaidi ya maneno matupu kwenye hizo link mlizotuma hapo juu?
 
Back
Top Bottom